Correspondence
JF-Expert Member
- Mar 29, 2025
- 310
- 313
🤣😂Iran labda apigwe kwa advanced technology zilizopo pale nevada area 51, Kama tetemeko la ardhi.
🤣😂Iran labda apigwe kwa advanced technology zilizopo pale nevada area 51, Kama tetemeko la ardhi.
Ulivyo mshamba unafikiri mgogoro huu ni wa Yesu!!!USA = Walokole (Wanamjua Yesu)
ULAYA MASHARIKI = Wakatoliki (Wanamjua Yesu)
ULAYA MAGHARIBI = Waprotestant (Wanamjua Yesu)
IRAN = Washia (Wanamjua Yesu)
SAUDIA = Wasini (Wanamjua Yesu)
ISRAEL = Judaisum (Hawamjui Yesu)
Walokole vs Washia Wote wafuasi wa Yesu bin Mariam
Kwani kafanyaje Iran mpaka aandaliwe mabomu yote hayo?Mada hii itakuwa inakuletea updates zote zinazopangwa na US akishirikiana na Israel dhidi ya Iran Hadi siku ambayo Iran itaenda kupigwa......
Toka juzi kuna zaidi ndege 6 hatari za kivita za B-2 bomber zimewasili tayari Huko DIEGO GARCIA AIR BASE.
Tukumbuke DIEGO GARCIA ni kisiwa kilichopo katika bahari ya Hindi kinachomilikiwa na UK - US Kwaajili ya mambo ya kijeshi
Sifa pekee za ndege hizi za B-2 bomber zina uwezo mkubwa wa kubeba makombora mazito ya GBU-57 yenye uzito wa tani 13 yaani uunganishe uzito wa mabus mawili ya Abood au Allys star.
DIEGO GARCIA AIR BASE IPO umbali wa miles 200 kutoka Iran,umbali huu inaifanya US NAVY kuwa na muda mzuri wa kujilinda na ndege za Iran, ballistic na drones pia itakuwa rahisi Kwa B-2 bomber kufanya mashambulizi ndani ya Iran na kurudi... Tukumbuke Iran nao sio wajinga ndiyo maana wamejenga base zao chini ya miamba na kwenye safu za milima hivyo inakuwa ngumu kuzifikia ngome zake.
Ila Kwa uwezo mkubwa wa mabomu ya GBU-57 wanaweza kupenya kwenye ngome yeyote Kwa umbali wa Mita 60 - 130 kwenda chini ya ardhi na miamba migumu.
Kwa mfano ngome zilizopo katika miji ya NATANZ NA FORDOW zipo chini Sana zaidi ya Mita 100 Hadi 180 chini ya ardhi huku mabomu ya GBU-57 yanaweza kupenya Kwa Mita 130(ili kuvunja ngome hizi lazima yatumike mabomu mengi ya kutosha)
Jana ndege 9 za KC-135 Ambazo kazi yake kubwa ni kujazia mafuta fighter jet zikiwa angani yaani Kwa lugha nyepesi hizi ndege ni vituo vya mafuta kama Puma,total,lake oil na nyinginezo,hizo ndege zote zimeshawasili tayari DIEGO GARCIA Kwaajili ya kazi ya kuichakaza Iran
Pia Jana hiyohiyo kuna fighter jets zaidi ya 100 za F-35,F-15 na F-18 zimeshawasili ndani ya nchi za UAE, QATAR, JORDAN,SAIDI ARABIA ikiwemo ndege zingine za USS Truman hizi zote zitatumika kupiga base zingine Ambazo zinatengeneza ballistic na silaha zingine za hatari za Iran
Ukiangalia Kwa jicho la tatu utaona kabisaa jinsi Iran inaenda kuzingirwa Kwa pande zote yaani hii inaitwa MTU kati
Hata Ile US AIR FORCE MOBILITY (AMC) imeondoka OSAN AIR BASE Huko South Korea kwenda kuongeza nguvu hapo mashariki ya Kati sio hivyo Tu Bali kuna ndege nyingine inayobeba vifaa vya ulinzi wa anga zimewasili tayari asubuhi ya Leo Huko ISA AIR BASE BAHRAIN, hizi ni ndege kubwa ya mkakati yenye kubeba "terminal high altitude area defence, Us army's MIM-104 patriot pamoja na surface -to-air missile system
Vifaa hivi vya ulinzi vilifanya kazi kubwa Sana kipindi kile ambacho iran alikuwa anapiga IsraelView attachment 3291074
Kwan wewe huamin kuwa Israel taifa fake la wazungu?Safari hii Iran kayakanyaga kibaya zaidi kwa uungaji wake wa magaidi wa Hamas,Hezbollah na Wahouth jamaa wameona kuwashinda magaidi hao ni mpaka wamponde kichwa nyoka ndiyo itakuwa salama. Binafsi Nina uhakika atapigwa tu na hakutakuwa na lolote.
Wafuga Midevu na Majini kila leo wanadai eti Israel ni Taifa fake la wazungu kauli inayotamkwa mara kwa mara na Viongozi wa Iran haiwezi kumzuia Ng’ombe kunywa maji. Watapiga kelele na usiku watalala.
Mimi siyo ZUZU kama wewe wa kuamini kila lisemwalo na Wafuga Midevu na Majini!!Kwan wewe huamin kuwa Israel taifa fake la wazungu?
Iran atapigwa ili kuondoa uwezekano wa kumiliki silaha za nyukilia,Iran itapigwa ili weje, ni kuondoa utawala wa maayatola au kuondoa kitisho mashariki ya kati?
Marekani kama yeye haitaji msaada wa NATO au Ulaya kumpiga roba IRAN.Hata Iraq alisema hivyo
Hao Iran unaowasema walishindwa kuzuia shambulizi la Wanawake wa IsraelSABABU kuuu kwann Marekani itamzuiya Tramp kuanzisha vita wenye ujuzi wa mambo ya Kijesh !!!!
kwanza akuna Faida mana uwezi angusha Utawala wa Iran kwa kushambulia angani !!!!
Ukipeleka Majeshi ya Ardhin Russia China lazima wajikite na ivyo ndio mwanzo wa vita ya Dunia !!!!
lkn apo apo kutokea Angani Ikiwa Iran inaweza kuzuiya Shambulizi kikamilifu Basi Marekani inaenda kwenye anguko kubwa itakuwa imejivua nguo yenyewe na kuingia asala kubwa ktk Biashara ya Silaha Dunian!!!! !!!
Washilika nao wataona akuna umuimu tena wa NATO na Marekani atabaki kwenye siasa za Uchumi tu lkn sio mambo ya Kijesh!!!
Kujiandaa kwa muda mrefu kwa Iran dhidi ya US hakuipi ushindi mzuri Iran dhidi ya US sababu US pia na washirika wake hasa Israel wamejiandaa muda mrefu pia dhidi ya Iran. Iran ndo nchi pekee tishio yenye itikadi za kufadhili magaidi, mbali na Iran hakuna taifa lingine lolote tishio kwa US na Israel na washirika wao.kumbuka tu vita ina hasara pande zote hata ukiwa mshindi ni lazima uwe umeumia vya kutosha
na siku zote kumshambulia mtu kwake inahitaji akili na nguvu za ziada zaidi mfano ni ISRAEL na HAMAS GAZA
So kaa tayari kwa lolote kwa7bu iran itakachowafanya ALLIED wote wa USA watakaoisaidia US wataumia zaidi
jambo jingine US kuishambulia IRAN nchini kwakwe inamaana Imetangaza VITA KAMILI ambapo IRAN imejiandaa hilo tangu 70s
Hii vita inaweza ikawa nzito sana na tukashuhudia mengi zaidi.Toka mwaka 1979 kumekuwa na mikwala mingi Toka Kwa pande hizi mbili lkn huyu mmoja amefungwa gerezani akijiaandaa na vita na mwingine yupo laboratory akijiandaa na vita huku akiweka military base kumzunguka aliyepo gerezani
Hivi hao Israel wamewakosea nini hadi mnawabagua kwa Yesu?😊USA = Walokole (Wanamjua Yesu)
ULAYA MASHARIKI = Wakatoliki (Wanamjua Yesu)
ULAYA MAGHARIBI = Waprotestant (Wanamjua Yesu)
IRAN = Washia (Wanamjua Yesu)
SAUDIA = Wasini (Wanamjua Yesu)
ISRAEL = Judaisum (Hawamjui Yesu)
Walokole vs Washia Wote wafuasi wa Yesu bin Mariam
Ulivyo mshamba unafikiri mgogoro huu ni wa Yesu!!!
NdiyoIran itapigwa ili weje, ni kuondoa utawala wa maayatola au kuondoa kitisho mashariki ya kati?
Anafadhili magaidi Houth, Hamas, Hezbolla na wengine.Kwani kafanyaje Iran mpaka aandaliwe mabomu yote hayo?
Hata mimi siaminiKwan wewe huamin kuwa Israel taifa fake la wazungu?
Sawa mkandala lufufu, mda ni mwalimu mzuri.Safari hii Iran kayakanyaga kibaya zaidi kwa uungaji wake wa magaidi wa Hamas,Hezbollah na Wahouth jamaa wameona kuwashinda magaidi hao ni mpaka wamponde kichwa nyoka ndiyo itakuwa salama. Binafsi Nina uhakika atapigwa tu na hakutakuwa na lolote.
Wafuga Midevu na Majini kila leo wanadai eti Israel ni Taifa fake la wazungu kauli inayotamkwa mara kwa mara na Viongozi wa Iran haiwezi kumzuia Ng’ombe kunywa maji. Watapiga kelele na usiku watalala.
Tatitizo usichokijua unaweza kuvianzisha vita, na bado ukashindwa kuvimaliza.Kujiandaa kwa muda mrefu kwa Iran dhidi ya US hakuipi ushindi mzuri Iran dhidi ya US sababu US pia na washirika wake hasa Israel wamejiandaa muda mrefu pia dhidi ya Iran. Iran ndo nchi pekee tishio yenye itikadi za kufadhili magaidi, mbali na Iran hakuna taifa lingine lolote tishio kwa US na Israel na washirika wao.
Pande zote mbili hizi, za Iran na Magharibi. Magharibi wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda sababu imepiga hatua kubwa ya kiteknolojia kijeshi, kiuchumi, kiushawishi n.k kuliko Iran. Kumbuka hata ile Helkopta ilomuua Rais Iran ilikuwa imetengenezwa US, F16 za Iran ni za US vile vile na bado zote hizo mpaka sasa zinatumika kijeshi na Iran. Kwa mbali unaweza kupata pisha Iran bado iko nyuma kwa namna gani dhidi ya adui zake.
Wakati huohuo, Iran ina maadui wengi wa kiislamu ambao wameshikamana na US, ikiwemo Saudi Arabia n.k mshirika mwenye nguvu kwa mbali ni Russia. Sasa kwa kuwaza tu, unafikiri ni rahisi Russia akaenda kumsaidia Iran? Jibu ni hapana, msaada utakuwa mdogo sana.
Ikiwa US, UK na Israel zikasuka karata zake vizuri, watakuwa na uwezo mkubwa wa kushinda.