Unawakumbuka watangazaji gani enzi hizo pale RFA na KISS FM?

Dah RFA miaka ya mwisho ya 90 naisikia kwa upande wa Dar nazikumbuka sauti za Double G, Isaack Gamba, Nkamiti Juma, Rahabu Fungo, Deo Kiduduye (R.I.P), Zubeir Msabaha (R.I.P, Rebeca Mulesi na Kid Bway
 
Stella situmbi
Roy maganga
Japo hukumuweka kwa list yako lakini Samadu Hasani (Marehemu) alikuwa bora kabisa wa usimulizi wa habari..
1. Fredwaa
2. Ahmed Juma Baragaza
2. Wambura Mtani
 
2000-2007
Fred wa,Rahabu fred,Kid bwoy,Glory Robinson,Doekaji Makomba,Juma Ahmed Baragaza,Zuberi Msabaha,Prince Kamukulu,Anko Sam,Beatrice Rabat,Stella Situmbi,Dj John, Baruan Abdallah Muhuza, nk

Sidhani kama itatokea tena ktk tasnia ya habari kuwa na muunganiko wa vipaji kama hivi, walikuwa na maadili, hii ndo ilikuwa RFA.

Vpindi vikali kama Vodacom burudani zaidi,RFA Bonanza,Show time,Mambo mambo,Je huu ni uungwana?,Duniani wiki hii,Weekend Fever,Bolingo time,Uliza ujibiwe,SITASAHAU,Reggae,watoto,
Tunamiss sana tukiokuwa wadau wa RFA.
 
 
Retrace NYERERE yuko wp mkuui?
 
Kumbe Irene Tylla alianzia Kiss FM? Mwaka gani alianza na kuacha na kwenda EA Radio?

Tobby Ze Splash na Stivie Kabuye ni Shida.

Baragaza/wambura mtani ni shidaaa Je huu ni ungwana /Sitasahau Jumanne Magasha
Tobby The Splash jamaa alikua na English tamu sana sijawahi ona aiseeeee
 
RFA na KISS FM walitangulia baada ya Redio one. Tatizo hawakuwa na Activity za kuengage society na maTamasha.
Kama Fiesta na Wasafi festival.
Kumbuka Redio inawakilisha sense Moja tu Kusikia.
Unapoongeza na Visual na Physical inakua business balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…