Ungekuwa wewe ungemshauri nini huyu dada?

Ungekuwa wewe ungemshauri nini huyu dada?

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Habari Kaka, mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa, mwkaa jana nilikorofishana na mume wangu, nilimfumania na dada wa kazi. KutoKana na kunidhalilisha nilichukua jukumu la kuondoka ili kumuacha, lakini alikuja kuomba msamaha nikamsamehe, lakini nilishindwa kusahau, nikiwa katika upweke huo nilijikuta naanzisha mahusiano na X wangu.

Mahusiano yaliendelea mpaka mwaka huu mwanzoni, mume wangu aligundua, nikamuambia kuwa nimemua kulipa kisasi kwakua nayeye alichepuka. Hicho kitu kilimuumiza sana mume wangu, akanifukuza na kusema kuwa hanitaki. Baada ya kuondoka kwa mume wangu nilibaki mwenyewe, nilienda kupangisha, X wangu hakuniacha, aliniambia kuwa nitafute pesa tufungue Biashara.

Nilikubali, nikatafuta pesa kwa kuchukua mkopo kazini tukafungua duka kubwa la spea, kwakua nilikua nakusoma nilisema kama tunafungua duka basi liwe duka la jina langu. Alikubali nikajua kuwa ananipenda, tulifungua duka, mimi nilichukua mkopo kazini, nikaweka milioni 15 na yeye akaweka milioni 15. Baada ya hapo kila kitu kilibaki jina langu, nikawa nasimamia mimi kila kitu.

Mke wake alijua na kuanza kunisumbua, mimi sikujali kwani kama ni ndoa ya kwangu ilishakufa. Tatizo Kaka lipo kwa huyu mwanaume, duka ni langu lakini sijui pesa zinaenda wapi? Yaani kitu kidogo anachukua pesa dukani, anasema kuwa atarudiasha lakini harudishi. Mwanzo nilimvumilia, lakini sasa hivi nimechoka, anajenga yeye na mke wake, wanakuja kuchukua vitu dukani kwetu ila kulipa inakua ngumu. Yaani duka la milioni 30 sasa hivi vitu vilivyobaki hata milioni 10 havifiki na zote kala yeye.

Nikikasirika ananiambia kuwa ataniacha, kaka nampenda, mume wangu ameshaniacha anaishi na mwanamke mwingine, nina watoto wawili naishi nao, mume wangu hahudumii watoto kwa chochote, nimehangaika ustawi wa jamii mpaka nimechoka, huyu mwanaume naye hahundumii watoto wangu, nina mimba yake ananiambia nikizaa wakwake ndiyo atahudumia, nimechaganyikiwa sana Kaka, naomba msaada wako, sitaki kumpoteza mimi nitakua mtu wa kuachwa mpaka lini?

Ingekuwa wewe ungemshauri nini mtu kama huyu?
 
Habari Kaka, mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa, mwkaa jana nilikorofishana na mume wangu, nilimfumania na dada wa kazi. KutoKana na kunidhalilisha nilichukua jukumu la kuondoka ili kumuacha, lakini alikuja kuomba msamaha nikamsamehe, lakini nilishindwa kusahau, nikiwa katika upweke huo nilijikuta naanzisha mahusiano na X wangu.

Mahusiano yaliendelea mpaka mwaka huu mwanzoni, mume wangu aligundua, nikamuambia kuwa nimemua kulipa kisasi kwakua nayeye alichepuka. Hicho kitu kilimuumiza sana mume wangu, akanifukuza na kusema kuwa hanitaki. Baada ya kuondoka kwa mume wangu nilibaki mwenyewe, nilienda
Ujinga ni wako na hiyo ni adhabu unatumikia we uliona wapi dhambi ya mtu ikalipwa kwa dhambi yani umeshindwa kutambua mwanaume ni mwanaume tu hata baba yako Hana mama yako mzazi pekee
 
Huyo aendelee kumpenda tu huyo X ,aachane na mambo ya duka yatamuharibia ,maana upendo utalisha familia yake na utarudisha hizo pesa zinazochukuliwa bila mpangilio hapo dukani.

Subiri duka liishe ili akili ikukae sawa
 
Tatizo la huyo dada ni pale aliposema mke wa X wake anasumbua ila yeye anakaza kwakua ndoa yake imekufa,kwaio alitaka na ya mwenzie ife,yani anafungua duka na mume wa mtu confortable kabisa,laana inakutafuna dada,omba Mungu akusamehe kwa kutaka kuvunja ndoa ya mwenzio.
 
Back
Top Bottom