Mada hii itakuwa inakuletea updates zote zinazopangwa na US akishirikiana na Israel dhidi ya Iran Hadi siku ambayo Iran itaenda kupigwa......
Toka juzi kuna zaidi ndege 6 hatari za kivita za B-2 bomber zimewasili tayari Huko DIEGO GARCIA AIR BASE.
Tukumbuke DIEGO GARCIA ni kisiwa kilichopo katika bahari ya Hindi kinachomilikiwa na UK - US Kwaajili ya mambo ya kijeshi
Sifa pekee za ndege hizi za B-2 bomber zina uwezo mkubwa wa kubeba makombora mazito ya GBU-57 yenye uzito wa tani 13 yaani uunganishe uzito wa mabus mawili ya Abood au Allys star.
DIEGO GARCIA AIR BASE IPO umbali wa miles 200 kutoka Iran,umbali huu inaifanya US NAVY kuwa na muda mzuri wa kujilinda na ndege za Iran, ballistic na drones pia itakuwa rahisi Kwa B-2 bomber kufanya mashambulizi ndani ya Iran na kurudi... Tukumbuke Iran nao sio wajinga ndiyo maana wamejenga base zao chini ya miamba na kwenye safu za milima hivyo inakuwa ngumu kuzifikia ngome zake.
Ila Kwa uwezo mkubwa wa mabomu ya GBU-57 wanaweza kupenya kwenye ngome yeyote Kwa umbali wa Mita 60 - 130 kwenda chini ya ardhi na miamba migumu.
Kwa mfano ngome zilizopo katika miji ya NATANZ NA FORDOW zipo chini Sana zaidi ya Mita 100 Hadi 180 chini ya ardhi huku mabomu ya GBU-57 yanaweza kupenya Kwa Mita 130(ili kuvunja ngome hizi lazima yatumike mabomu mengi ya kutosha)
Jana ndege 9 za KC-135 Ambazo kazi yake kubwa ni kujazia mafuta fighter jet zikiwa angani yaani Kwa lugha nyepesi hizi ndege ni vituo vya mafuta kama Puma,total,lake oil na nyinginezo,hizo ndege zote zimeshawasili tayari DIEGO GARCIA Kwaajili ya kazi ya kuichakaza Iran
Pia Jana hiyohiyo kuna fighter jets zaidi ya 100 za F-35,F-15 na F-18 zimeshawasili ndani ya nchi za UAE, QATAR, JORDAN,SAIDI ARABIA ikiwemo ndege zingine za USS Truman hizi zote zitatumika kupiga base zingine Ambazo zinatengeneza ballistic na silaha zingine za hatari za Iran
Ukiangalia Kwa jicho la tatu utaona kabisaa jinsi Iran inaenda kuzingirwa Kwa pande zote yaani hii inaitwa MTU kati
Hata Ile US AIR FORCE MOBILITY (AMC) imeondoka OSAN AIR BASE Huko South Korea kwenda kuongeza nguvu hapo mashariki ya Kati sio hivyo Tu Bali kuna ndege nyingine inayobeba vifaa vya ulinzi wa anga zimewasili tayari asubuhi ya Leo Huko ISA AIR BASE BAHRAIN, hizi ni ndege kubwa ya mkakati yenye kubeba "terminal high altitude area defence, Us army's MIM-104 patriot pamoja na surface -to-air missile system
Vifaa hivi vya ulinzi vilifanya kazi kubwa Sana kipindi kile ambacho iran alikuwa anapiga Israel
View attachment 3291074