Passion Lady
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 8,694
- 4,643
Roho mbaya hulka tu...weusi tunaroho mbaya na umaskini juu..Watu weusi hawana roho ngumu kuliko hao waarabu na wahindi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Roho mbaya hulka tu...weusi tunaroho mbaya na umaskini juu..Watu weusi hawana roho ngumu kuliko hao waarabu na wahindi
Watu wanajidai hawafahamu haya mambo ndio maana wanakuja na nyuzi zao kujidai wanatafuta uhakika.
Wamuulize UMUGHAKA
Unadhani kwanini?Ukifuatilia story za kila familia duniani unaweza kusema ni za kutatanisha sana ila kiwango cha utajiri na umaarufu ndio unazifanya familia nyingine kuongelewa zaidi kuliko familia nyingine.
Duh! Aisee 🤔Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo
Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.
Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
Hapo ndio utajua kwamba hakuna utajiri wa kishetani.Ila najiuliza swali Moja kwanini watu wengi ambao inasemekana wana utajiri wa kichawi, hawana utajiri mkubwa wa kumfikia bakhresa, mo dewji au hata Reginald Mengi 🤔 wengi utakuta Wana vighorofa viwili mjini, ndo utajiri wa kichawi huo ephen_
Upo sahihi Kbsa mkuuUtajiri unatokana na mipango na juhudi, hata uende kwa mwamposa kama hauna mipango na juhudi utaendelea kuwa maskini. Ndio maana humu Kuna watu wanasema walokole wengi ni maskini kwa sababu mtu anashinda kanisani anaacha kufanya kazi kwa bidii kutafuta maendeleo
Usijepoteze muda kwa huyo baba hapo.Siwezi kupoteza muda kukujibu hayo maswali yako sababu mimi na wewe tayari tunaamini vitu viwili tofauti.
Ningekujibu kama ungekua unataka kueleweshwa na sio kushindana
We jamaa bado unakazia msimamo wako tu kwamba Mungu Wala utajiri wa kishirikina havipo eeh😅Hapo ndio utajua kwamba hakuna utajiri wa kishetani.
Maana watu wanaodai kuna utajiri wa kishetani ukiangalia huo utajiri wao bado ni wa kiwango cha chini sana.
Hawamfikii hata Mo Dewji, Bakhressa au Dangote.
Kama mtu anadai kuna utajiri wa kishetani, Kwa nini asiutumie kwa nguvu zake zote awazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos, Billgates, Warren Buffett na wengineo?
Utakuta mtu anadai kuna utajiri wa kishetani lakini maisha yake ni ya kimaskini halafu anakomaa tu kuna utajiri wa kishetani!!!
Kuutumia atajirike, hataki.
Unajua hawa waafrika hasa watanzania maskini wana mentality za kijinga sana.
Duh yani mtu unatafuta ajira ujikwamue kimaisha kazi unapata na nyota yako inachukuliwa. Hatari sanaMimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo
Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.
Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
😮😮😮Nakumbuka nipo mdogo Moshi huko kuna nyumba moja ina mtoto/kijana ambae akili zake sio nzuri, yule kijana ilikuwa kila ikifika jioni ya saa 12 analia kama ng'ombe na kweli kwao wanafanya biashara ya kuuza nyama mjini /Dar na unaambiwa walikuwa wanauza balaa.
Jioni ndio mida ya kufunga biashara/hesabu!!
mbona jibu jepesi sana hilo.Ila najiuliza swali Moja kwanini watu wengi ambao inasemekana wana utajiri wa kichawi, hawana utajiri mkubwa wa kumfikia bakhresa, mo dewji au hata Reginald Mengi 🤔 wengi utakuta Wana vighorofa viwili mjini, ndo utajiri wa kichawi huo ephen_
Kuna watu wanabishia hiki kitu ila haya mambo yapo sanaNamfahamu jamaa mmoja alikuwa tajiri sana enzi sisi tunakuwa jamaa alikuwa anatumia baiskeli tu kama usafiri wake binafsi ila alikuwa na magari mengi tu.
Ajabu alikuwa na hilux ya mizigo ila bidhaa za duka lake alikuwa anafuata yeye mwenyewe kwa baiskeli yake ila kwa wengine anakodishia hizo gari za kubeba mizigo.
Sisi tulizoea kumuita TAJIRI MCHAFU wananzengo walikuwa wanasema kamtoa sadaka mdogo wake na huyo mdogo mtu alikuwa chizi fresh anakaa hapo dukani kwa kaka yake tu na hakuna wakumtoa hapo.
Haya mambo yanawezekana ila nafikiri ni mateso sana.
Kama vipo nenda kavitumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa duniani kama Elon musk na Jeff Bezos.We jamaa bado unakazia msimamo wako tu kwamba Mungu Wala utajiri wa kishirikina havipo eeh😅
Kama unajua yapo, mbona huyatumii?Kuna watu wanabishia hiki kitu ila haya mambo yapo sana
Usishangae ukatafutwa PM na huyu huyu aliyekataa uwepo wa utajiri wa namna hii akataka umpe connection ya Malawi😀Waniulize Mimi,nimewahi kuishi kwenye utajiri wa nguvu za kishirikina na Nina Wajua watu wangu wa karibu ambao wanaishi na utajiri huo!
Lakini pia,binafsi hadi hivi Sasa Nina Wajua watu wawili (wataalamu) ambao wanatoa utajiri wa nguvu za Giza,mmoja yupo Zanzibar na Mwingine yupo Malawi!
Mkuu maisha yangu ni simulizi tosha,sema kwasababu ya wapumbavu wa hapa JF huwa naamua tu kukaa kimya maana ukibishana na mjinga yawezekana ukawa mjinga zaidi yake!
Nimewahi hadi kulala na maiti hapo Malawi ili nifanikiwe na nilifanikiwa sema ndo hivyo maisha yangu yote ya mafanikio wanawake ndo huwa kikwazo kwangu !
Mtu anakuja hapa anabisha hata hajawahi Kutembea popote zaidi ya kutoka Mbeya kuja Dar au kutoka Dar kwenda Arusha !
Sihitaji kuuliza Kwa mtu Mimi mwenyewe ndiye ushuhuda !
Kama watabisha ngoja waendelee kubisha but for now Sina muda wa kubishana na Abharisya!
Ndugu yangu wa kifikia; mtoto wake wa kwanza ana utindio wa ubongo, na mtoto wake wa pili na wa mwisho alizaliwa mlemavu wa miguu ILA sikuwahi kusikia anahusishwa na imani za kafara ajabu alilaumiwa mke wake kwamba ana mikosi.Mojawapo ya story huwa nazisikia sana na mtu kuwatoa watoto wake au ndugu zake kafara ili afanikiwe katika biashara au siasa. Utoaji kafara huwa unaelezewa kwa mtu huyo aliyoetolewa kafara kufariki kwa kinachodhaniwa kifo cha utata au kupatawa matatizo ya akili(kichaa).
Unaweza kuonyeshwa kichaa fulani ukaambiwa huu ni mtambo wa kutengeneza pesa wa tajiri fulani au ndio chanzo cha mafanikio cha mwanasiasa fulani.
Unajuaje au unathibitishaje kwamba fulani amefanikiwa kwa sababu ya kafara ya mtoto, mzazi, mke au ndugu yake?
Ndugu yangu haya mabo yapo omba Mungu akuhepushilie mbali unaweza kutolewa kafara wewe..
Acha uoga mkuu.Siku ingine unamuomba urafiki wa kalamu na namba ya simu kabisa in case of emergencies.Utakosa vitu vizuri!