Mpo salama!
1. Sisi watibeli tunachozingatia ni Haki, Haki kwa Kila mmoja. Bila kujali chama chake, itikadi yake, kabila lake au dini yake.
2. Mara nyingi nawasikia wanaharakati wanaosema wanapigania Haki, kama kina Mange Kimambi na wengineo. Hata humu JF wakisema wanapigania Haki lakini muda huohuo wanataka kukifuta chama cha CCM. Jambo ambalo linakinzana na Haki.
3. Ndugu zangu, unafuta ccm na wanaccm unawapeleka wapi?
Au unafuta Chadema na wanachadema unawapeleka wapi?
Ni kuwakosea haki.
4. Hoja kuu iwe kupigania haki na usawa wa makundi yote na vyama vyote ndani ya jamii na taifa.
Ili iwe hiyari ya watu kuchagua wawe chama kipi.
Hicho ndicho hata sisi watibeli tunakitaka na kukipigania.
5. Kwa sababu kama chadema wakiwa na mtazamo wa kufuta ccm. Siku wakiingia madarakani tutaanza tena hapa kukimbizana, tukipigania Haki za CCM na wanachama wake.
6. Tunajua watu wabaya wapo vyama vyote na watu wema wapo vyama vyote pia.
7. Naona makosa ya kiufundi yanayofanywa na wanaohamasisha maandamano hiyo tar 29 ni kusema ndio mwisho wa CCM. Na hapo wanatenga kundi kubwa la wananchi ambao bado wanaamini kwenye ccm.
8. Kosa jingine ni kusema hawamtaki Samia. Humtaki Samia kwani yeye sio mtanzania kulwa anahaki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya nchi hii kisheria.
Hoja kuu iwe Reforms kwenye tume ya uchaguzi kutoa uwanja sawa kwa vyama vyote katika uchaguzi mkuu.
Hiyo ni haki na mapambano ya kizalendo. Lakini sio useme tuu hatumtaki Samia.
Sasa unatofauti gani na hao wanaochagua kimabavu wapinzani wa kushindana nao. Kwamba Mpina asipite huko ili nisipambane naye. Au muweke ndani Lisu ili asinisumbue kwenye kinyang'anyiro. Tofauti yenu ni ipi?
9. Tunachotaka ni HAKI.
Haki kwa wote.
10. Kwamba mtu kuwa Chadema iwe ni haki yake ikiwa amechagua hivyo. Na asilazimishwe vinginevyo.
Chadema waheshimu uamuzi wa mtu kuwa CCM na sio kumdhalilisha, kumdharau, kumtolea maneno ya dhihaka. Huko ni kuingilia haki za wengine.
Haina tofauti na CCM wanaotumia nguvu kuwadhibiti upinzani.
11. Upiganaji wa Haki usibebe mihemko na mitazamo ya kisiasa au kidini. Ubebe utu na uzalendo wa taifa mbele.
Hivyo ndivyo tutapiga hatua.
12. Vinginevyo tutakuwa tunapig marktim tuu
Tupo!
Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam