Unapozomewa ni tafsiri watu hawakuheshimu kama unavyofikiria. Hawakuonei haya

Unapozomewa ni tafsiri watu hawakuheshimu kama unavyofikiria. Hawakuonei haya

Habari za Sabato!

Kuna ile unafikiri watu wanakuheshimu kwa kiwango cha juu. Kiasi kwamba hata ukitema shudu, pumba, ukitoa boko basi watu kwa heshima waliyonayo kwako watakustahi.

Ni kweli mtu anayekuheshimu sana hawezi kukuzomea, kukukatili, kukukatisha, kukufedhehesha. Hilo ni kweli kabisa.

Lakini kuna ile mtu unajiona wa muhimu sana. Kwamba mimi siwezi kuzomewa. Kwa niliyofanya siwezi kuzomewa. Kwa jinsi tulivyo na mahusiano yetu siwezi kumwagiwa majitaka, kupigwa mayai viza.

Sasa kumbe heshima yako sio kubwa kihivyo. Sio kama unavyofikiria, unavyodhani, kama ulivyo jidanganya.

Ndio ile unaongea utopolo, unamwaga ukoko alafu watu hawakukawizi wanakumwagia majitaka. Dadeki!

Sasa kwa vile bado huamini unafikiri labda ni bahati mbaya, unakazana kuzima jaribio la kuzomewa hapo ndipo unaharibu kabisa. Watu wanafungulia Chemba zote za jiji, mwendo wa majitaka unamwagiwa tuu.

Ni muhimu kujua hasa ukiwa kiongozi wa siasa. Heshima uliyonayo sio kubwa kama unavyojidanganya. Heshima ndogo uliyonayo jitahidi uilinde ili aibu za rejareja kama hizo zisikupate.

Usiweke rekodi mbaya kwamba uliwahi kuzomewa mbele ya halaiki, mbele ya media, watu bila kusita walikumwagia majitaka. Kwani hiyo wapinzani wako wa kisiasa wataitumia sana Huko mbeleni kama reference.

Kiufupi ni kujiharibia CV kwamba haikubaliki kivile.

Mtu mwenye kupendwa na kuheshimiwa sana kamwe hawezi kuzomewa. Watu lazima wamvumilie, wamstahi.

Wataishia kusema mzee kazingua lakini sio kwa kummwagia ukoko na majitaka.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Alafu dj alikua na makusudi mdau anazomewa dj anapiga aibu utaona wewe
 
Uko sahihi kabisa. Kilichobakia sasa ni wananchi kuonyesha hisia za kwa vitendo. Hii hatua inakuja, hasa ikizingatiwa kuwa CCM wenyewe wanaiharakisha kwa mambo wanayofanya baada ya kulewa madaraka. Wanajioana kwamba ndiyo wenye haki ya kufanya lolote hata kuua. Nlishangaa sana hicho kimama kinasema eti serikali haiamrishwi cha kufanya.
KIBURI ndio hatua ya mwisho ya mshenzi kuelekea kwenye anguko kuu
 
Walivyo wajinga watajibu mapigo. Ki-vipi? Wataandaa hadhara nyingine, watapandikiza ma-chawa wengi. halafu jina la Samia likitajwa, watarukaruka kwa furaha na vigelegele kuonyesha kuwa ''anapendwa''. Serikali ya wapumbavu hii!
Kwa kizazi hiki sio rahisi hivyo watajaribu ila ni ngumu

Kuweka divai mpya kwenye kiriba cha kale ni shida.!

Kuweka kiraka kipya kwenye vazi kukuu ni msiba.!
 
Kwa kizazi hiki sio rahisi hivyo watajaribu ila ni ngumu

Kuweka divai mpya kwenye kiriba cha kale ni shida.!

Kuweka kiraka kipya kwenye vazi kukuu ni msiba.!
Nakubaliana na wewe. Ila wao walivyo wajinga, hawana hizo busara.
 
inawezeka a tatizo ni UJUMBE aliokuwa anataka kuufikisha wa mama anaupiga mwingi
kwa hadhira ile(WRONG PLACE IN A WRONG TIME)
 

Attachments

  • images - 2025-03-30T152501.267.jpeg
    images - 2025-03-30T152501.267.jpeg
    10 KB · Views: 13
Babalevo mjanja sana, hadi nalala sijamsikia kabisa akichomkea siasa siasa.
Yule sio mwenzao na wanamjuwa ni mtu wa haki, amejipenyeza tu pale kwasababu za njaa na kujijenga, tunza manenoyangu, hatapata nafasitena ya kwenda mjengini.
 
Ishikawa kipengele.
Hapo tricks isingekuwa hiyo.

Kazi za heshima hupewa watu wa heshima.
Hiyo kazi ya kumtaja Rais Samia angepewa Mwijaku au Dotto watu wa kazi cha lawama, kutukanwa kama sehemu ya kupima upepo.

Lakini mtu kama Mwana FA kuwa mtu wa majaribio kwa kazi hiyo tayari rekodi mbaya ameshaiweka. Kuzomewa. Sio jambo dogo katika mambo ya heshima
Lakini pale alizomewa boss wake bana
 
Waandaaji wanatakiwa kukamatwa haiwezekani uandae tamasha la kuidogosha AWAMU. Wameandaa tamasha wakaleta na wanaharakati wanaolipwa na mabeberu kuja kupinga kutajwa kwa AWAMU mbele ya hathiri hii haikubaliki. AWAMU lazma itajwe popote penye kusanyiko 😙😙 ilitakiwa milango ifungwe kila atakae toka viboko viwil
Mkuu ukinuka kimavi, hasa cha Okt29, ujue hakuna perfume itakiondoa hicho kimavi.
 
Back
Top Bottom