Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

...ukienda kwa mtu mda wa chakula, kama hamkuwa na miadi na unaona kabisa menu iliyopo haiwezi kukodhi wao na wewe, vunga tu, omba maji au juice.
Weeeeh acha uchoyooo, tutagawana hicho hicho.
 
...ukienda kwa mtu mda wa chakula, kama hamkuwa na miadi na unaona kabisa menu iliyopo haiwezi kukodhi wao na wewe, vunga tu, omba maji au juice.
Kwamba hata ukikaribishwa msosi kwa msisitizo wenye nia ya kweli utavunga unaangalia teevee kwa umakini mkubwa?😎
 
Unapokuwa na safari ya kumtembelea mtu hakikisha umevua viatu mlangoni.
NB;Kwa wavaao soksi hakikisha una pairs nyingi,unabadilisha na ziwe safi hazijatobokatoboka.
 
1. Ukipewa simu kama unaoneshwa pengine picha, tazama kisha rudisha na sio kuendelea kutazama picha zingine.

2. Ukipiga simu kama haitopokelewa, tuma meseji na sio kupiga mara nyingi hususani kama jambo sio dharura.

3. Ukipigiwa simu baada ya maongezi, usikate simu... Acha akate aliyepiga.

4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

5. Ongezea................
Hakikisha unashiriki katika shughuli za furaha pia kwa ndugu, jamaa na marafiki wengi wanatoa kipaumbele kwenye majanga tu

Anaweza akatoa mchango ila asifike kwenye shughuli ni muhimu kushiriki kote kote
 
Back
Top Bottom