"Ungekuwa Mzuri ungekuwa Umeolewa" kauli hii Wanawake wanapenda kuambiana inaukweli kiasi gani?

"Ungekuwa Mzuri ungekuwa Umeolewa" kauli hii Wanawake wanapenda kuambiana inaukweli kiasi gani?

Kila mtu huoa au huolewa na wa level yake,

Hakuna Mwanamke akawa mbaya kwa wanaume wote,suala la kuoa au kuolewa ni uamuzi wa mtu binafsi na pia hua ni riziki inayotoka kwa Mungu.

Lakini MTU anaweza kuikataa riziki Kutoka Kwa Mungu.
Yaani unapewa riziki yako lakini hauitaki Kwa sababu huridhiki nayo.
Vipi Hilo?
 
Kauli za wenye wivu tu isitoshe uzuri wa mtu uko machoni pa mtazamaji, tatizo watu wamegeuza kuolewa km hitaji la msingi kumbe sio kweli,

Labda km huyo mwanamke alikuwa ananata na kudharau ndoa halafu aanze kuhangaikia kuolewa hapo sasa waja tutampa ya kumpa,, na vicheko tutacheka

😀😀

Sasa kizuri kikikosa Mtazamaji kitaendelea kuwa Kizuri? Yàani Ipi faîda ya Ûzuri ikiwa hakuna Mtazamaji?

Au ndîo ûzuri Usio na Tija?

NI Sawa na Mtu aambiwe anaakili lakini Akili Zake hazitumii Wala kutumika,
Au Mtu awe na Pesa lakini hakuna watumiaji au hazitumiki .
 
Mabishano ndo wanaume hawapendi Ila sio smartness .

😆😆

Challenge ni muhimu sana.

Darasani Mwalimu Kilaza Hapendi mwanafunzi anayemchallenge, ni kawaida waalimu Wakali wengi kuwa na uwezo mdogo katika kufundisha na kujua contents

Mwanamke huwa mbishi akishagundua uwezo wako mdogo au akitilia Mashaka uwezo wako.

Lakini Wakati mwingine Mwanamke hubisha ili Kupima Uelewa wako kuhusu kile anachokubishia.
Wanawake most of them wàpo hivyo hasa wale Smart
 
😀😀

Sasa kizuri kikikosa Mtazamaji kitaendelea kuwa Kizuri? Yàani Ipi faîda ya Ûzuri ikiwa hakuna Mtazamaji?

Au ndîo ûzuri Usio na Tija?

NI Sawa na Mtu aambiwe anaakili lakini Akili Zake hazitumii Wala kutumika,
Au Mtu awe na Pesa lakini hakuna watumiaji au hazitumiki .
Umeona eeh raha ya uzuri watazamaji wawepo

Ila watz tunapenda kujiliwazia matatizo yetu kwa kutumia maisha ya wengine
 
Kuvumilia uhalifu NI kuwa mhalifu na kujifanyia uhalifu.

Uvumilivu unaotajwa ni uvumilivu wa Changamoto za Maisha zikiwemo uchumi, ugonjwa, na madhaifu Mengine àmbayo siô dhambi mfano Hasira, usahaulifu, upole, n.k.

Siô kuvumilia matusi, kipigo, umalaya, uchoyo, Usaliti, unyanyasaji n.k. huo haupo sehemu ya uvumilivu
Amina👊
 
Habari za Sabato Mkûu!

Ni Jambo la kawaida Kabisa kusikia Watu hasa Wanawake Wakitumia kauli za namna hii katika mazîngira tofautitofauti Kwa mfano wakichambana, kusutana au Wakati wakisikia unamsifia Mwanamke mwenzao àmbaye hajaolewa lakini amefikisha Umri WA kuolewa.

Mfano wa kauli hizô;
1. Ungekuwa mzuri Ungekuwa Mpaka Sasa hajaolewa.
2. Kwa ûzuri gàni alionao. Mbona kila Siku Wanaume wanamkimbia hata kuolewa haolewi.

Pia soma: Wanawake wengi wameolewa ila hawawapendi waume zao kutoka moyoni

3. Hana maajabu ndîo maana anaachwa. Kwa nje yupo hivyo lakini sivyo anavyoonekana ndàni.

Kwa nini Watu wengi zikiwemo za Waafrika, Asia, na kidôgo Ulaya wanamtazamo wa kuhusisha Mwanamke Kuolewa na ûzuri wake?
Huku wale ambao labda hawajapata Bahati au fursa ya kuolewa wakionekana wanatatizo, Kasoro Fulani àmbayo hata kama haionekani Basi wanaamini Ipo Ndani Kabisa?

Kûna ûzuri wa tàbia,
Uzuri WA maumbile,
Uzuri wa Nafasi na Roho,
Uzuri wa Akili

NI ûzuri upi àmbao Unamaanishwa kwamba mwanamke akiwa hajaolewa na anaumri na kuolewa hayuko nao?

Mbona wàpo weñye mwonekano usiovutia wameolewa huku ambao wanamuonekano mzuri wakiwa nje.
Wàpo weñye tàbia Njema hawajaolewa na wàpo tunaowajua waliokuwa wanauza mpaka miili Yao na wameolewa.

NI ûzuri upi unaomaanishwa?

Je nawe NI miongoni mwa Watu unayeamini Mwanamke asipoolewa anakasoro Fulani yàani Hana ûzuri fulani wa msingi?

Karibuni Kwa mjadala.
Uzuri tabia ni vile hawa wakina delila wanazani sisi tunangalia sura na shepu wakati wa kuoa
 
😆😆

Challenge ni muhimu sana.

Darasani Mwalimu Kilaza Hapendi mwanafunzi anayemchallenge, ni kawaida waalimu Wakali wengi kuwa na uwezo mdogo katika kufundisha na kujua contents

Mwanamke huwa mbishi akishagundua uwezo wako mdogo au akitilia Mashaka uwezo wako.

Lakini Wakati mwingine Mwanamke hubisha ili Kupima Uelewa wako kuhusu kile anachokubishia.
Wanawake most of them wàpo hivyo hasa wale Smart

Challenges muhimu ila usimchallange MTU Ila challenges mambo yake.

Sio unakaa unasema wanaume wafupi wabaya au wanawake wembamba wabaya hii itaonesha haupo smart.
 
Umeona eeh raha ya uzuri watazamaji wawepo

Ila watz tunapenda kujiliwazia matatizo yetu kwa kutumia maisha ya wengine

Labda awe miss world, au ûzuri wake unatumika kwèñye matangazo ya biashara, au air hostess, au tourhostess au receptionist katika maduka, hoteli au biashara, au video Vix sijui video queen.

Sasa hujaolewa, hufanyi biashara yoyote, ûzuri wako hautumiki popote unafikiri Hiko kichambo utakachopewa na Waja hakitakuwa na mantiki?

Uzuri lazima úwe na Tija.
Yani ukisikia kitu NI kizuri ujue kina mambo yafuatayo;
1. Kinafurahisha,
2. Kitamu
3.kina rahisisha mambo au Vitu na kina ufanisi.
 
Mimi kwa mtazamo wangu na kwa upembezi wa mambo nimejionea baadhi ya mambo.
1. Unaweza ukawa umevutiwa na Mwanamke ukahangaika mpaka ukapata mawasiliano yake mkaanza kuwasiliana vizuri mpaka kuanza kuitana majina yote mazuri lakini unakuta, Mwanamke anakuwa na mambo ya kuvunja moyo sana anaomba Vocha unamtumia bando la data na kifurushi hata kukupigia simu hapigi hata kukusalimia kwa ujumbe pia no ngumu nayo. Huwa inafadhaisha sana.

2. Anavaa anapendeza vizuri lakini kila siku anakwambia sijaoga na anataka ale chipsi 🤣🤣🤣

Mambo ni mengi sana kwahaya mawili tayari kwangu anakuwa ameshapoteza sifa ya kuwa Girlfriend kabisa.
 
Mwanamke WA aina hiyo anakuwa hajakupenda.
Wengi Kutumia Mbinu hizo kupunguza idadi ya waliofanya Application 😃
 
Back
Top Bottom