Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

Unasema humtambui kiongozi halafu unalalamika hujamuona

Kwinini unaandika manamba mengi lkn point ya msingi huna!!
Point ni tusiviongelee tusivyokuwa na ushahidi wake na tusishabikie matatizo yampatayo mtu baaasi. Vingine ni viumbea vyakusutana sutana!!

Mwisho...tupambane na korona kwa userious kama wenzetu,maisha ya kilammoja nimuhimu sana na si kila mmoja atapozidiwa anauwezo kwenda kutibiwa nje ya nchi!!
Kenyata (mzee wa wine kuliko chachi) alisema "lazima tuyalinde maisha ya watu kwanguvu zote,uchumi unaweza kufufuliwa lakini MTU akifa hatuwezi kumfufua"
Tujifunze bila ushabiki wakijinga!!!
#hapa kazi na tija!! Sio kazi tuu!!!!
 
Alafu eti kundi hili linalo zusha uzushi ndio katiyao angetoka rais wanchi???

Kwa coments zotenilizo soma tangu huu uzushi uchwara ulivyo anzishwa dhidi ya Jembe, CCM itatawala milele hapa Tanzania.

Kwamba serikali imekaa kimya haisemi rais yukowapi.
PM akajitokeza kuongea, lakini bado watu hawariziki.

Najiuliza serikali gani ilitakiwa kutoa tamko kuhusu huu uzushi kama PM pia haeleweki??

Nimegundua kumbe walio leta huu uzushi uchwara na wanao taka majibu kuhusu rais alipo ni wahunitu.
 
Queen Ester; Covid-19 ipo endelea kuchukua tahadhari! Taarifa kamili utazipata very soon!
 
Mi CCM na mi chadema ndio imelifikisha taifa hapa tulipo, watu wapuuzi sana nyie.
 
Haya maelezo yote ni kuhusu hilo jizi la kura?
 
Great Thinkers habari za mchana.

Nimeona Ndg zetu hususan wa CHADEMA wakihangaika sana mitandaoni kujua Rais Magufuli yuko wapi. Nimeshangaa kwa kweli 'wonders will never end"! Nina maswali yafuatayo:-

1. Je, Mnamtambua Rais Magufuli kama Rais wa Tanzania?

2. Mmelisha wananchi matango pori kila aliyekula anacheua kwa njia ya mdomo au haja kubwa au zote mbili. Na mpaka sasa mmeshindwa kuonesha ushahidi wowote uwe wa picha ya mgando au video fupi. Nyie mlivyo na kiherehere mmekwama wapi kwenye ushahidi?

3. Mmeanza kutangaza habari kuwa Rais Magufuli amelazwa Nairobi. Ulinzi umeimarishwa hali ni tete. Mkabadili gia angani mkasema kahamishiwa India na amefia huko. Hivi kweli hata picha moja mmeshindwa kupata? Hata ka video tuu!

4. Rais wa Korea alizushiwa kifo na hakutoka zaidi ya miezi. Siku alipojitokeza ikawa aibu kubwa kwa wabaya wake, wambea, waongo, wazandiki nk Na mjiandae kwa aibu hiyo.

5. Unang'ang'ania ajitokeze, halafu ndio utaanza kumpenda na kuondoa chuki uliyonayo! Kujitokeza kwake kutakusaidia nini?

6. Kumekuwa na utamaduni wa kuwachukia viongozi wanaokuwa madarakani na kamwe haitawasaidia chochote. MLIMTUKANA SANA JK NA KUMZUSHIA VIFO TENA SIO MARAMOJA. Leo ghafla amegeuka kipenzi chenu! Acheni unafiki na uzandiki.

7. Changamoto za kisiasa na uanaharakati haijaanza awamu ya tano. Tatizo mna akili za kuku mnasahau mapema sana. Ukiorodhesha matukio ya ajabuajabu kwenye kila awamu utasemaji leo awamu ya tano ndio imezidi! Tulizeni akili ongeeni kama watu mlio timamu. Uchaguzi 2020 umeisha vizuri kuliko wakati wowote wa Historia tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vya vyama vingi Tanzania.

8. Katika maisha haijawahi kutokea kiongozi akapendwa na watu wote. Hata Mungu alisalitiwa na malaika theluthi moja! Tena wasaliti huwa wana kelele mingi sana! Endeleeni na kelele zenu kwani "DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA".

9. CHUMA KIPO IMARA NA SIONI SABABU YA KUKILAZIMISHA ETI ATOKE SABABU YA KELELE ZA KASUKU! NOPE!!!!

10. Hivi hamuoni wananchi wanavyowapuuza. Watu wanaendelea na kazi zao. Na Serikali inaendelea na kazi kama Mhe. Majaliwa Waziri Mkuu alivyoeleza jana. Mlianza ooh! Serikali ipo kimya!! Serikali kupitia Mtendaji Mkuu ambaye ni PM ameongea mmeanza tena oooooh! Aongee mwenyewe tumuone. Then what!!!

11. Balozi wa Namibia Mhe. Dr. Kipilimba alipohojiwa na Reuters jana ameeleza Rais yupo salama kabisa na anachapa kazi. Sasa mnataka nini? Hahaaaa! Kuna wanaume mwaka huu MMTATAGA! Maana sio kwa kiherehere hicho!

12. MLIMZUSHIA MHE. MPANGO KUWA KAFA MKAAIBIKA, MKAJA KWA SABAYA, MKAJA KWA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU BILALI nk

Mlipoona kimya na wananchi WAMEWAPUUZA mkajiyengenezea tukio la Mrema na Mbowe. Mrema akajitokeza huku akisisitiza na Rais Magufuli ajitokeze. Sinema ikabuma! Rudini studio mpaka sasa mmefeliiii!

13. Mwisho Zaburi ya 35 na 109 (Psalms 35 and 109) ndiyo majibu wenu wote mnaomwazia Rais Magufuli mabaya. Jitahidi uisome!! Tuendelee kuiombea Nchi yetu na Rais wetu kipenzi Magufuli, na viongozi wote! MUNGU HAJAWAHI KUSHINDWA!!

Muda ni mwamuzi mzuri! Mwisho wa ubaya ni AIBU!

Queen Esther
Amekufa
 
Propaganda zilizojaa utopolo mtupu.
The Bible says, " Mpende adui yako na umwombee"
Magufuli alishatangaza uadui na Wapinzani na wapinzani wanajua Maguguli hawapendi. Lakini wao wanataka kumwombea adui Magufuli. Ili umeombee adui ni LAZIMA UJUE YUKO WAPI NA ANA TATIZO GANI ILI ULIOMBEE/UMWOMBEE!!
Hivo CHADEMA NA RAIA WOTE WALIOATHIRKA NA UTAWALA WA JIWE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WANA HAKI YA KUTAKA KUJUA ALIPO ADUI YAO ILI WAENDELEE KUMWOMBEA MUNGU ASKIE NA AJIBU MAOMBI.
Ni hayo tu kwa sasa!!
Hata wafanyabiashara waliofungiwa biashara zao, Account zao, kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wengine kuporwa pesa zao, madini yao Airport na mipakani nao wanataka kujua alipo Rais wao ili na wao wamuombee apone haraka
 
Isijekuwa wasio julikana washamteka?mbona maneno yamekuwa teleee
 
Endeleeni kungoja kama fisi anayesubiri mkono udondoke! Katika kungoja kwenu msitikise na wengine.

Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili! Uwe na uhakika siku Rais atakapojitokeza hata akisema amewasamehe waliomzushia bado ukumhuke amesimama na andiko linalosema KISASI NI CHA MUNGU!

Chadema wamefanywa nini kwenye uchaguzi wa 2020. Labda huijui Chadema na waliyoyapitia kabla ya kuingia awamu ya tano. Kamtafute Dr. Slaa atakwambia Chadema ilipotoka, ilipo na iendako. Kazi za Rais Magufuli zimewafunika. Mmebaki kutamba mitandaoni. Wananchi walio wengi vijijini hawawafahamu! Mtasubiri sanaaaaaa!
Wananchi hawajaikataa chadema hata uchaguzi mkuu waliichagua chadema lakini Polisiccm Tumeccm wakurugenziccm na wewe mkafanya uchakachuaji mkapora haki za wapiga kura kwa njia haramu za kishetani, ni mungu yupi unamsemea? Hakuna mungu anakubali uonevu wa kupora haki za wapiga kura, kufunga biashara, Account za watu kuwapora mali zao kuwabambikia kodi, kesi na uonevu mwingineo kibao.
 
huyo akamatwe poa ni mchochoezi wa kupandikiza taharuki kwa wananchi wasio jua lolote.
tabia hii ikiachiwa ni hatari sana, last time walizusha wakaachiwa safari hii wasipuuzwe wakamatwe na hatua kali zichukuliwe, hakuna aliye juu ya sheria.
Huu upumbavu wa kukamata kamata watu hovyo hovyo kwa uonevu wa kishamba ndiyo imepelekea chuki kubwa kwa utawala wako wa kidikteta, acheni huo uovu wa kuonea watu kwa kutumia vyombo vya dola kwani unazidi kuongeza chuki dhidi ya utawala wako
 
Isijekuwa wasio julikana washamteka?mbona maneno yamekuwa teleee
Wasiojulikana wengi wamekufa kwa kusomewa Albadiri ama kwa adhabu ya mungu hata aliyempiga Tundu lisu risasi alikufa kule mbeya kwa ajali na wengi wamepata mitihani mingi ya kidunia
 
Back
Top Bottom