Unaweza kupata mwanaume wa kukuoa ambaye hatakushawishi ufanye naye ngono kabla ya ndoa

Unaweza kupata mwanaume wa kukuoa ambaye hatakushawishi ufanye naye ngono kabla ya ndoa

Jumamosi iliyopita tulikuwa na semina kanisani kwetu, semina hiyo iliyohusu mambo ya mahusiano mapenzi hadi ndoa ilichangamsha sana vijana wanaosubiria ndoa, maswali mbalimbali yaliulizwa na wanasemina wa jinsia zote. Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa kulikuwa na swali moja zuri sana ambalo liliulizwa na binti moja muhanga wa kuachwa na wachumba wapenda ngono kabla ya ndoa. Swali lilitanguliwa na maelezo mafupi kama ifuatavyo.

Binti : Mwalimu, mimi ni binti mwenye umri wa miaka 27, Nimewahi kuchumbiwa na wanaume 3 kwa nyakati tofauti maishani mwangu. Hao wote niliishia kuachana nao kwa sababu nilikataa kulala nao kabla ya ndoa . Bado sijaolewa hadi sasa. Kwa kuachana na hao wachumba 3 nimekuwa nikisumbuka sana kwa kujiuliza hili swali a mbali ni hili "Je naweza kupata mwanaume ambaye hatanishawishi nifanye naye ngono kabla ya ndoa?"

Mwalimu: Pole sana mpendwa kwa hiyo changamoto. Kiukweli hata kama ungelala nao wangekuacha tu. Kwa kuwa wangekutumia kingono kutimiza tamaa zao kisha wangekukimbia na kukuacha unaumia kihisia kwa kuwa ungekuwa umetumika kingono na kutupwa pasipo kuolewa.

Katika hali yoyote ile, unatakiwa usipunguze kiwango chako cha maadili kwa kukubali kuchezewa na wanaume wasio na maadili walio na tamaa ya kukufanya chombo cha kutimizia tamaa zao tu. Mwanamume anayetaka kukuoa kwa dhati huvutiwa na maadili yako na si vinginevyo.

Swali lako nalijibu hivi : UNAWEZA KUPATA MWANAUME WA KUKUOA AMBAYE HATAKUSHAWISHI UFANYE NAYE MAPENZI KABLA YA NDOA.

Kupitia Mungu utapata Mwanaume wa Kukuoa aliye mkomavu wa maadili. Siku zote, Mungu ni mwaminifu na anaheshimu uaminifu wa mtu mwaminifu. Achana na hofu.Hujachelewa. Tulia na uendelee kukomaa katika maadili na Mungu atakupatia mume mwema.

Mwenza mwema huletwa na BWANA.


Binti : Asante mwalimu kwa kunielewesha na kuwaelewesha wote waliowahi kupata changamoto kama yangu.

Mwalimu :Mbarikiwe nyote.
Kama bikra sawa ila kama wamekutoboa usiniambie habarii hizo
 
Mazingira yenu ndo chachu haswa katika kufanya au kutofanya kabla ya ndoa.
Ondoa neno "mazingira yetu" kisha weka "mporomoko wa maadili " hapo itaeleweka wazi kuwa kufanya au kutofanya kabla ya ndoa hutegemeana na mhusika (hasa ke) kulelewa nje ya maadili.

Na ndio maana wanawake wengi wa aina hiyo huchezewa mno na wanaume kisha huachwa.
 
Sex before marriage dini zote na mila pia zinapinga jambo Ili KWA faida ya jinsia zote mbili.
Ukifanya ngono na mtu unakuwa umeunganisha nafsi na mkiungana nafsi huwezi tambua mabaya ya mwenza, sababu ya ule msukumo wa nyege, nyege sio upendo. Nyege uisha miezi 3 ya ndoa na kuona kawaida tu, ndipo tabia uonekana, tabia ndio ufanya ndoa kudumu au kutodumu.
Tabia ni matokeo ya malezi.
 
Ndoa Haina formula mara nyingi ni kitu kigumu kujua kitakuaje mbeleni.

Kuna ambao walioana bila kusex kabla ya ndoa na wakapata magarasa na ndoa zikafika ukingoni.

Kuna waliooana baada ya kusex sana na na hata wengine kusogezana na ndoa zao zinadumu kwa mafanikio na furaha.

Ndoa ni fumbo ambalo Halina majibu na utatoa tu majibu kutegemea uko wapi na nani ila uhalisia unabaki palepale hakuna formula ya ndoa haipo.

Matatizo ya ndoa yanawakumba watu wote na haitegemei Imani yao zaidi Ili kukutwa na changamoto za ndoa ila namna ya kutatua hizo changamoto ndio inatofautiana.
Kwa wasio wakristo huita matatizo/migogoro ya ndoa.
Kwa wakristo huita majaribu

Matatizo na majaribu ni kitu kilekile ni mtazamo tu

Mungu atujalie hekima ya kutokariri maisha na majibu ya maswali ya maisha.
Umenena vyema ndoa na kifo havieleweki.
 
Sex before marriage dini zote na mila pia zinapinga jambo Ili KWA faida ya jinsia zote mbili.
Ukifanya ngono na mtu unakuwa umeunganisha nafsi na mkiungana nafsi huwezi tambua mabaya ya mwenza, sababu ya ule msukumo wa nyege, nyege sio upendo. Nyege uisha miezi 3 ya ndoa na kuona kawaida tu, ndipo tabia uonekana, tabia ndio ufanya ndoa kudumu au kutodumu.
Tabia ni matokeo ya malezi.
Umeeleweka mkuu
 
Back
Top Bottom