Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Utajiri unatokana na mipango na juhudi, hata uende kwa mwamposa kama hauna mipango na juhudi utaendelea kuwa maskini. Ndio maana humu Kuna watu wanasema walokole wengi ni maskini kwa sababu mtu anashinda kanisani anaacha kufanya kazi kwa bidii kutafuta maendeleo
 
Watu wanajidai hawafahamu haya mambo ndio maana wanakuja na nyuzi zao kujidai wanatafuta uhakika.
Wamuulize UMUGHAKA

Ukifuatilia story za kila familia duniani unaweza kusema ni za kutatanisha sana ila kiwango cha utajiri na umaarufu ndio unazifanya familia nyingine kuongelewa zaidi kuliko familia nyingine.
Unadhani kwanini?
 
Duh! Aisee 🤔
 
Ila najiuliza swali Moja kwanini watu wengi ambao inasemekana wana utajiri wa kichawi, hawana utajiri mkubwa wa kumfikia bakhresa, mo dewji au hata Reginald Mengi 🤔 wengi utakuta Wana vighorofa viwili mjini, ndo utajiri wa kichawi huo ephen_
Hapo ndio utajua kwamba hakuna utajiri wa kishetani.

Maana watu wanaodai kuna utajiri wa kishetani ukiangalia huo utajiri wao bado ni wa kiwango cha chini sana.

Hawamfikii hata Mo Dewji, Bakhressa au Dangote.

Kama mtu anadai kuna utajiri wa kishetani, Kwa nini asiutumie kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett na wengineo?

Utakuta mtu anadai kuna utajiri wa kishetani lakini maisha yake ni ya kimaskini halafu anakomaa tu kuna utajiri wa kishetani!!!

Kuutumia atajirike, hataki.

Unajua hawa waafrika hasa watanzania maskini wana mentality za kijinga sana.
 
Upo sahihi Kbsa mkuu
 
We jamaa bado unakazia msimamo wako tu kwamba Mungu Wala utajiri wa kishirikina havipo eeh😅
 
Duh yani mtu unatafuta ajira ujikwamue kimaisha kazi unapata na nyota yako inachukuliwa. Hatari sana
 
😮😮😮
 
Ofisi za Freemasons kwa DSM ziko wapi ? Ukiachana na jengo la mason hall posta mwenye kujua anijuze ndugu zanguni
 
Ila najiuliza swali Moja kwanini watu wengi ambao inasemekana wana utajiri wa kichawi, hawana utajiri mkubwa wa kumfikia bakhresa, mo dewji au hata Reginald Mengi 🤔 wengi utakuta Wana vighorofa viwili mjini, ndo utajiri wa kichawi huo ephen_
mbona jibu jepesi sana hilo.
Ila ninaweza kukuuliza swali pia
Unahisi Iq zao, na creativity zinafanana? na muda walio initiate?
 
Kuna watu wanabishia hiki kitu ila haya mambo yapo sana
 
We jamaa bado unakazia msimamo wako tu kwamba Mungu Wala utajiri wa kishirikina havipo eeh😅
Kama vipo nenda kavitumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk na Jeff Bezos.

Wewe si unadai na kuamini kuna utajiri wa namna hiyo, Mbona umeshindwa kuutumia au mbona huutumii ili utajirike?
 
Kuna watu wanabishia hiki kitu ila haya mambo yapo sana
Kama unajua yapo, mbona huyatumii?

Kama unajua mambo hayo yapo, Mbona umeshindwa kuyatumia kwa juhudi zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk au angalau basi ufikie utajiri wa kina Bakhressa?

Mbona waafrika hawautumii huo uchawi wao kuwazidi wazungu?

Tumieni huo uchawi kujenga viwanda vikubwa, barabara za juu (fly overs), Airports, Ports, shule na hospitali na mlete maendeleo kwenye jamii zenu kwa kutumia huo uchawi.

Kama kweli huo uchawi wenu una nguvu na unafanya kazi kweli.
 
Usishangae ukatafutwa PM na huyu huyu aliyekataa uwepo wa utajiri wa namna hii akataka umpe connection ya Malawi😀
 
Ndugu yangu wa kifikia; mtoto wake wa kwanza ana utindio wa ubongo, na mtoto wake wa pili na wa mwisho alizaliwa mlemavu wa miguu ILA sikuwahi kusikia anahusishwa na imani za kafara ajabu alilaumiwa mke wake kwamba ana mikosi.

Naamini angekuwa na uchumi wa kutisha ama nafasi ya cheo basi hizi tuhuma zingemhusu moja kwa moja.

Japo sikatai haya mambo yapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…