Unasomea Udaktari miaka mingi, kisha unakuja kulipwa hivi

Unasomea Udaktari miaka mingi, kisha unakuja kulipwa hivi

Kwa tunapoelekea, hata specialist wataanza kulipwa upuuzi very soon. Washaanza kuwa wengi, Gyne, pediatricians, surgeons wamejazana madarasani kibao, in 5 years tutakuwa na floods of them. Btw, hata specialists serikalini hawana mshahara wa kutisha hivyo. Wengi bila kujiongeza na private clinics, malalamiko yatakuwa makubwa.
Mshahara huwa hautoshi. Kujiongeza muhimu.
 
Sasa nani anapata 3-5m kirahisi? Labda uwe mwizi. Hakuna hela rahisi sio mwajiriwa wala aliejiajiri. Mshahara wa kuanzia huwa ni mdogo popote pale,ila ukiendelea na kuwa specialist unapanda sio Dr tu hata taaluma nyingine.
Mkuu kuna watu wanakunja pesa ndefu kwa masaa yasiozidi 8 wameajiriwa hapo na wikiend haendi kazini...ila Medicine ili upate hayo maisha ndo unakuta mtu asubuhi saa 2 yupo Uhimbili mpaka saa 8 mchana ,akitoka hapo mbio anakimbia Hindu mandal mpaka saa 2 usiku hapo bado kuna sehemu kaomba kazi afundishe..huyu mtu anapata pesa ila haifaidi hana uhuru nayo ni mateso sasa hiyo kazi gani?
 
Enhe na MD wa hifadhi za taifa TANAPA(serikali),analipwa bei gani?,........au unadhani TANAPA hamna madaktari wa binadamu na wanyama?😆😃
Tayari umeshazungumzia Daktari ambaye ana taaluma lakini huyu anayelipwa almost milioni 3 hana elimu yoyote wala fani yoyote lakini anakunja aidha sawa ama kumzidi mwenye taaluma.
 
Mshahara wa mtu ni Confidential, wewe umeonaje? report central police mara moja
Kwa sababu watu wananyonywa.. enzi za ujamaa kila kazi mshahara wake unajulikana... hizo za confidential umezitolea wapi katika nchi hii? wabunge tu tunajua wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya n.k au kujifanya mjuaji tu.. kuna watu hawastahili aina ya mishahara pengine sababu wapo makazini kwa kutoa umbea tu kwa mabosi wanapata mishahara mikubwa kuliko slary scale wanazostahili
 
1.Fani zipi watu walisoma na sasa ni matajiri?
2.kua walimu wa chuo kikuu nao ni miongoni mwa watu masikini hapa Tanzania?
1. Fani ya TRA. Hujasikia hata rais anaongelea TRA ni balaa na nusu TRA, Bank, BOT, TPA, REA, TANESCO, EWURA, TPDC, NIC, Insurance nk.

2. Maisha ya walimu Tanzania yanafanana haijalishi anafundisha chuo kikuu ama anafundisha vidudu(chekechea). Tofauti yao ni ndogo sana. Maisha yao yanafanana kuanzia tabia hadi maisha ya kawaida.
 
Back
Top Bottom