Unataka kuamini kauli za chadema kwamba CCM hawajaleta maendeleo yoyote tangu uhuru? Ushahidi huu hapa, jionee mwenyewe.

Unataka kuamini kauli za chadema kwamba CCM hawajaleta maendeleo yoyote tangu uhuru? Ushahidi huu hapa, jionee mwenyewe.

Acha mambo ya kijima,hizi enzi zilikuwa za kuzungumza habari za Bullet train,akina AI,na habari za kwenda kutua mwezini kwa rasilimali na technologia za ndani.Unaongea habari ya mtwara ilikuwa siku ngapi kufikaa?
Hamia huko kwenye AI. Pumbav
 
CCM wamekuwa wakijigamba kwamba nchi wameitoa mbali, wameleta maendeleo. Upande wa upinzani wanasema nchi imekuwa ya hovyo kabisa ni afadhali mkoloni. Sasa mimi naweka ushahidi wote hapa kuunga mkono hoja za Chadema.

View attachment 3374152View attachment 3374155
Huoni kwamba barabara za 1970 zilikuwa nzuri zaidi zikiwa na alama za barabarani, miti na kijani kibichi na parking kubwa za magari wakati barabara za 2025 hazina alama, miti, ukoka wala parking nzuri?
 
Angalia vizuri
 
CCM wamekuwa wakijigamba kwamba nchi wameitoa mbali, wameleta maendeleo. Upande wa upinzani wanasema nchi imekuwa ya hovyo kabisa ni afadhali mkoloni. Sasa mimi naweka ushahidi wote hapa kuunga mkono hoja za Chadema.

View attachment 3374152View attachment 3374155
Tafsiri ya maendeleo huijui mapicha picha sio maendeleo. Elimu, maji kwa uhakika na kwa wote , madaraja na Barbara, bima ya afya kila Mtanzania, ajira, utafiti na ugunduzi, uzalishaji wa viwanda, kujitosheleza kwa chakula.
 
Unachotakiwa kutambua ni kwamba; Maendeleo ni neno mtambuka.

Maendeleo yamepatikana bila shaka. Ila hayaendani na uhalisia, muda, na pia kipato cha mwananchi mmoja mmoja.
Tate Mkuu,
Ukisema maendeleo ni neno mtambuka utakuwa unampa mleta mada sehemu ya kujificha akijibiwia hoja yake dhaifu...
Mwambie ukweli mleta mada,..tunaposema CCM haijaleta maendeleo toka tupate uhuru tunajiuliza maswali kadha yanayokosa majibu.......

1; Kwa nini miaka 63 baada ya kupata uhuru wake China ikamzidi mkoloni wake wa zamani Japan kwa pato la mwaka(GDP) huku Tanzania bado ikiendelea kuchangiwa na mkoloni wake wa zamani pamoja na wahisani wengine katika bajeti yake hata bada ya miaka zaidi 60 baada ya uhuru?

2: Kwa nini baada ya zaidi ya miaka 60 toka uhuru, Tanzania bado imeshindwa kuzalisha na kuajiri walimu wakati kuna uhaba mkubwa wa walimu mshuleni....,ikizingatiwa kwamba elimu bora na inayofikika kwa wote ndiyo mama wa maendeleo kamili kwa jamii?

3: Kwa nini hadi leo baada ya zaidi mika 60 ya uhuru ,Tanzania imeshindwa kuzalisha na kuajiri madaktari na watendaji wengine katika sekta ya afya ili kupunguza uwiano mkubwa wa wagonjwa na watoa huduma kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora na ya uuhakia ya afya ?

4: Hivi kama kweli tunaongozwa na watu wenye mtazamo wa mbali, inawezekana vipi miaka 60 baada ya uhuru nchi iliyozungukwa na maji ya maziwa na mito mikubwa lakini wananchi wake wawe na uhaba mkubwa maji ,na wawe na milipuko ya mgonjwa yanayotokana na uchafu/ ukosefu wa maji kila mwaka?

5: kwa nini Singapore ambayo tulikuwa nayo sawa kiuchumi mwaka 1965 ,leo wakiwa na pato kubwa la kiuchumi kwa nchi na mtu mmoja mmoja,huku wakiwa na huduma bora kabisa za elimu na afya....na ikizingatiwa kwamba kwa yeyote asiyejua matumizi ya computer Singapore anahesabiwa kama asiyejua kusoma na kuandika...kwa vile mafunzo na matumizi yake yaanzia madarasa ya mwanzo shule ya msingi......,sasa utafananisha na hayo anayoyaita maendeleo ya Tnzania ambako zaidi ya ¾ ya watu wake hawana hata elimu ya sekondari?
 
Tafsiri ya maendeleo huijui mapicha picha sio maendeleo. Elimu, maji kwa uhakika na kwa wote , madaraja na Barbara, bima ya afya kila Mtanzania, ajira, utafiti na ugunduzi, uzalishaji wa viwanda, kujitosheleza kwa chakula.
Nimekupa sehemu tu, haya mambo yapo nchi nzima
 
Tunawatu wanamibichwa mizito hii nchi!! Ndomana wenye akili wako jela wasiojaaliwa hiyo wanazurura wakisema nchi inaendelea kuliko nchi zinazotusaidia bajeti na vingine vingi😢
Sasa we kichwa box yanayoongelewa ni maendeleo ya kweli yanayoendana na rasilimali zetu tele na muda mrefu toka uhuru!!
Nchi wanazobadili mifumo na uongozi wanazaidi yauto tugorofa ulitoonesha hapo uwe unasafiri nchi za watu utoe uzwazwa ulokujaa kichwani... nenda hata hapo Kenya tuu.
Wajinga mnaihujumu saana hii nchi simhamie somalia
 
Wapi nimetukana? Wewe ni miongoni mwa mnaotumia vichwa kubebea kamasi
Wenye vichwa vilivyobeba ubongo mnaishia kuongea ujinga mkiwa mmejificha katika majina bandia.

Hamza alipigwa risasi muda ule ule baada ya kumuua askari mmoja pale salendar.

Mnataka vijana wenye ujasiri unaopotezwa muda huo huo na maaskari wetu?. Alijitoa muhanga, vijana wangapi Tanzania hii wenye uwezo wa kujitoa muhanga?.
 
CCM ilikua enzi za mwalimu. Ukisikia mwalimu ametembelea mkoani kwako ukienda kumsikiliza lazima uende na notebook ili ukapate nondo halafu uwahi mapema maama wanaokuja kumsikiliza ni wengi mno. Siku hizi kiongozi wa CCM akija mahali lazima awe na wasanii, t shirt au pilau ndio apate watu.
 
Back
Top Bottom