Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Jumamosi iliyopita tulikuwa na semina kanisani kwetu, semina hiyo iliyohusu mambo ya mahusiano mapenzi hadi ndoa ilichangamsha sana vijana wanaosubiria ndoa, maswali mbalimbali yaliulizwa na wanasemina wa jinsia zote. Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa kulikuwa na swali moja zuri sana ambalo liliulizwa na binti moja muhanga wa kuachwa na wachumba wapenda ngono kabla ya ndoa. Swali lilitanguliwa na maelezo mafupi kama ifuatavyo.
Binti : Mwalimu, mimi ni binti mwenye umri wa miaka 27, Nimewahi kuchumbiwa na wanaume 3 kwa nyakati tofauti maishani mwangu. Hao wote niliishia kuachana nao kwa sababu nilikataa kulala nao kabla ya ndoa . Bado sijaolewa hadi sasa. Kwa kuachana na hao wachumba 3 nimekuwa nikisumbuka sana kwa kujiuliza hili swali a mbali ni hili "Je naweza kupata mwanaume ambaye hatanishawishi nifanye naye ngono kabla ya ndoa?"
Mwalimu: Pole sana mpendwa kwa hiyo changamoto. Kiukweli hata kama ungelala nao wangekuacha tu. Kwa kuwa wangekutumia kingono kutimiza tamaa zao kisha wangekukimbia na kukuacha unaumia kihisia kwa kuwa ungekuwa umetumika kingono na kutupwa pasipo kuolewa.
Katika hali yoyote ile, unatakiwa usipunguze kiwango chako cha maadili kwa kukubali kuchezewa na wanaume wasio na maadili walio na tamaa ya kukufanya chombo cha kutimizia tamaa zao tu. Mwanamume anayetaka kukuoa kwa dhati huvutiwa na maadili yako na si vinginevyo.
Swali lako nalijibu hivi : UNAWEZA KUPATA MWANAUME WA KUKUOA AMBAYE HATAKUSHAWISHI UFANYE NAYE MAPENZI KABLA YA NDOA.
Kupitia Mungu utapata Mwanaume wa Kukuoa aliye mkomavu wa maadili. Siku zote, Mungu ni mwaminifu na anaheshimu uaminifu wa mtu mwaminifu. Achana na hofu.Hujachelewa. Tulia na uendelee kukomaa katika maadili na Mungu atakupatia mume mwema.
Mwenza mwema huletwa na BWANA.
Binti : Asante mwalimu kwa kunielewesha na kuwaelewesha wote waliowahi kupata changamoto kama yangu.
Mwalimu :Mbarikiwe nyote.