Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

1. Ukipewa simu kama unaoneshwa pengine picha, tazama kisha rudisha na sio kuendelea kutazama picha zingine.

2. Ukipiga simu kama haitopokelewa, tuma meseji na sio kupiga mara nyingi hususani kama jambo sio dharura.

3. Ukipigiwa simu baada ya maongezi, usikate simu... Acha akate aliyepiga.

4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

5. Ongezea................
Mkuu,

Shukurani kwa mafunzo.

Namba 3 hapo vipi kama aliyekupigia hamalizi maongezi anaweza kuongea zaidi ya masaa mawili mambo ambayo unaona hayana tija?
 
Nilifundishwa kwenye miadi usiwahi zaidi ya dakika 15, na usichelewe zaidi ya Dk 5.

Huenda ni mambo ya kizamani najitahidi kuzangatia hili nikiwa na miadi.
 
Watu wanavyotiririka pointi humu utasema sio wao ambao ukiwakopesha fedha, hawarudishi hadi wanakuzimia na simu kabisa ama kukublock🙌

Mtu anakuja nyumbani kwako bila taarifa, anakukuta unakula zako, nawe unazuga kumkaribisha chakula naye anakuja kula hadi chakula kinaisha chote mnaishia kunywa Maji Lita 1 Moja ili kujaza tumbo 😅 🙌

Watanzania sio Waungwana kabisa
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom