Unasemaje kuwa umefunga wakati kila jioni unakula?

Nenda kajifunze maana ya maneno kwanza. Wivu siyo husda.

Na wewe unae kula unatakiwa uheshimu jambo la mwenzako. Hapa kuna vitu mnachanganya na mnakuja kuongelea mambo kihisia.

Mathalani nchi kama Zanzibar ni sahihi kufanya maamuzi yale sababu wao kule zaidi ya asilimia 80 ni Waislamu hata huku Bara pia. Ustaarabu ni wewe kuheshimu imani ya mwenzako hasa ukijua. Kwanini ule mbele ya mwenzako na unajua amefunga ?
Sasa ndio nikauliza, kwanini ughafirike kwa mwenzako amabe hajafunga kula mchana wakati kufunga kwako ni imani yako, yaaani why uone wivu kiasi ufungie migahawa? Kwanini usishike imani yako na kuendelea na funga yako? Anyway

Kwa sisi ambao usiku hatuki wala hatunywi, bali tunalala tu hadi asubuhi ndio tunakunywa chai, tunakuwa tumefunga?
 
Hakika, hakuna anayempangia mwingine cha kufanya. Ni kuelimishana tu.
Yeah uko sahihi.

Lakini kwanini wewe umethubutu kuwapangia wengine cha kufanya?
Pale uliposema kwamba " Nadhani wanapaswa kutumia jina jingine lakini sio kufunga."

Hauoni kama hapo unaingilia maamuzi na maono ya wengine pia kuwapangia nini cha kufanya?
 
Tafuta wewe tafsiri yako, wewe ndio unaejua nini unachokifanya, hata ukiwa kila muda unakula na ukasema umefunga labda utakuwa sahihi, maana unaweza sema unaifunga njaa, kwa vile utakiwi kuwa na njaa waelevu kama sisi tutakuelewa.

Huyo jamaa anashangaa jinsi linavyotumika neno funga hajui hata kwenye mipira, mabao, madrafti na michezo mingine inatumia neno funga tofauti na funga aijuae yeye.
Okay, unadhani kitendo cha wengine kutokula wala kunywa usiku hadi inapofika asubuhi ndio wanakunywa chai, na kitendo cha wengine kutokula asubuhi hadi inapofika usiku ndio wanakula futari, kinatofauti gani kimsingi?
 
Maji ya Nini brother...?? Me nawajua watu wanafunga 40 kavu bila kula kitu we unasema maji... Bado hujui kufunga na wewe tafuta neno jingine...
Huyo atakae maliza siku tatu bila maji nampa millon
 
Hicho ni kitu cha mtu binafsi na maamuzi yake.
Anaweza kusema chochote kile eidha amefunga au lah na kama akikubali basi sawa. lakini cha muhimu ni kwamba mimi sina mamlaka ya kujudge maamuzi wala maono ya mtu binafsi.
Well, tunataka kupata mantiki ya hiki kinachoendelea, yaani what is truely the logic behind?!

Kuna tofauti ipi ya kimsingi, kwa ambae usiku hali wala hanywi, bali analala tu hadi asubuhi halafu anakunywa chai, na huyu mwingine yeye kuanzia asubuhi hali wala kunywa, hadi usiku ndio anakula futari, kuna tofauti gani kiasi kwamba huyu wa kutokula mchana anapiga piga kelele sana juu ya kitendo chake hicho huku huyu ambae hali usiku yeye anafanya kitendo hicho bila kupiga piga kelele sana kwa wenzake juu ya kitendo hicho? Nini maoni yako, ni utaahira au ulimbukeni?
 
Yeah uko sahihi.

Lakini kwanini wewe umethubutu kuwapangia wengine cha kufanya?
Pale uliposema kwamba " Nadhani wanapaswa kutumia jina jingine lakini sio kufunga."

Hauoni kama hapo unaingilia maamuzi na maono ya wengine pia kuwapangia nini cha kufanya?
Hayo ni maoni yangu na ndio maana nimesema nadhani na sijamuamrisha mtu.
 
Well, tunataka kupata mantiki ya hiki kinachoendelea, yaani what is truely the logic behind?!

Kuna tofauti ipi ya kimsingi, kwa ambae usiku hali wala hanywi, bali analala tu hadi asubuhi halafu anakunywa chai, na huyu mwingine yeye kuanzia asubuhi hali wala kunywa, hadi usiku ndio anakula futari, kuna tofauti gani kiasi kwamba huyu wa kutokula mchana anapiga piga kelele sana juu ya kitendo chake hicho huku huyu ambae hali usiku yeye anafanya kitendo hicho bila kupiga piga kelele sana kwa wenzake juu ya kitendo hicho? Nini maoni yako, ni utaahira au ulimbukeni?
It's a matter of different perspectives and perceptions.
Binadamu anaishi kwa hivyo vitu viwili ili kupata maana nzima ya maisha.

Ni maswala ya makubaliano kwamba jambo fulani litakuwa hivi na kuonekana hivi, litaitwa hivi na litachukuliwa hivi, na kama kuna makubaliano basi itakuwa hivyo.
Na mimi nadhani ni kitu kizuri kuheshimu hayo makubaliano yao. bila kuwaingilia maamuzi yao wala kuwapangia.

Unachokiona mmoja sicho anachokiona mwengine.
 
Well yeah hatuwezi kuingilia makubaliano, lakini hoja bado iko pale pale, kwamba, kwanini anaefunga usiku hapigi pigi kelele kama hawa wanaofunga mchana, why?
 
Hayo ni maoni yangu na ndio maana nimesema nadhani na sijamuamrisha mtu.
Kuingilia maamuzi ya mtu sio lazima umuamrishe kwa nguvu bali hata kutoa tu idea yako juu yake ni tayari umeshaingilia maamuzi ya mtu.
Maana ya neno "nadhani" ni kuwa na maoni, imani au wazo juu ya mtu au kitu fulani.
Means kusema "nadhani" ni tayari umeshaingilia maamuzi ya mtu.

Ni sawa na kusema "unachofanya umekosea na hauko sahihi lakini utajua mwenyewe." tofauti ni kwamba hiyo sentensi umeifunga ndani ya neno moja "nadhani."
Mara zote ni vizuri kuheshimu uhuru na maamuzi ya watu wengine ili kuepusha uvunjifu wa amani na heshima pia kuepusha migogoro isiyo na lazima.
Hata kama haukubaliani na maamuzi hayo.

Heshima ni moja ya kielelezo cha mtu mwenye utu na ustaarabu ndani yake.
 
Well yeah hatuwezi kuingilia makubaliano, lakini hoja bado iko pale pale, kwamba, kwanini anaefunga usiku hapigi pigi kelele kama hawa wanaofunga mchana, why?
Clearly ni sababu wameingiliwa makubaliano na maamuzi yao.
 
Humu kuna wajinga wengi sana huwa nawapuuzia sana hasa Wasio Waislamu hutubeza ya kuwa tunabadilisha muda wa kula.

Sasa nakuuliza maana ya kufunga ni kujizuia kula pekee ? Huu ujinga amewaambia nani ?

Kwetu sisi Waislamu kufunga ni kujizuia kula, kufanya uovu, batili kuanzia alfajiri ya kweli mpaka jua linapo zama. Hii ndiyo maana ya funga kwetu sisi Waislamu.

Sasa unapotushangaa sisi na sisi tunakushangaa wewe kuhusu maana yako batili ya kufunga.
Halafu hajishangai anafunga siku 7 wakati.wengine wanafunga 20. Na pia.kunywa mami siyo kula?.kama.uliambiwa ufunge 40 kwann ufunge 7????? Tena kwa kujitahidi
 
Kuingilia maamuzi ya mtu sio lazima umuamrishe kwa nguvu bali hata kutoa tu idea yako juu yake ni tayari umeshaingilia maamuzi ya mtu.
Maana ya neno "nadhani" ni kuwa na maoni, imani au wazo juu ya mtu au kitu fulani.
Means kusema "nadhani" ni tayari umeshaingilia maamuzi ya mtu.

Ni sawa na kusema "unachofanya umekosea na hauko sahihi lakini utajua mwenyewe." tofauti ni kwamba hiyo sentensi umeifunga ndani ya neno moja "nadhani."
Mara zote ni vizuri kuheshimu uhuru na maamuzi ya watu wengine ili kuepusha uvunjifu wa amani na heshima pia kuepusha migogoro isiyo na lazima.
Hata kama haukubaliani na maamuzi hayo.

Heshima ni moja ya kielelezo cha mtu mwenye utu na ustaarabu ndani yake.
Unataka kumaanisha kwamba siwezi kutoa maoni yangu kwasababu yatatofautiana na ya mtu mwingine?

Hapo ndio utakuwa umeharibu dhana nzima ya uhuru wa mawazo.

Ukiona mawazo yangu hayakufai unayaacha na kuendelea na yakwako bila kunizuia mimi kutoa maoni yangu.
 
Ilibidi wewe ndio uwe wa kwanza kufanya hivyo.
Kwamba ukiona ya wengine hayakufai basi unayaacha na kuendelea na ya kwako.

Lakini umeshindwa kufanya hivyo.
that's why nikamalizia na quote ya "Heshima" mwishoni sababu najua hiyo ni circle paradox, means hata wewe statement yako ya mwisho inaingilia freedom of speech.
 
Halafu hajishangai anafunga siku 7 wakati.wengine wanafunga 20. Na pia.kunywa mami siyo kula?.kama.uliambiwa ufunge 40 kwann ufunge 7????? Tena kwa kujitahidi
Kufunga kwa afya unaamua wewe mwenyewe kutegemeana na matokeo unayotaka.

Siku saba ni basic kwa kufanya detoxification ya mwili na ikifika siku 14 unapata kusafishwa kabisa mwili. Seli, tissue na ogani zote zinasafishwa na ikifika siku 21 ni total restoration.

Yaani hapa mwili wako unakuwa kama alivyo mtoto mchanga. Hutahitaji tena sukari wala chumvi wala kula vyakula vingi bali utakula mlo kamili kwa kiwango kidogo na utapata afya. Magonjwa yote yanatoweka.

Sasa ukienda kwenye imani ya kikristo mtu anatakiwa kufunga na kuna aina mbalimbali za kufunga kama vile siku tatu (hizi huwa zinafanywa bila kugusa maji wala chakula na huwa ni kwa ajili ya maombi ya dharula) pia zipo siku 21 (ambazo huwa ni kwa ajili ya urejesho) na halafu zipo hizo 40 (ambazo mara nyingi ni kwa ajili ya maandalizi ya kutimiza kusudi fulani).

Sasa hekima ya kawaida ni kwamba ili uweze kufunga siku 21 na kuendelea unapaswa kuwa na uzoefu wa siku saba ili usije ukadhoofu au kufa kabisa. Na hata siku saba unatakiwa uwe umezoea kufunga zile tatu.

Ukristo hauna sheria ya kukulazimisha ufunge zipi. Ni wewe tu na shauku yako ya kumtafuta Mungu.
 
Ilibidi wewe ndio uwe wa kwanza kufanya hivyo.
Kwamba ukiona ya wengine hayakufai basi unayaacha na kuendelea na ya kwako.

Lakini umeshindwa kufanya hivyo.
that's why nikamalizia na quote ya "Heshima" mwishoni sababu najua hiyo ni circle paradox, means hata wewe statement yako ya mwisho inaingilia freedom of speech.
Mimi nimetoa maoni yangu bila kumzuia mwingine kutoa yakwake. Pia sijamzuia mwingine kuendelea na mawazo yake.
 
Freedom of speech ina boundaries na limitations.
Kama kila mtu angekuwa anatoa maoni yake anavyopenda basi kungekuwa hakuna amani nchini.
In your case umevuka hizo boundaries na limitations.

Vipi kuhusu heshima na ustaarabu sababu hivyo ndio vitu vinavyotafsiri utu wa binadamu?
 
Sioni mpaka wowote niliovuka. Mods wangekuwa wameshaifuta hii mada kama wangeona kuna hali ya kuvunjiana heshima.
 
Back
Top Bottom