Ungepata nafasi ya kufanya kazi Serikalini, ungependa kufanya kitengo gani? Na kwanini?

Ungepata nafasi ya kufanya kazi Serikalini, ungependa kufanya kitengo gani? Na kwanini?

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
Ungepata nafasi ya kufanya kazi Serikalini ,ungependa kufanya kitengo gani?

Na kwanini!

Majibu yako, yatazingatiwa
 
Ugavi. Mambo ya manunuzi, unafanya deal na wazabuni. CAG akija anatoa tu report fedha imetumika au kuna deni na wanaodaiwa hawajulikani.

Sio ualimu hata chaki huwezi kuuza. Mafundi nguo wanatumia mkaa.
 
Ningependa nifanye kazi wizara ya fedha na mipango akiamungu wallahi pesa zingeadimika isingeliwa hata sent tano kizembe zembe Na mwigulu ningemfanyia makusudi mshahara wake ningekua nafanya mipango na watu wa hazina uwege unachelewa chelewa
 
Hivi wale waliokataa uteuzi wamebadilishiwa kazi au Fire on Fire
 
Ningepeda kuwa idara ya usalama wa taifa.
Ni kushughulika na hawa wezi, hakuna wa kuiba mali zetu.
 
Kitengo chenye mamlaka ya kulifanya bunge navyotaka. ***** ningemhonga mtu bunge zima na wabunge wenu wangejenga jingine
 
Waziri wa Fedha na Mipango. 😇

Kila mwaka ningekuwa naingiza nchini Yutong zisizopungua 60, ninakuwa na majumba yangu lukuki ya kifahari, magari ya kifahari, vituo vya mafuta, timu ya mpira wa miguu, vimada, na machawa wangu nchi nzima.

Dah! Ngoja niwahi kulala ili kesho niwahi sokoni kuuza nyanya chungu zangu.
 
Waziri wa Fedha na Mipango. Kila mwaka naingiza zangu Yutong 60, ninakuwa na majumba yangu lukuki ya kifahari, magari ya kifahari, vituo vya mafuta, timu ya mpira wa miguu, vimada, na machawa wangu nchi nzima.
Hahaha..
Ungemuiga kabisa wa sasa!
 
Manunuzi,kitu cha million 100 ninaandika million 250 hahahhahh.Ndo wanavyofanya.Unafungwa baadae unatoka uanpewa adhabu ya kufagia sehemu za umma.Huku uliiba umewekeza mali za kula mpaka vitukuu wa vitukuu wako.Kama unabisha muulize Daniel Yonah.aliiba na sasa anaenjoy na vizazi.vyake vitaenjoy.
 
Ugavi .
Mambo ya manunuzi, unafanya deal na wazabuni. CAG akija anatoa tu report fedha imetumika au kuna deni na wanaodaiwa hawajulikani.
Sio ualimu hata chaki huwezi kuuza. Mafundi nguo wanatumia mkaa
Nimecheka mafundi hawatumii chaki ili uwauzie😀
 
Back
Top Bottom