Undumilakuwili huu wa TEC na Kitime mpaka lini?

Kitima na Maaskofu wamezingua.

Haijulikani wao ni moto au baridi.
Miezi kibao wametoa maneno kuonyesha ubovu wa uchaguzi uliopita, kwamba hakukuwa na uchaguzi halafu leo wanatwambia eti tumtambue rais. Na sababu wanayoitoa eti ni kwa kuwa rais keshaapishwa.

Kwanza kwa nini hawakuitoa kauli siku hiyo hiyo aliyoapishwa?.

Pili kwa nini waliendelea kutoa matamko ya kumdescredit rais hadharani mbele ya wananchi kama walikuwa wanajua rais akishaapishwa aheshimiwe?

Tatu hiyo hoja ya kuapishwa inaishinda vipi nguvu hoja ya kuwa rais lazima apatikane kwa ridhaa ya wananchi?. Kipi chenye nguvu zaidi, mtu kuapishwa au kupatikana kwa ridhaa ya wananchi?.

TEC wajitafakari, Je wanahalalisha batili au wasimame kuhesabiwa ili rekodi iingie kwenye kumbukumbu.
 
Hakuna undumilakuwili au undumila kutatu.

Hii inaitwa kutesa kwa zamu. Sarafi hii ni zamu ya kobaz kula kwa fujo.

Kuleni vya bure vya Watanganyika.
 
Ccm ni Mali ya TEC tangu zamani na Nyerere ni kijana wao!!

Katiba iliyomwaga damu October 29 ilikuwepo tangu 1977 wao ndio wapishi wa katiba mbovu kupitia Nyerere na wao wamefurahia matunda haya tangu uhuru!

Leo samiah katumia ubovu ule ule wa katiba kufanya Yale yale aliyofanya Mzee mkapa na jpm Zanzibar kwenye vugu vugu la chaguzi anaonekana mbaya!!
Wakati katiba ilisimamiwa na kijana wao ndani ya chama chao!!

TEC wametukosea sana,

Baada ya kuona katiba ile Ile imetumika hata kuwaponda madhabahuni na wakapigika Hadi kulazwa ndio wamekuja na ngonjera za kua upande wa wananchi kudai katiba!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…