Elections 2015 Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na kuwa mgombea Urais?

Elections 2015 Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na kuwa mgombea Urais?

Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na Kugombea Urais?

  • NDIYO

    Votes: 318 59.8%
  • HAPANA

    Votes: 214 40.2%

  • Total voters
    532
  • Poll closed .
Je,utaunga mkono uamuzi wowote wa kumfanya Lowassa awe mgombea uraisi kwa ticket ya CHADEMA/UKAWA endapo uamuzi huo utafikiwa?

Jibu Ndio/Hapana/Sijui

Kura hii inawahusu Pro-UKAWA wote na wengine wenye kuunga mkono umoja huu tu.

ndiooooooo mia kwa mia
 
Na mkome wanaosema lowassa ni mwizi aliwaibia nn? Kakubali kubeba lawama zisizo zake still hilo hamuoni? Towen unafiki fungua macho alilazimika kuwajibika kisiasa kuilinda serikari leo kashfa eti mwizi? Acheni chuki binafsi.

Heri aliyenacho kama ni kuiba ataiba kidogo kuliko kafifi.
 
Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa hapo chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.


Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.


Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
 
Upigaji kura hii nashauri ufungwe 10/8/2015 badala ya 07//09/2015 kwa sababu mbili kuu zifuatazo;

1. Ndiyo muda ambao kwa vyovyote vile vyama vyote vitakuwa vimemaliza michakato vya kupata wagombea wa uongozi wa kuchaguliwa kwa ngazi zote kwa maana ya udiwani, ubunge na urais. Na kwa mantiki hii ni kwamba tayari itakuwa imejulikana kama Edward Lowassa amehamia CHADEMA na kupata nafasi hiyo ya ugombea Urais au La!

2. Nature ya swali lenyewe kwamba "Unaunga mkono Edward Lowassa kuhamia CHADEMA na kugombea Urais".

7th September, 2015 tayari watu watakuwa katikati ya kampeni, hivyo kwa namna yoyote, swali hili litakuwa tayari out of date!

Vinginevyo mimi naunga mkono EL aje na si tu kuja bali aendelee na "Safari ya uhakika" na si ile "ya matumaini" tena.

Muhimu ni kuwa wajiridhishe pasipo shaka kuwa huyu bwana ana nia ya dhati kuleta mabadiliko ktk siasa za Tanzania na si kuwa kawa katumwa kuja kufanya kazi ya CCM ndani ya CHADEMA/UKAWA kuwasambaratisha km ilivyo hofu ya wengi!!
 
utayaona mafuriko baada ya lowasa kuanza kutambulishwa rasmi kama mgombea urais...binafs kulikuwa na mgongano sana ukawa kuhusu nani asimame kugombea kati ya lipumba na slaa......kama mwanachadema niliona upepo ulivyobadilika watu wengi wakisema watampigia kura magufuli lakini ubunge watawapa wapinzani lkn ule ulikuwa ni unafiki ....kwa sasa kibao kimegeuka kila kona ni lowasa.......kimsingi slaa asingeweza kumshinda magufuli
 
utayaona mafuriko baada ya lowasa kuanza kutambulishwa rasmi kama mgombea urais...binafs kulikuwa na mgongano sana ukawa kuhusu nani asimame kugombea kati ya lipumba na slaa......kama mwanachadema niliona upepo ulivyobadilika watu wengi wakisema watampigia kura magufuli lakini ubunge watawapa wapinzani lkn ule ulikuwa ni unafiki ....kwa sasa kibao kimegeuka kila kona ni lowasa.......kimsingi slaa asingeweza kumshinda magufuli

Umenena vizuri mkuu!
 
Shida mnaishi maisha ya mazoea Na.kucremishaa, We believe in change together we can
 
Back
Top Bottom