Unaweza Kupata Pesa kwa Kutumia AI Bila Kuacha Kazi Yako

Unaweza Kupata Pesa kwa Kutumia AI Bila Kuacha Kazi Yako

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888

Unaweza Kupata Pesa kwa Kutumia AI Bila Kuacha Kazi Yako​

1*H8X9cV0Q1qTV4KnoB2NzNg.png

Nafanya hivi, masaa 3 kwa siku ⏳💰

Watu wengi wanadhani lazima waache kazi ili waanze maisha mapya ya kujiajiri online.


Mimi nilifikiri hivyo pia.

Ukiangalia mitandao, unaona Influencers, wafanyabiashara, watu wa YouTube, wataalam wa AI, wanaonekana kama wote wanafanya kazi zao full time.

Lakini hiyo si kweli kabisa!

Mimi sijaacha kazi.
Lakini ninatumia AI kufanya kazi na kupata pesa.​



Masaa matatu tu kwa siku (Saa mbili mpaka saa tano).

Na mimi si mtaalamu wa kompyuta, sina digrii ya sayansi ya kompyuta. sijui kufanya mambo makubwa ya computer, wala sikuandika hata mstari mmoja wa programing.

Nilichofanya ni kuruhusu AI kunisaidia kutengeneza pesa huku bado nina mshahara wangu wa kawaida. (AI is the new programing language)

Jinsi nilivyoanza​

Siku moja nilikuwa kwenye meeting tukijadiliana mambo ya kazi. Akili yangu ilikuwa imechoka. Nikajiuliza: Hivi kweli haya ndiyo maisha?

Kazi, meeting, Kahawa, Kulala, NA kurudia tena.

Lakini moyoni nilijua nataka zaidi. Nilikuwa naogopa kusema hivyo wazi.
Maana una kazi, unalipwa, unajiona kama umefika au umefanya kila kitu.

Ndani ya nafsi yako, unajua hutaki kubaki hapo miaka mitano ijayo ukiangalia wengine wakitengeneza pesa mtandaoni.

Na unajiambia, “nitajaribu siku moja.”

Ile siku moja ndiyo inakuchelewesha!

Huna Lazima Kuacha Kazi Kuanza​

Ngoja nikueleze ukweli:

Hunahitaji kuacha kazi yako ili kuanza kutafuta pesa mtandaoni.
Hunahitaji kuhatarisha kila kitu.
Hunahitaji hata masaa mengi masaa mawili au matatu kwa siku yanatosha.

Kinachotakiwa ni ushahidi kuwa njia hii inafanya kazi.

Na mimi nina ushahidi.

Jinsi Ninavyotumia Masaa Matatu kwa AI​

Kila siku, baada ya kazi, nakaa chini kwa masaa mawili.

🚫 Hakuna kupoteza muda kwenye TikTok au movies.
✅ Naweka akili yote kwenye kazi.

Nafanya hivi:

✅ Natumia ChatGPT na Claude AI kuandika maudhui kwa ajili ya huduma na bidhaa zangu.
✅ Naandika makala, x posts, thread, Likedin posts, na maelezo ya bidhaa.
✅ Napata wateja kupitia Twitter, Reddit na Linked in. (Nafanya affiliate marketing)
✅ AI inanisaidia kufanya kazi 80%, na mimi nakamilisha kwa uangalifu.
✅ Ninalipwa $250 hadi $500 kulingana na bidhaa ulizouza. Kuna muda napata pesa zaidi.

Sina website, sina followers wengi. Ninatumia AI tu

Ni AI, na masaa matatu ya kuwa serious.

Kinachokuzuia Kuanza Ni Nini?​



Si kazi yako. Ni hofu.

Hofu ya kushindwa. Hofu ya kuonekana mjinga. Hofu ya kupoteza muda.

Lakini ukweli ni huu: tayari unapoteza muda kwa kutokujaribu.

Ilinichukua muda mrefu saa kuanza nikifikiri kuna siku nitajikuta niko tayari.
Lakini siku nilipopata dola 100 ya kwanza kwa kutumia AI, mambo yote yalieleweka.

Huu si uchawi. Ni hesabu rahisi: unasaidia mtu kuokoa muda au kupata pesa. Wanakulipa. Unatumia AI kuharakisha kazi.

Unataka Kuanza? Fanya Haya Kwanza​

✅ Chagua jambo moja unaloweza mfano: Kuandika? Kuchora? Kuongea na watu? Anza hapo. (Ukishindwa nitafute nikupe ushauri)
✅ TumiaAI ikurahisishie kazi: tumia ChatGPT au Claude.
✅ Tengeneza huduma: usianze kutengeneza kozi au YouTube, toa msaada kwa watu moja kwa moja.
✅ Tafuta wateja: Twitter, Reddit, groups za Facebook.
✅ Anza kimya kimya bila kuwaambia watu wanaokufahamu.

Ndivyo nilivyoanza, mambo mengine unajifunza mbele ya safari.

Watu Wengi Bado Watabaki Hawana Pesa​

Ukifika mwaka 2025 huna kipato cha ziada kupitia AI?
Ni kwa sababu umeamua kubaki hivyo.

AI sasa imefungua njia kwa kila mtu. Huhitaji digrii. Huhitaji kuwa mtaalamu.
Unahitaji tu kujifunza kutumia zana hizi.

Kwa sababu ukweli ni huu:

AI haitakufuta kazi. Lakini mtu anayetumia AI atakushinda.​



Ukiweza kutengeneza dola 50 au dola 100 ya kwanza, pesa ya kwanza utakayopata mtandaoni itakufungua macho.

Ukweli Ni Huu…​

Mtu yeyote yule anaweza kufanya kazi online kwa kutumia AI

Unaweza pia.
Unahitaji tu kuanza hata kama hujajua kila kitu bado.

Hakuna mtu anakuja kukuokoa.

Lakini AI inaweza kukusaidia kujiokoa.

Anza sasa.
 
Mimi Al inaniingizia Hadi 50,000-100,000 kwa wiki , naitumia kuandaa documents mbalimbali,za watu kufanya maombi ya kazi, kutengeneza matangazo ya kazi,kuunda CV ,cover letter,n.k
 
AI inanisaidia kupata majibu yote ya maswali au matatizo uhitaji kuuliza watu AI ni jibu
 
Uhuni tu kama wa heche na lisu

USSR
 
Back
Top Bottom