Ungana nami katika kukuletea updates za maandalizi na mikakati ya US kuipiga Iran

Ulivyo mshamba unafikiri mgogoro huu ni wa Yesu!!!
 
Iran itapigwa ili weje, ni kuondoa utawala wa maayatola au kuondoa kitisho mashariki ya kati?
 
Kwani kafanyaje Iran mpaka aandaliwe mabomu yote hayo?
 
Kwan wewe huamin kuwa Israel taifa fake la wazungu?
 
Hata Iraq alisema hivyo
Marekani kama yeye haitaji msaada wa NATO au Ulaya kumpiga roba IRAN.
Iran ni mchanga.
Lakini Marekani chini ya Raisi Trump hatabiliki kama kweli anataka kumfanyia kitu mbaya Iran au ni miyeyusho na mikwala ili Iran akubali masharti ya kutotengeneza siraha za nuclear.
Anaekoleza chumvi si Marekani bali ni Israel ya Benjamin Netanyahu anaeamini kwamba usalama wa Israel ni kuondoa uongozi wa Iran na kuibadirisha kabisa kisiasa ama irudishe utawala wa Shah.
Lakini Saudia, Oman,UAE,Qatar,Misri, Jordan na nchi za waislamu wa Suni wanamwona Iran kama muhujumu wa dini kwa upande wao.
Kwanza Iran sio mwaarabu ni Muajemi.
Lakini Iran ni mshirika wa karibu na Urusi ya Putin,kwa kuwa Putin na Trump ni marafiki sana,sioni kama Trump atataka kufanya kweli.
Labda watafanya plan B ambayo mapinduzi ya uongozi nchini Iran ambacho ni jambo gumu sana.
 
Hao Iran unaowasema walishindwa kuzuia shambulizi la Wanawake wa Israel
 
Kujiandaa kwa muda mrefu kwa Iran dhidi ya US hakuipi ushindi mzuri Iran dhidi ya US sababu US pia na washirika wake hasa Israel wamejiandaa muda mrefu pia dhidi ya Iran. Iran ndo nchi pekee tishio yenye itikadi za kufadhili magaidi, mbali na Iran hakuna taifa lingine lolote tishio kwa US na Israel na washirika wao.

Pande zote mbili hizi, za Iran na Magharibi. Magharibi wana nafasi kubwa zaidi ya kushinda sababu imepiga hatua kubwa ya kiteknolojia kijeshi, kiuchumi, kiushawishi n.k kuliko Iran. Kumbuka hata ile Helkopta ilomuua Rais Iran ilikuwa imetengenezwa US, F16 za Iran ni za US vile vile na bado zote hizo mpaka sasa zinatumika kijeshi na Iran. Kwa mbali unaweza kupata pisha Iran bado iko nyuma kwa namna gani dhidi ya adui zake.

Wakati huohuo, Iran ina maadui wengi wa kiislamu ambao wameshikamana na US, ikiwemo Saudi Arabia n.k mshirika mwenye nguvu kwa mbali ni Russia. Sasa kwa kuwaza tu, unafikiri ni rahisi Russia akaenda kumsaidia Iran? Jibu ni hapana, msaada utakuwa mdogo sana.

Ikiwa US, UK na Israel zikasuka karata zake vizuri, watakuwa na uwezo mkubwa wa kushinda.
 
Hivi hao Israel wamewakosea nini hadi mnawabagua kwa Yesu?😊
 
Sawa mkandala lufufu, mda ni mwalimu mzuri.
 
Tatitizo usichokijua unaweza kuvianzisha vita, na bado ukashindwa kuvimaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…