Habari za Sabato!
Kuna ile unafikiri watu wanakuheshimu kwa kiwango cha juu. Kiasi kwamba hata ukitema shudu, pumba, ukitoa boko basi watu kwa heshima waliyonayo kwako watakustahi.
Ni kweli mtu anayekuheshimu sana hawezi kukuzomea, kukukatili, kukukatisha, kukufedhehesha. Hilo ni kweli kabisa.
Lakini kuna ile mtu unajiona wa muhimu sana. Kwamba mimi siwezi kuzomewa. Kwa niliyofanya siwezi kuzomewa. Kwa jinsi tulivyo na mahusiano yetu siwezi kumwagiwa majitaka, kupigwa mayai viza.
Sasa kumbe heshima yako sio kubwa kihivyo. Sio kama unavyofikiria, unavyodhani, kama ulivyo jidanganya.
Ndio ile unaongea utopolo, unamwaga ukoko alafu watu hawakukawizi wanakumwagia majitaka. Dadeki!
Sasa kwa vile bado huamini unafikiri labda ni bahati mbaya, unakazana kuzima jaribio la kuzomewa hapo ndipo unaharibu kabisa. Watu wanafungulia Chemba zote za jiji, mwendo wa majitaka unamwagiwa tuu.
Ni muhimu kujua hasa ukiwa kiongozi wa siasa. Heshima uliyonayo sio kubwa kama unavyojidanganya. Heshima ndogo uliyonayo jitahidi uilinde ili aibu za rejareja kama hizo zisikupate.
Usiweke rekodi mbaya kwamba uliwahi kuzomewa mbele ya halaiki, mbele ya media, watu bila kusita walikumwagia majitaka. Kwani hiyo wapinzani wako wa kisiasa wataitumia sana Huko mbeleni kama reference.
Kiufupi ni kujiharibia CV kwamba haikubaliki kivile.
Mtu mwenye kupendwa na kuheshimiwa sana kamwe hawezi kuzomewa. Watu lazima wamvumilie, wamstahi.
Wataishia kusema mzee kazingua lakini sio kwa kummwagia ukoko na majitaka.
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam