Ungeishi vipi kama ungekuwa na jinsia tofauti na ya sasa?

Ungeishi vipi kama ungekuwa na jinsia tofauti na ya sasa?

Mara paah unaamka mwenyewe unajikuta una jinsia tofauti na hiyo uliyonayo sasa.

Yani kama wewe ulikuwa KE umebadilika kuwa ME na wale ME umekuwa KE.

Ungeishi vipi?

Ungefanya nini?

Haya sasa yuhuuu! Twende kazi
tangu nizaliwe sijawahi kuwa na mawazo ya aina hiyo kamwe, ukishaona unawaza kuwa jinsia nyingine jua kuna mdudu ameshakuingia. Mungu akusaidie.
 
Mimi ningezaliwa mwanaume ningefurahi infact sifurahii kivile kuwa mwanamke, maana kuna mambo napenda kuyafanya ambayo kwenye jamii yetu akifanya mwanamke inaonekana ajabu, ila akifanya mwanaume inaonekana kawaida tu

Kitu pekee kinachofanya nisitamani kuwa mwanaume ni tamaa ya ngono tu, maana inaonekana hiyo kitu inawaendesha sana ndugu zetu hadi kupelekea kuwa malaya zaidi kuliko wanawake, ambao hizo hamu hazituendeshi sana na tunaweza kujizuia

Ukitoa hilo suala la ngono mengine yote yanafanya nione bora kuwa mwanaume
 
Back
Top Bottom