Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea kwa uchungu sana mkuu, na iwe kwako kama ulivyoomba. Mungu hadhihakiwi.Leo kwa Mara ya kwanza nimekutafakari kwa kina na kukuelewa tofauti. Nadhani hata baadhi ya maandiko yako huwa ni katika hali ya kisiasa tuu lakini huna roho ya korosho kama nilivyo dhani awali.
Kama kweli iishivyo, na Mbowe yupo kitandani anaugulia maumivu makali namna ile na bado wenzake (wabunge) wapo wanaosimama na kumkejeli kwa vijembe na matusi kwa ruhusa ya Spika basi Mungu atatenda jambo ASAP kabla hata bunge hili halijavunjwa wiki ijayo ili mafundisho yake yapate kutimia.
Nimeona sura ya PM Majaliwa akiwasikiliza kina Lijualikali kwa mshangao na majonzi lakini Spika akichekelea na kuchombeza bila aibu.
Baba wa mbinguni twajua yaweza kuwa Mbowe ni mdhambi kama sisi wanadamu tulivyo, lakini twajua amejitoa kwa mengi sana kwa watu wako kuliko sisi. Usiache maumivu ya kejeli hizi yapite hivihivi bila kumjibia kwa waliotoa kejeli nao kuwapa vilio vya uchungu kabla hatujasahau.
Amen