Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Matokeo ya mazoezi unayaona mwezi?

Inategemea pia na mtu na mtu ila kuanzia mwezi unaanza kuona Matokeo hasa kwa ndani mfano pumzi wepesi nk Matokeo ya nje yanahitaji muda na uvumilivu
 
Hata mimi nimeridhika na kitambi changu,hata kama nimeishiwa naonekana niko na pesa.
Hata kama natembea kwa miguu naonekana niko na gari ila nimeamua tu kufanya mazoezi.

Endelea kujifariji mkuu na ujinga wako
 
Wewe ndio mjinga unayepoteza muda wako kutafuta malimao sijui ndizi uondoe tumbo badala ya kupoteza muda kutafuta pesa

Daaah afya ikizingua utaona hizo pesa utazipata wapi na utaona utakavyogramika matibabu acha kujipakaza ujinga wa kijinga
 
Yaap!!!, Kitambi kina heshima yake bhana.
kwa mfano mkienda sehemu ya huduma watu wawili mwenye kitambi na mwingine flat lazima ataanza kuhudumiwa mwenye kitambi na aliye flat atafuata baadae.
Utakuta wahudumu wanakuita kwa unyenyekevu"Karibu Boss,tunaomba tukuhudumie" sasa hii favour ndio inayonifanya niache kujichosha au kujishindisha na njaa kwa ajili ya kukiondoa kitambi.
 
Umeona eenhh???, Kitambi ndo hbr ya mjini.
 
Na sisi wanawake wenye vitambi tutapewa kipaumbele???
 
Kwa mujibu wa wataalamu kupunguza unene kunachangiwa na:-
1. Aina ya lishe(diet)-50%
2. Mazoezi - 30%
3. Kupumzika - 20%

Kupunguza kiwango cha wanga na mafuta mengi kwenye diet. Jikite kula mboga mboga, matunda, nuts, Jamii ya mikunde na kunywa maji ya kutosha. So vyema kabisa kuacha kula wanga usije kuokosesha kabisa mwili nguvu na kuanza kupata kizunguzungu.
 
Mmmh mpangilio wa kuandaa hivi vitu ni ngumu, mchana kazini inakuwaje? Kweli kutengeneza mwili ni gharama na muda juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…