Ungekuwa wewe ungemshauri nini huyu dada?

Ungekuwa wewe ungemshauri nini huyu dada?

Mwambie arudi akaombe msamaha kwa mume wake aseme uchafu wake wote hadharani kama alivokusimulia wewe, huenda akasemehewa.
 
Habari Kaka, mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa, mwkaa jana nilikorofishana na mume wangu, nilimfumania na dada wa kazi. KutoKana na kunidhalilisha nilichukua jukumu la kuondoka ili kumuacha, lakini alikuja kuomba msamaha nikamsamehe, lakini nilishindwa kusahau, nikiwa katika upweke huo nilijikuta naanzisha mahusiano na X wangu.
"ukionja au kunywa sumu mwenyewe usitegemee afe mtu mwingine".
"Haraka haraka haina baraka"

Mwisho wa kunukuu...
Huyu alitaka kumkomoa jamaa bila kujua kuwa anajikomoa mwenyewe. Kila kitu kina faida na hasara. So, alipoamua kulipiza kisasi tena waziwazi alijua faida na hasara atakazozipata. So, Hana budi kuvumilia anayapitia hadi mwisho.

Mwisho: "Huwezi kupata jema kwa malipo ya kumfanyia mtu mwingine ubaya"...
 
Heh huu mseto si mdogo sasa hapo ni kwamba umelikoroga vibaya mno...huyo mwanaume ulocheat nae mpaka akavunja ndoa yako na ww mnaendana na kufanana mlipaswa kuwa pamoja.Namuonea huruma huyo mke wake(ex wako)!Hivi nafsi haikusuti unayomfanyia mwanamke mwenzio?Machozi yake yatakucost sana.Unataka kusambaratisha familia yake kwasababu ya kwako umeshaivuruga?yaani ww utapata shida dada!

Hilo duka kwa nilivyoelewa litafilisika,huyo mwanaume atakuacha na watoto wako aende kwa mkewe ubaki unahangaika na dunia peke yako!Ulifanya makosa sana kuendeleza mahusiano na ex wako angali umempa matumaini mumeo kama umemsamehe!
 
Habari Kaka, mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa, mwkaa jana nilikorofishana na mume wangu, nilimfumania na dada wa kazi. KutoKana na kunidhalilisha nilichukua jukumu la kuondoka ili kumuacha, lakini alikuja kuomba msamaha nikamsamehe, lakini nilishindwa kusahau, nikiwa katika upweke huo nilijikuta naanzisha mahusiano na X wangu.
We ni mpuuzi tu 😅 sasa umeacha ndoa yako umekimbilia kwa X ambaye pia ameoa tayari ana mkewe? Hivi wanawake ujinga huu mtaachaga lini aisee
 
Tatizo la huyo dada ni pale aliposema mke wa X wake anasumbua ila yeye anakaza kwakua ndoa yake imekufa,kwaio alitaka na ya mwenzie ife,yani anafungua duka na mume wa mtu confortable kabisa,laana inakutafuna dada,omba Mungu akusamehe kwa kutaka kuvunja ndoa ya mwenzio.
Yani kavunja nyumba yake mwenyewe kwa kiburi kisha anataka avunje na ya X wake pia
 
tucheke kidogo jmn...hahaa yaani mtu kamkimbia mume kwa kuchepuka alafu kaenda kuwa mchepuko wa mme wa mtu.....wanawake akili zenu zipo matakoni
Nasindikia na wimbo mmoja hivi wa zamani..
homa imenizidia mi eyooo kutwa nashinda nalia jua linapochomoza machozi huwa yanitoka
... nimeachana na mume wangu nimekwenda kwa rehani badaa muda si mrefi anasema niondoke sina tabia nzuri
 
Kwa kuwa duka ni kwa jina la mwanamke awe na msimamo"hakuna kuchukua kitu bila idhini yake" akija juu basi mgawane, utakuwa unalisha mwanamke mwenzio. Nimemaliza umbea wangu!
 
Habari Kaka, mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa, mwkaa jana nilikorofishana na mume wangu, nilimfumania na dada wa kazi. KutoKana na kunidhalilisha nilichukua jukumu la kuondoka ili kumuacha, lakini alikuja kuomba msamaha nikamsamehe, lakini nilishindwa kusahau, nikiwa katika upweke huo nilijikuta naanzisha mahusiano na X wangu.

Mahusiano yaliendelea mpaka mwaka huu mwanzoni, mume wangu aligundua, nikamuambia kuwa nimemua kulipa kisasi kwakua nayeye alichepuka. Hicho kitu kilimuumiza sana mume wangu, akanifukuza na kusema kuwa hanitaki. Baada ya kuondoka kwa mume wangu nilibaki mwenyewe, nilienda kupangisha, X wangu hakuniacha, aliniambia kuwa nitafute pesa tufungue Biashara.

Nilikubali, nikatafuta pesa kwa kuchukua mkopo kazini tukafungua duka kubwa la spea, kwakua nilikua nakusoma nilisema kama tunafungua duka basi liwe duka la jina langu. Alikubali nikajua kuwa ananipenda, tulifungua duka, mimi nilichukua mkopo kazini, nikaweka milioni 15 na yeye akaweka milioni 15. Baada ya hapo kila kitu kilibaki jina langu, nikawa nasimamia mimi kila kitu.

Mke wake alijua na kuanza kunisumbua, mimi sikujali kwani kama ni ndoa ya kwangu ilishakufa. Tatizo Kaka lipo kwa huyu mwanaume, duka ni langu lakini sijui pesa zinaenda wapi? Yaani kitu kidogo anachukua pesa dukani, anasema kuwa atarudiasha lakini harudishi. Mwanzo nilimvumilia, lakini sasa hivi nimechoka, anajenga yeye na mke wake, wanakuja kuchukua vitu dukani kwetu ila kulipa inakua ngumu. Yaani duka la milioni 30 sasa hivi vitu vilivyobaki hata milioni 10 havifiki na zote kala yeye.

Nikikasirika ananiambia kuwa ataniacha, kaka nampenda, mume wangu ameshaniacha anaishi na mwanamke mwingine, nina watoto wawili naishi nao, mume wangu hahudumii watoto kwa chochote, nimehangaika ustawi wa jamii mpaka nimechoka, huyu mwanaume naye hahundumii watoto wangu, nina mimba yake ananiambia nikizaa wakwake ndiyo atahudumia, nimechaganyikiwa sana Kaka, naomba msaada wako, sitaki kumpoteza mimi nitakua mtu wa kuachwa mpaka lini?

Ingekuwa wewe ungemshauri nini mtu kama huyu?
Mumeo amesha oa yuko na mke, x ,wako ane yuko na mke, wewe ndio upo katikati kwa nini usitafute mwanaume mwingine ili mfanane??!!
 
Mwanamke simsikitikii kabisa yani hata kidogo kinachoniumiza roho mimi ni hao watoto,hakuna kitu sipendi kama mimi nakula vizuri halafu watoto sijui wamekula hawajakula wameshiba au hawajashiba!mwanaume usimpe mwanamke wanao akulelee tafuta option ujue watoto wako usalama wao uko vipi maana mwisho wa siku ndo wamebeba asili yako mwanamke hana hasara hata wakiharibika.

Inaonekana huyu mwanamama ni mchepukaji mzoefu kiasi jamaa kila akiwaangalia watoto haioni sura yake kwao ila anaiona sura ya X wa mwanamke akaona mapema arudishe mpira kwa kipa ila ningepata wasaa wa kumshauri jamaa ningemwambia awapime watoto DNA kama wake aimarishe kizazi chake shule nzuri etc huyo malaya amuache akafie mbali.
 
Back
Top Bottom