Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Usiende nyumbani kwa mtu/watu bila kutoa taarifa.
 
1. Ukipewa simu kama unaoneshwa pengine picha, tazama kisha rudisha na sio kuendelea kutazama picha zingine.

2. Ukipiga simu kama haitopokelewa, tuma meseji na sio kupiga mara nyingi hususani kama jambo sio dharura.

3. Ukipigiwa simu baada ya maongezi, usikate simu... Acha akate aliyepiga.

4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

5. Ongezea................
Namba 4 hiyo naifanya sana.
Lazima nikutumie na pesa ya kutolea
 
mke/mchumba akisema mmemalizana usimdhalimishe mrudiane utaumia zaidi
 
Nilikuwa na girlfriend unakuta mie ndio napiga simu tummemaliza maongezi halafu yy anakata.kuna siku alikata nilikaa bila kupiga akawa anapiga yy tu mpaka siku akaniuliza kulikoni napiga mm tu nikamwambia mm siwezi kukupigia simu halafu ukate ww as if ww ndio umekata.
Uhafidhina huu
 
1. Ukipewa simu kama unaoneshwa pengine picha, tazama kisha rudisha na sio kuendelea kutazama picha zingine.

2. Ukipiga simu kama haitopokelewa, tuma meseji na sio kupiga mara nyingi hususani kama jambo sio dharura.

3. Ukipigiwa simu baada ya maongezi, usikate simu... Acha akate aliyepiga.

4. Ukikopeshwa pesa, unaporudisha kama ni kwa njia ya simu hakikisha unaongeza na kiasi cha makato atayokatwa wakati anatoa au mpe cash.

5. Ongezea................
huu ndio uungwana
 
Ukipewa ofa ya kula mgahawani/hotelini usizidishe bili/bajeti. Ukipewa chapati mbili na kikombe kimoja ishia hapohapo
 
Back
Top Bottom