Unawezaje kuishi Kwa kutegemea kuendesha bodaboda

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Huwa nashangaa sana unakuta mtu anakuambia. Nalisha familia kupitia hii bodaboda aisee ukicheki yeye mwenyewe alivyojichokea sijui hiyo familia yake itakua katika Hali Gani mpaka kumruhusu ndugu Yao kuingia barabarani kucheza na moto ambao hautozimika ukimkumba maana bodaboda ni kitendo Cha dakika 1 unaitwa kilema au maiti, hii kazi siwezi kuifanya
 
Ulitaka awe jambazi aje kukuua na kukupora?
 
Kijana jiheshimu! Shughuli yoyote halali ni kazi ili mradi mkono uende kinywani. Watu tunasomesha na tumejenga kwa shughuli hii hii ya bodaboda.
 
Kaa kimya wewe mtoto wa Masaki. Hujui shida wewe. Hujui dhiki wakishua wewe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…