Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Kuna baadhi ya sehemu usipokula chakula cha msibani unaonekana una dharau na wako radhi kwenye msiba wa nyumbani kwako wote wakufanyie hivyo (wasile na kuondoka). Uswahilini kuna mambo mengi sana
huku kwetu sio uswahilini,,ila ukijifanya huli chakula wanakaa kimya,,sasa siku likukute utajuta,,yaani wanapika misosi kama kawaida wanaenda kuzika,wakitoka apo ni nyumbani wanakuacha na masufuria yako apo.
 
Unakuta mtu anapiga anapiga weeh,anapiga tu misscall 10,hapo we hupokei labda uko na Boss mnaongea mambo ya maana kikazi,
Unajiuliza huyu jamaa ananidai hapana.
Unamshtua boss nna udhuru ngoja nipokee nakuja.
Khee unapokea jitu linaanza kukufokea.
Mi napiga hupokei mara zote hizo.
Ongea unasemaje? linajichekesha eeh "nilikua nakusalimia tu"
Kubababandeki,malaka maleke,maluku🤢
Unatamani lingekua karibu ulizabue makofi aisee.
Unarudi bosi anauliza vp kuna tatizo.
Inabidi useme yah nishamaliza.
Kumbe tatizo ni matako mmoja anasumbua tu ili agongee umtoe.
 
Unakuta mtu anapiga anapiga weeh,anapiga tu misscall 10,hapo we hupokei labda uko na Boss mnaongea mambo ya maana kikazi,
Unajiuliza huyu jamaa ananidai hapana.
Unamshtua boss nna udhuru ngoja nipokee nakuja.
Khee unapokea jitu linaanza kukufokea.
Mi napiga hupokei mara zote hizo.
Ongea unasemaje? linajichekesha eeh "nilikua nakusalimia tu"
Kubababandeki,malaka maleke,maluku🤢
Unatamani lingekua karibu ulizabue makofi aisee.
Unarudi bosi anauliza vp kuna tatizo.
Inabidi useme yah nishamaliza.
Kumbe tatizo ni matako mmoja anasumbua tu ili agongee umtoe.
Hahaha umeliongea Kwa uchungu sana hili mkuu, nahisi limekutokea mda mfupi tokea sasa .
 
Mm nipo tofauti na hayo aisee, alafu nai-enjoy kinoma

1) ukinipa simu nione picha lazima niangalie na mengine hadi msg nitazisoma

2) nikipiga simu usipopokea nakupigia hata mara 20, kila baada ya dk 5 nakupigia utakuta missed calls hata 100 na lawama juu

3)ukinipigia nikaona kuongea imetosha nakata wala sisubiri ww ndio ukate

4) ukinikopesha tu suala la kukulipa sahau
 
Nilikuwa na girlfriend unakuta mie ndio napiga simu tummemaliza maongezi halafu yy anakata.kuna siku alikata nilikaa bila kupiga akawa anapiga yy tu mpaka siku akaniuliza kulikoni napiga mm tu nikamwambia mm siwezi kukupigia simu halafu ukate ww as if ww ndio umekata.
 
Umekutana na mtu baada ya kuachana miaka mingi sana (>20), epuka kuuliza maswali kama haya
1. Umepungua sana siku hizi
2. Una watoto wangapi?
3. Unafanya kazi gani??
4. Umeshajenga? Nk nk nk
Hayo maswali ni ya wasio kuwa na hekima
 
Ukipewa Lift using'ang'anie kupiga honi au kujua geji ya mafuta ilipoishia😂😂
 
Ukienda kwa watu nenda mida ambayo unajua kua washakula tiyar
 
Back
Top Bottom