Pre GE2025 Ungependa zoezi la Upigaji Kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 lifanyikaje?

Pre GE2025 Ungependa zoezi la Upigaji Kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 lifanyikaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Unatamani Zoezi la Upigaji Kura mwakani 2025 liweje?

  • a) Tupige Kura kupitia Mfumo wa Kidigitali

  • b) Tupige kura kwa njia tuliyoizoea ya karatasi na box

  • c) Njia nyingine; itaje


Results are only viewable after voting.

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

kura.jpg

Mwaka huu 2024 tutafanya uchaguzi wa serikali za mtaa na mwakani 2025 tutafanya uchaguzi Mkuu ambapo tutachagua Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.

Kwa kuzingatia chaguzi za nyuma mpaka kufikia leo ungependa zoezi la uchaguzi lifanyikaje ili kuongeza uwajibikaji, utawala bora pamoja na demokrasia?

Wagombea waweje? Wawe na sifa gani? Kampeni zifanyikaje? Mchakato wa Kupiga Kura ufanyikaje? Usimamizi wa zoezi la upigaji kura ufanywe na nani? Ili viongozi tunaowapata wawe wawajibikaji na wenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi?
 
Uchaguzi usitishwe hadi tufanye makubaliano kwanza namna bora ya kuendesha nchi. Tuandike katiba mpya kwanza itakayotambua uwepo wa Tanganyika, Katiba itakayoweka bayana na kukiri kuwa ardhi ni mali ya wananchi wa Tanganyika na sio Serikali wala Rais.
Utawala uliopo uendelee lakini uanzishe pia mchakato wa kura ya turufu kuamua uwepo wa muungano kama unakubalika na katika muundo upi. Katiba mpya ikiwepo ndio ipangwe siku ya uchaguzi wa viongozi watakaozingatia matakwa ya wananchi.
 
Kila mgombea wafuasi wake wajipange nyuma yake. (means kuwe na mwakilishi wake kila kituo ambaye atasimama mbele wanaomuunga mkono wajipange nyuma yake. Hakuna wizi hapo
 
Inajulikana kuwa kwa upande wa Urais uchaguzi umeshaisha. Ni Mama Samia hadi 2030. Kilichobaki tuwachague viongozi wa ngazi za chini wenye sifa kuanzia ubunge bila kujali vyama. Kwenye ubunge na udiwani sio vibaya kuchagua hata mpinzani mwenye kupenda maendeleo. Bunge la sasa limejaa vilaza wa kutisha.
 
Inatakiwa ziwekwe picha za wagombea, kila moja na ubao wake. Na wafuasi wao waelekee kwenye picha husika. Kisha kura zihesabiwe na ziandikwe chini ya picha ya mhusika.
Kwa nchi hii ni Bora kuhesabu kizamani kuliko kwenye box zao.
 
Back
Top Bottom