Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

1. Ukipewa simu kama unaoneshwa pengine picha, tazama kisha rudisha na sio kuendelea kutazama picha zingine.

2. Ukipiga simu kama haitopokelewa, tuma meseji na sio kupiga mara nyingi hususani kama jambo sio dharura.

3. Ukipigiwa simu baada ya maongezi, usikate simu... Acha akate aliyepiga.

4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

5. Ongezea................
5.Ukienda ukweni nenda na hela.
 
Hiyo number 3 unaweza kuacha kukata kumbe aliyekupigia naye kasahau kukata,ghafla anaanza kukusagia kunguni kwa watu aliokaa nao.

Mimi tukimaliza maongezi lazima nikate simu chap.Haijalishi nimepigiwa au nimepiga mwenyewe 😅
 
...unapokuwa na appointment na mtu/watu, hakikisha unaenda kwa wakati. La kama utashindwa kwenda, wajulishe mapema ili waendelee na mambo mengine.

...Panga mipango yako ya siku, usifanye mambo kwa kubahatisha.

...usitumie pesa ovyo, dunia ya sasa sio ya kijamaa, ni ubepari ambao kama ukichezea ukwasi wako leo huenda ukaja kujuta badae.
 
Usimle demu wa mshkaji uliemzidi parameters za kimaisha kama Hela, connections, muonekano na vngn

Usiongee madhaifu ya wanao

Usikosoe in public vitu ambavyo ni starehe kwa wengine mfano kitimoto, kununua malayer, kutumia bange na Shisha .....kama ww huvitumii bas havijaletwa kwa ajili yako we endelea kunywa chai ya rangi saa saba mchana
 
4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

Hilo nalo neno:

Je, yeye alikopeshwa kwa kupewa cash au kwa njia ya simu/bank.

Kama alipewa cash, arudishe cash. Akirudisha kwa njia nyingine aongezee na gharama ya makato.

Kama alipewa kwa kutumiwa, arudishe kiasi kile kile alichotumiwa kwa njia ile ile aliyopokea, otherwise wakubaliane kivingine.
 
Watu wanavyotiririka pointi humu utasema sio wao ambao ukiwakopesha fedha, hawarudishi hadi wanakuzimia na simu kabisa ama kukublock🙌

Mtu anakuja nyumbani kwako bila taarifa, anakukuta unakula zako, nawe unazuga kumkaribisha chakula naye anakuja kula hadi chakula kinaisha chote mnaishia kunywa Maji Lita 1 Moja ili kujaza tumbo 😅 🙌

Watanzania sio Waungwana kabisa
 
Kwanza unamuonesha wa nini, muelezee kwa maneno tu 🤓
Sa ingine unakuta ni kitu kinachekesha anaona unajichekea anauliza unacheka nini unamwonyesha anataka aangalie kwa karibu unampa simu huyo anazama kuangalia galleri.
Nilimpokonya nikamkoromea sana.
Anyway hashiki mtu simu yangu siku hizi.
Akiuliza natuma link tu.
 
Back
Top Bottom