Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

mbona akila mahindi barabarani huwa mnatuonyesha, akinywa kahawa migahawani mnatuonyesha, akiota jua kwenye mawe mnatuonyesha? kuna shida gani mkatuonyesha na anavyopiga kazi sasa
Huwa tunaamua kufanya hivyo Ila siyo bavicha kutupangia cha kufanya[emoji23][emoji23]
 
Mleta mada uwezo wako wa kufikiri upo chini sana, kikubwa kinachoendelea kwa sasa siyo kutambua au kutotambua cheo,kikubwa ni kwamba watu hao wanafurahia majanga kumpata bwana mkubwa. Fikiria kwa upana.
Mimi kinachoniogopesha ni kwamba mpango wa kuamia Dodoma hautafanikiwa,utaishia katikati uku mabilioni ya fedha yakiwa yameshatumika.
Hahaha acha kubeti kwenye siasa....bakia huko huko kwenye bongo muvi!
 
Kwani ameamuka?
KWani alikuwa amelala wapi...NAirobi, India, Mloganzila..Bado unaamini maneno ya kigogo hadi sasa hivi...ubongo wako ni zawadi kubwa kutoka kwa muumba, acha kuwapa akina Lissu wakushikie hicho kiungo, dunia ni ndogo hii!
 
Unawasemea wananchi wapi? Hakuna mwananchi mwenye Akili timamu atapuuza juu ya ukimya wa Serikali kuhusu afya ya Rais, umejitahidi kuandika ujinga ukijua utapata Uteuzi hakuna uteuzi tena nafasi zote zimejaa, kapilimba yupo Namibia na Rais yupo kwingine? na huyo kapilimba siyo mungu nani atamwamini? Rais mwenyewe hakumwamini akamvua cheo kikubwa na kumtupia ubalozi, acha kusaka uteuzi kwa njia haramu za kishetani, Tambua kuwa watanzania wameamka wanajua mbivu na mbichi wenyewe hawataki CCM kuwapangia cha kusikia
 
Hivi JPM nani anampenda zaidi yako na akina polepole. Huku mtaani watu wameshajiandaa kunywa bia wakisikia amekata Moto.
Watu wote waliobambikiwa kesi, kufungiwa biashara, Account, kuporwa kura kwenye chaguzi mbalimbali wana jambo lao moyoni
 
Maisha yamekuwa magumu sana,,, Raia tumeanza kuchukiana wenyewe...


Ila mkuu jipe muda,,,, Ukweli huwa unajitenga na Uongo...
Japo tulipofika ni pabaya
 
Hii ilianza toka kwa Kikwete huko ile 2010 walisema hawamtambui ila baadaye wakamtambua,wanachangamsha tu habari za siasa kama unavyoona wasanii wetu wanavyochangamsha kwa kufanya kiki hivyo usiwachukulie serious.
 
Mleta mada ni mjinga sana alijua watu wamelala ataandika ujinga ili polepole akiona amsaidie kupata Uteuzi
 
Back
Top Bottom