Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

Great Thinkers habari za mchana.

Nimeona Ndg zetu hususan wa CHADEMA wakihangaika sana mitandaoni kujua Rais Magufuli yuko wapi. Nimeshangaa kwa kweli 'wonders will never end"! Nina maswali yafuatayo:-

1. Je, Mnamtambua Rais Magufuli kama Rais wa Tanzania?

2. Mmelisha wananchi matango pori kila aliyekula anacheua kwa njia ya mdomo au haja kubwa au zote mbili. Na mpaka sasa mmeshindwa kuonesha ushahidi wowote uwe wa picha ya mgando au video fupi. Nyie mlivyo na kiherehere mmekwama wapi kwenye ushahidi?

3. Mmeanza kutangaza habari kuwa Rais Magufuli amelazwa Nairobi. Ulinzi umeimarishwa hali ni tete. Mkabadili gia angani mkasema kahamishiwa India na amefia huko. Hivi kweli hata picha moja mmeshindwa kupata? Hata ka video tuu

4. Rais wa Korea alizushiwa kifo na hakutoka zaidi ya miezi. Siku alipojitokeza ikawa aibu kubwa kwa wabaya wake, wambea, waongo, wazandiki nk Na mjiandae kwa aibu hiyo.

5. Unang'ang'ania ajitokeze, halafu ndio utaanza kumpenda na kuondoa chuki uliyonayo! Kujitokeza kwake kutakusaidia nini?

6. Kumekuwa na utamaduni wa kuwachukia viongozi wanaokuwa madarakani na kamwe haitawasaidia chochote. MLIMTUKANA SANA JK NA KUMZUSHIA VIFO TENA SIO MARAMOJA. Leo ghafla amegeuka kipenzi chenu! Acheni unafiki na uzandiki.

7. Changamoto za kisiasa na uanaharakati haijaanza awamu ya tano. Tatizo mna akili za kuku mnasahau mapema sana. Ukiorodhesha matukio ya ajabuajabu kwenye kila awamu utasemaji leo awamu ya tano ndio imezidi! Tulizeni akili ongeeni kama watu mlio timamu. Uchaguzi 2020 umeisha vizuri kuliko wakati wowote wa Historia tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vya vyama vingi Tanzania.

8. Katika maisha haijawahi kutokea kiongozi akapendwa na watu wote. Hata Mungu alisalitiwa na malaika theluthi moja! Tena wasaliti huwa wana kelele mingi sana! Endeleeni na kelele zenu kwani "DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA".

9. CHUMA KIPO IMARA NA SIONI SABABU YA KUKILAZIMISHA ETI ATOKE SABABU YA KELELE ZA KASUKU! NOPE!!!!

10. Hivi hamuoni wananchi wanavyowapuuza. Watu wanaendelea na kazi zao. Na Serikali inaendelea na kazi kama Mhe. Majaliwa Waziri Mkuu alivyoeleza jana. Mlianza ooh! Serikali ipo kimya!! Serikali kupitia Mtendaji Mkuu ambaye ni PM ameongea mmeanza tena oooooh! Aongee mwenyewe tumuone. Then what

11. Balozi wa Namibia Mhe. Dr. Kipilimba alipohojiwa na Reuters jana ameeleza Rais yupo salama kabisa na anachapa kazi. Sasa mnataka nini? Hahaaaa! Kuna wanaume mwaka huu MMTATAGA! Maana sio kwa kiherehere hicho!

12. MLIMZUSHIA MHE. MPANGO KUWA KAFA MKAAIBIKA, MKAJA KWA SABAYA, MKAJA KWA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU BILALI nk

Mlipoona kimya na wananchi WAMEWAPUUZA mkajiyengenezea tukio la Mrema na Mbowe. Mrema akajitokeza huku akisisitiza na Rais Magufuli ajitokeze. Sinema ikabuma! Rudini studio mpaka sasa mmefeliiii!

13. Mwisho Zaburi ya 35 na 109 (Psalms 35 and 109) ndiyo majibu wenu wote mnaomwazia Rais Magufuli mabaya. Jitahidi uisome!! Tuendelee kuiombea Nchi yetu na Rais wetu kipenzi Magufuli, na viongozi wote! MUNGU HAJAWAHI KUSHINDWA!!

Muda ni mwamuzi mzuri! Mwisho wa ubaya ni AIBU!i

Queen Esther
Wacha kutiririsha masuali mengi hapa! hebu jibu hili
1. Umemuona mheshimiwa kanisani sunday hii? umeona clip zake za sunday kanisani wiki hii?
2. Unajua ni kwa nini mheshimiwa ameshindwa kuhudhuria virtual conference ya wakuu wa nchi za EAC?
3. Kwa nini imechukua zaidi ya wiki nzima kwa serikali kukanusha uvumi uliopo?

Tafuta majibu hayo, halafu utaweza kujijibu mtiririko wa masuali uliyoyaleta hapa.
 
Aisee
Hakuna Mtihani mgumu kama kuridhisha Watu...Hata mitume walishindwa

Raisi MAGUFULI usitoke nje kutaka kuwaridhisha maana hautaweza

Ila ujue hapangiwi wala hajaribiwi. Pia ni chuma kweli kweli; siamini kama anahitaji kutetewa kwa nguvu na jazba kiasi hiki.
 
Hata kama hatambuliki lakini anatumia kodi zetu lazima tuhoji kama yupo hai au kafa au anaumwa lazima tujue hili si ombi ni takwa la kikatiba
KUMBE SASA HIVI MNAMTAMBUA KUWA NIKIONGOZI KWA MJIBU WA KATIBAA?? UFIPANI BILA SHAKA MUMEVURUGWA. SITAKI NATAKA NI TABIA ZA JINSIA FLANI. HAAAA HAAAA.
 
Ndiyo hawamtambui lakini kwa vile kalazimisha kuwa rais na kula pesa zetu. Basi wao CHADEMA wanayo haki ya msingi ya kumuuliza yupo wapi. Sisi wananchi ndiyo waajiri wake, au wewe hukuombwa kura?

Hakuna rais aliyekuwa wa ovyo kama huyu na haitatokea kwenye historia ya nchi yetu. Watu wanalia nchi nzima kwa kuumizwa na utawala huu dhalimu
Kwani hamlalii kuhangaikia alielazimisha matokeo kuwa raisi?? Au mnamtambua kwa sasa?? Mumeeneza uongo hadi vyombo vyote mumewatapeliii, nao pasipokujua kuwa nyie nimatapeliii wakafakamia kutangaza uongo. Vyombo vya habari vya kimataifa mumevitapeli vyakutoshaa
 
Babu jibu swali rahisi saana na nyongeza yake!!
Rais yupo wapi?
Je ana hali gani kiafya?
 
Kumekuwa na utamaduni wa kuwachukia viongozi wanaokuwa madarakani na kamwe haitawasaidia chochote. MLIMTUKANA SANA JK NA KUMZUSHIA VIFO TENA SIO MARAMOJA.

Wewe muongo hakuna hata siku moja wakati wa utawala wake mkwere alizushiwa kifo!!! Alipougua tezi dume wananchi hatukufichwa na ndio maana kia kona ya nchi watu walikuwa wanamuombea mpaka akapona!!! Onyesha ushahidi kuwa JK alizushiwa kifo? Mnahangaika kutaka kumfananisha Jiwe na watangulizi wake; huko nyuma hakuna kiongozi hata mmoja aliyeugua wananchi wakasherekea!!!
 
Wewe muongo hakuna hata siku moja wakati wa utawala wake mkwere alizushiwa kifo!!! Alipougua tezi dume wananchi hatukufichwa na ndio maana kia kona ya nchi watu walikuwa wanamuombea mpaka akapona!!! Onyesha ushahidi kuwa JK alizushiwa kifo? Mnahangaika kutaka kumfananisha Jiwe na watangulizi wake; huko nyuma hakuna kiongozi hata mmoja aliyeugua wananchi wakasherekea!!!
Umenikumbusha kuna Rais WA Nchi jirani alimletea mbofumbofu Mkwere tuliungana humu wote kumshambulia. Siku anaelezea ugonjwa wake nilitaka kulia. Hakuna mpinzani aliwahi kumwombea kifo, nyuzi zipo azilete.
 
Wewe muongo hakuna hata siku moja wakati wa utawala wake mkwere alizushiwa kifo!!! Alipougua tezi dume wananchi hatukufichwa na ndio maana kia kona ya nchi watu walikuwa wanamuombea mpaka akapona!!! Onyesha ushahidi kuwa JK alizushiwa kifo? Mnahangaika kutaka kumfananisha Jiwe na watangulizi wake; huko nyuma hakuna kiongozi hata mmoja aliyeugua wananchi wakasherekea!!!
Kumbe naongea na mtoto mdogo! Nilidhani wewe ni mkubwa mwenzangu! Endelea kunyonya maziwa na mama akukorogee uji wa kutosha. Jitahidi kulala mapema ukuwe mtoto mzuri eeeee!
 
Back
Top Bottom