Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Kutafuta Uthibitisho Katika Inshu Za Mambo Ya Kiroho Inahitaji Juhudi.Kwa Mfano Mtu Anaweza Akawa Mchawi na Ni Kweli Mchawi Kweli Kweli Lakini Hauwezi Kuthibitisha Kirahisi.Mambo Ya Kiroho Ni Mambo Ya Sirini.
Kuna Siku Kwa Macho Yangu Naked Kabisa Nlishuhudia Mchawi Namuangalia Ananiangalia.Mwaka 2013 Hiyo Magomeni
Hukumwambia salamaleko?
 
Bado sijawahi kuwa na vielelezo visivyotia shaka kuhusu kutokea kwa hayo mambo.Huwa nasikia masimulizi tu au ushuhuda ambao nao sina hakika nao.
Kuna mwanangu mmoja huko moshi anayo pesa sio kidogo , sasa mwamba anakidonda mguuni hakiponi kwa sababu jamaa ana sukari ya kupanda , sasa huko kitaa wanadai ana donda ndugu , ndio linamletea pesa na yeye amevunga tu ili wamwogope hata kuibiwa haibiwi kisa hiyo hofu😁😁😁
 
Huko ndiyo kuishi kwa akili sasa.Yaani inaitwa "mbele mbele yao"!
 
Kutafuta Uthibitisho Katika Inshu Za Mambo Ya Kiroho Inahitaji Juhudi.Kwa Mfano Mtu Anaweza Akawa Mchawi na Ni Kweli Mchawi Kweli Kweli Lakini Hauwezi Kuthibitisha Kirahisi.Mambo Ya Kiroho Ni Mambo Ya Sirini.
Kuna Siku Kwa Macho Yangu Naked Kabisa Nlishuhudia Mchawi Namuangalia Ananiangalia.Mwaka 2013 Hiyo Magomeni
Ulishuhudia huyo mchawi kwa macho yapi mkuu yale ya kwenu ya kiroho au haya haya ya kawaida na ulijuaje ni mchawi?
 
Mimi namjua mmoja alikua rafiki wa mama yangu utajiri wake ni wa kutumia nyota za wafanyakazi wake
Ila ilipofika mwaka 2018 ikabidi amtoe mtoto wake na akafanya hivyo

Ashawahi kumshawishi mama yangu ajiunge huko mama akakimbia nduki na urafiki ukaisha.

Alikuja dar kama housegirl kutoka Upareni ila sasa hivi ni tajiri.
Watu wanajidai hawafahamu haya mambo ndio maana wanakuja na nyuzi zao kujidai wanatafuta uhakika.
Wamuulize UMUGHAKA
 
Kutafuta Uthibitisho Katika Inshu Za Mambo Ya Kiroho Inahitaji Juhudi.Kwa Mfano Mtu Anaweza Akawa Mchawi na Ni Kweli Mchawi Kweli Kweli Lakini Hauwezi Kuthibitisha Kirahisi.Mambo Ya Kiroho Ni Mambo Ya Sirini.
Kuna Siku Kwa Macho Yangu Naked Kabisa Nlishuhudia Mchawi Namuangalia Ananiangalia.Mwaka 2013 Hiyo Magomeni

Hukumwambia salamaleko?
Ebhan eh kwanza Ni Wanatisha Nilihisi Hii Movie Au Ni Nini..Yaan namshangaa Nayeye kanikodolea Ila Kun Vitu Kapaka Usoni.Aisee Nilikimbia Kurud Ndani Haraka Na Mkojo Wote Uliisha
 
Mojawapo ya story huwa nazisikia sana na mtu kuwatoa watoto wake au ndugu zake kafara ili afanikiwe katika biashara au siasa. Utoaji kafara huwa unaelezewa kwa mtu huyo aliyoetolewa kafara kufariki kwa kinachodhaniwa kifo cha utata au kupatawa matatizo ya akili(kichaa).

Unaweza kuonyeshwa kichaa fulani ukaambiwa huu ni mtambo wa kutengeneza pesa wa tajiri fulani au ndio chanzo cha mafanikio cha mwanasiasa fulani.

Unajuaje au unathibitishaje kwamba fulani amefanikiwa kwa sababu ya kafara ya mtoto, mzazi, mke au ndugu yake?
Nakumbuka nipo mdogo Moshi huko kuna nyumba moja ina mtoto/kijana ambae akili zake sio nzuri, yule kijana ilikuwa kila ikifika jioni ya saa 12 analia kama ng'ombe na kweli kwao wanafanya biashara ya kuuza nyama mjini /Dar na unaambiwa walikuwa wanauza balaa.
Jioni ndio mida ya kufunga biashara/hesabu!!
 
Acha uoga mkuu.Siku ingine unamuomba urafiki wa kalamu na namba ya simu kabisa in case of emergencies.Utakosa vitu vizuri!
 
Mojawapo ya story huwa nazisikia sana na mtu kuwatoa watoto wake au ndugu zake kafara ili afanikiwe katika biashara au siasa. Utoaji kafara huwa unaelezewa kwa mtu huyo aliyoetolewa kafara kufariki kwa kinachodhaniwa kifo cha utata au kupatawa matatizo ya akili(kichaa).

Unaweza kuonyeshwa kichaa fulani ukaambiwa huu ni mtambo wa kutengeneza pesa wa tajiri fulani au ndio chanzo cha mafanikio cha mwanasiasa fulani.

Unajuaje au unathibitishaje kwamba fulani amefanikiwa kwa sababu ya kafara ya mtoto, mzazi, mke au ndugu yake?
Imani kama hizi zinatakiwa kupigwa marufuku kwa nguvu zote kwa sababu zinasababisha vifo kwa watu wasio na hatia. I mean mtu akisikia hii imani, anakwenda kuua ndugu yake akitegemea kuwa atapata mafanikio.
 
Nakumbuka nipo mdogo Moshi huko kuna nyumba moja ina mtoto/kijana ambae akili zake sio nzuri, yule kijana ilikuwa kila ikifika jioni ya saa 12 analia kama ng'ombe na kweli kwao wanafanya biashara ya kuuza nyama mjini /Dar na unaambiwa walikuwa wanauza balaa.
Jioni ndio mida ya kufunga biashara/hesabu!!
Mkuu kwani hamjui pia mtu mwenye tatizo la akili anaweza toa sauti za wanyama? Hasa schizophrenia au autism?
 
Tuliishi Nyumba Maeneo Ya Kimara...Ile Nyumba Ni Kubwa na wapangaji Wengi.Sasa Mmiliki Wa Ile Nyumba Alikuwa Na Ndugu Yake Wa Damu Kabisa ni Ka Chizi Amewehuka.Yule bwana ndie aliekuwa ametolewa Chambo Kulinda Ule Utajiri.
Kwa nini watu wanasema huyo ndugu chizi ametolewa chambo ili kulinda utajiri?
 
Nakumbuka nipo mdogo Moshi huko kuna nyumba moja ina mtoto/kijana ambae akili zake sio nzuri, yule kijana ilikuwa kila ikifika jioni ya saa 12 analia kama ng'ombe na kweli kwao wanafanya biashara ya kuuza nyama mjini /Dar na unaambiwa walikuwa wanauza balaa.
Jioni ndio mida ya kufunga biashara/hesabu!!
Haiwezekani labda hilo tatizo la akili la huyo kijana linakuwa baya zaidi wakati giza linakaribia kuingia na kumpelekea kufanya hivyo?
 
Ulishuhudia huyo mchawi kwa macho yapi mkuu yale ya kwenu ya kiroho au haya haya ya kawaida na ulijuaje ni mchawi?
Yaani Umeamka Zako Usiku Unaenda Msalani Nje Ukutane Na Lijitu limepak mavitu meupe Usoni..halielewek..Unashangaa Nalo Limekukazia Macho utajiuliz Mara mbil mbil aliyeko mbele yangu Ni Nani?..
Kitu Kiliniacha Na Bumbuazi Hadi Leo.Yule Ni either alitaka antishe au dawa zake ziliisha Nguvu Sabab mm Sina Nguvu yoyote ya kumwona mchawi Na Nlikuwa Bado Dogo
 
Usiombe ufanikiwe kibiashara halafu bahati mbaya upate mtoto ana mtindio wa ubogo au ulemavu.
Wewe tayari jamii itasema umemfanya msukule.
Wanapotoa habari ni washirika wenzake! Duniani hakuna siri ndg.
Miaka ya 2010 ilikuwa niondolewe, jina langu lilikataliwa kwa kuwa sikuwa ndugu wa damu wa mtoaji.

Badala yangu alitolewa ndg wa damu wa mtoaji.

Nilijulishwa baadaye sana na mtu iyensindikiza (msiri) huyo mtoaji kwa mganga; na hakuniambia moja kwa moja, Bali alimwambia mwenza wangu ".....ana bahati sana, jina lilikataliwa .....". Pia alifanya hivyo akijua mimi sio mtu wa shari, Kwa kuwa aliwahi nidhulumu kiwanja, wala hata sikunshtaki kwenye familia. Nilipotezea tu.

Omba ktk familia kusiwe na mtu mwenye roho ya kutoa kafara, atawamaliza wote.
 
Back
Top Bottom