GE2025 Unasema unadai haki halafu muda huohuo unasema tar 29 utaifuta CCM. Je, utakuwa umewatendea Haki wanaccm?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Mpo salama!

1. Sisi watibeli tunachozingatia ni Haki, Haki kwa Kila mmoja. Bila kujali chama chake, itikadi yake, kabila lake au dini yake.

2. Mara nyingi nawasikia wanaharakati wanaosema wanapigania Haki, kama kina Mange Kimambi na wengineo. Hata humu JF wakisema wanapigania Haki lakini muda huohuo wanataka kukifuta chama cha CCM. Jambo ambalo linakinzana na Haki.

3. Ndugu zangu, unafuta ccm na wanaccm unawapeleka wapi?

Au unafuta Chadema na wanachadema unawapeleka wapi?
Ni kuwakosea haki.

4. Hoja kuu iwe kupigania haki na usawa wa makundi yote na vyama vyote ndani ya jamii na taifa.
Ili iwe hiyari ya watu kuchagua wawe chama kipi.

Hicho ndicho hata sisi watibeli tunakitaka na kukipigania.

5. Kwa sababu kama chadema wakiwa na mtazamo wa kufuta ccm. Siku wakiingia madarakani tutaanza tena hapa kukimbizana, tukipigania Haki za CCM na wanachama wake.

6. Tunajua watu wabaya wapo vyama vyote na watu wema wapo vyama vyote pia.

7. Naona makosa ya kiufundi yanayofanywa na wanaohamasisha maandamano hiyo tar 29 ni kusema ndio mwisho wa CCM. Na hapo wanatenga kundi kubwa la wananchi ambao bado wanaamini kwenye ccm.

8. Kosa jingine ni kusema hawamtaki Samia. Humtaki Samia kwani yeye sio mtanzania kulwa anahaki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya nchi hii kisheria.
Hoja kuu iwe Reforms kwenye tume ya uchaguzi kutoa uwanja sawa kwa vyama vyote katika uchaguzi mkuu.
Hiyo ni haki na mapambano ya kizalendo. Lakini sio useme tuu hatumtaki Samia.

Sasa unatofauti gani na hao wanaochagua kimabavu wapinzani wa kushindana nao. Kwamba Mpina asipite huko ili nisipambane naye. Au muweke ndani Lisu ili asinisumbue kwenye kinyang'anyiro. Tofauti yenu ni ipi?

9. Tunachotaka ni HAKI.
Haki kwa wote.

10. Kwamba mtu kuwa Chadema iwe ni haki yake ikiwa amechagua hivyo. Na asilazimishwe vinginevyo.
Chadema waheshimu uamuzi wa mtu kuwa CCM na sio kumdhalilisha, kumdharau, kumtolea maneno ya dhihaka. Huko ni kuingilia haki za wengine.
Haina tofauti na CCM wanaotumia nguvu kuwadhibiti upinzani.

11. Upiganaji wa Haki usibebe mihemko na mitazamo ya kisiasa au kidini. Ubebe utu na uzalendo wa taifa mbele.
Hivyo ndivyo tutapiga hatua.

12. Vinginevyo tutakuwa tunapig marktim tuu

Tupo!

Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Upo mda utafika haki haitaombwa itachukuliwa tu

Shida ipo kwenye kutafsiri hiyo haki.
Kila mmoja anaweza kujiona anahaki kuliko mwingine na hapo vurugu ndio zitakuwa kubwa na mwenye nguvu ndiye atashinda badala ya haki ya kweli kushinda.

Unajua hata wahalifu hujiona wanahaki ya kufanya wanayofanya?
 
Aisee
Mmeanza kutukimbia?
Kwahiyo utaandamana au una familia na ndugu wanaokutegemea ?
 
Ipo haki ya kweli mbele tuwe na imani ya turajiayo
 
Animal Farm hii ...Unaweza kupigania haki ikiwa anaekudhulumu ana backup ya CCM ?
 
Aisee
Mmeanza kutukimbia?
Kwahiyo utaandamana au una familia na ndugu wanaokutegemea ?

Hatuwezi kukimbia watanzania wenzetu lakini lazima tuwekane sawa.
Sio maandamano ya kudai haki kumbe upande mwingine ni kuvunja haki za watu wengine.
Huo ndio msingi wa hoja.

Unaandamana unaitoa ccm kwa maandamano. Next time ccm nao wanaandamana kuitoa chadema. Hivyohivyo.
 
Ni sahihi chama cha kifashisti kufutwa
 
Unadili vipi na chama ambacho hakiamini katika haki za wapinzani/washindani wake kuchagua viongozi wanaowataka?
Kama wewe ni timu pinzani utadili vipi na timu inayokuja uwanjani na refa wake, sheria zake na matokeo yake mfukoni ?
 
Ni sahihi chama cha kifashisti kufutwa

Na kile unachosema ni chama cha kifashisti fikiria kinamtazamo kama wako. Kwamba chama chako ni chama cha kifashisti. Kinataka kifute chama chako kitakutendea haki?
 
Unadili vipi na chama ambacho hakiamini katika haki za wapinzani/washindani wake kuchagua viongozi wanaowataka?
Kama wewe ni timu pinzani utadili vipi na timu inayokuja uwanjani na refa wake, sheria zake na matokeo yake mfukoni ?

Namna ya kudili nacho ni maandamano makali yenye kudai haki sawa na sio kukifuta. Kwa sababu sio kila mwanachama wa ccm anatabia za ukandamizaji.

Na sio kila mwanaupinzani ni mwadilifu

Hoja yangu unaipata lakini
 
Na kile unachosema ni chama cha kifashisti fikiria kinamtazamo kama wako. Kwamba chama chako ni chama cha kifashisti. Kinataka kifute chama chako kitakutendea haki?
Ndiyo kama itakuwa mchakato wa kukifuta chama ni kupitia mahakama huru.
 
Basi unaimani potofu.
Unaamini kwamba kuna chama hapa tz hakina wahalifu? Wadhulmaji wakubwa?
Swali lako lilikuwa ni wakandamizaji, sijui suala la uhalifu limetokea wapi.
Chama kinaweza kuwa na baadhi ya watu wachache wadhulumaji wa haki halafu pia chama kizima kinaweza kikawa ni wadhulumaji wa haki.
 
Namna ya kudili nacho ni maandamano makali yenye kudai haki sawa na sio kukifuta. Kwa sababu sio kila mwanachama wa ccm anatabia za ukandamizaji.

Na sio kila mwanaupinzani ni mwadilifu

Hoja yangu unaipata lakini
Mwanachama gani wa CCM asiye na tabia za ukandamizaji? Unaweza kuwa na mfano hata mmoja?
 
,😀😀😀😀
Unakosea sana mkuu.

Unajua kuwaona wengine wanamakosa kuliko wewe ni moja ya ishara ya kiburi.
Maana wanaccm wengine nao wana mtazamo huohuo kuwa wanachama wa vyama vingine ni wahalifu ndio maana unaona yanayotokea
 
Back
Top Bottom