Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

Unataka Tumbo Flat na Six Packs? Cheki Hapa

mkuu, hicho ya kitaili mmmh unaweza ng'oa meno!!

vipi nikipiga mengine bila ya hicho kitaili?
 
Ukianza mazoezi iwe ndio kama kilevi chako,sio eti baada ya kupungua uache UTAKUWA BONGE AFADHARI YA MWANZO,NA WATU WENGI HAWALIONGEI HILI. WAANGALIE WANAMICHEZO WOTE WALIOACHA AU KUPUNGUZA MAZOEZI WANAVYOKUWA.
ok, nna wiki tatu,, najiina kamwili kanakatika ile kisawasawa,,, siwez acha,
 
Kuruka kamba na Roller vimenisaidia sana kupunguza mwili ila huwa napata uvivu sana nikifanya hayo mazoezi nikiwa hme hadi najikuta naacha Roller na Kamba home naenda Gym kwa ajili ya hivyo hivyo vifaa ila kwa sababu Gym napata kampani nafanya najikuta nafanya mazoezi mda mrefu...
shida ya gym mahela, sie wa kuunga unga mwana tunazipga hizo home tu
 
Mazoezi ukiyazoea inakuwa ni kama starehe. Nilianza kuota kitambi mara tu nilipopata kiajira na kuanza kuzikunja noti na kubahatika kupata kausafiri kakutembelea, nikaona sasa huko ninapoelekea nitapasuka. Nikiangalia muda wa kufanya mazoezi nakosa kabisa, naingia kazini asubuhi narudi jioni. Nikaona chakufanya hapa ni kuamka alfajiri nifanye mazoezi ndio niende kazini. Nikaanza kuamka saa 11:00 alfajiri kila siku, naenda uwanjani kukimbia kuzunguka uwanja. Siku ya kwanza nilizunguka mara 6, siku zilivyozidi kwenda nikawa naongeza, hatimaye nikawa naweza kuzunguka mara 35, na nikitoka kukimbia nikifika home nafanya mazoezi ya tumbo kama crunches, sit ups, n,k.

Siku hizi nimebadili utaratibu, sihesabu tena mizunguko ninayozunguka uwanja bali nakimbia kwa saa 1 bila kupumzika. Kitambi kimeyeyuka na nina six-pack, najisikia vizuri muda wote, nimechangamka na ninajiamini. Nimezoea kufanya mazoezi hadi nikikosa kufanya nahisi kupungukiwa kitu kwa siku hiyo.

Ukichukulia mazoezi ni adhabu, utafanya kwa siku chache na kuacha. Mazoezi ni matamu asikwambie mtu. Tufanye mazoezi wakuu.

Nimeona nishee hii ili wengine nao wahamasike
kabisa mkuu, huwa natabasam pale napojichek kwa kioo,, kuona niko na mwili uliovunjika vunjika,, [emoji23]
 
Hongera sana hapo sasa vyombo vinaingia
hakika mkuu, kwa haraka haraka nimeanza ona mabadiriko ktk mwili wangu,, kifua kishaanza kukatika, paja naliona linaanza kukatika,, kwenye mbavu naiona V nikinyoosha mikono juu, trycep inatoka fast sana, hadi nikitembea nahisi kamwendo kamebadilika [emoji23]

ila tumbo ndo mziki baba,, kwa mbaaaali nazioona two pack nikikaa mbele ya kioo [emoji23] [emoji23]

ila mkuu vipi niongeze round maana hizi round tano kama nishazimudu?!
 
Ongeza.

Na ukizimudu unaongeza tena.

Ukizimudu unaongeza tena.

Yaani mwendo ni huo.

Ni njia nzuri kutrain kwa kujichallenge.

Hapo kwenye kamwendo jiangalie usijeanza kutamani ugomvi.
 
Zoezi lepesi ambalo linaondoa mafuta tumboni/ mwilini na na kulifanya kuwa flat ni skipping rope au jumping rope yaani kuruka kamba!

Aina hii ya zoezi kushughulika na mwili wote na mojawapo wa cardiovascular health exercise! Yaani humfanya afanyae zoezi hili kuvuta hewa na kupumua kwa kiwango kikubwa- hali hii hufanya kuyeyesha mafuta na kuruhusu mzunguko mkubwa wa damu !
Likifanywa kwa muda wa dk 30 kila siku ndani ya mwezi mmoja, lazima utakuwa flat, bila kitambi na packs zitaonekana !
Jumping rope is among the best exercise for our body! Harafu ni cheap, na yaweza kufanyika popote!
 
Kwa muda gani kuruka kamba kutafanya hivyo?
 
Back
Top Bottom