Unguja: Mke achoma moto gari ya mumewe baada ya kuoa mke wa 2

Sisi ukijidai kuzaa na mwanaume wa mtu imekula kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi siyo kwamba lazima mke wa kwanza aridhie kwanza ndipo mme unaongeza mke wa pili? Na kama ndivyo iweje jamaa aongeze mke bila kupata ridhaa ya mke mkubwa?
Sio lazimu kuridhia na wala haina hata ulazima wa kumpa taarifa mke wa kwanza. Unaweza kuoa tu, kukataa mke mkubwa kuolewa uke wenza ni kuiharifu Quran.... Allah kaelekeza oeni wawili na kuendelea, ukishindwa oa mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujitahidi kuwa na option mbili tunapokumbana na hali zisizotupendeza, kama haupo tayari kuwa uke wenza ni bora kuondoka kimoja, ukae kungoja mtalikianae kwa amani, mambo ya kuchoma nyumba kudhuru, ama kuua ni ujinga.

Mwanaume kama mwanamke hakufai na unaona huwezi endana na tabia zake achana nae, sio lazima umshindilie magunia ya mkaa au umpige mithili ya kibaka alienaswa kariakoo ni ujinga. Maana mwisho wa siku utajutia tu hata kama ni wewe ulianza kukosewa.
 
Daah hapo bas wanawake wanaonewa. Sema kwa vile ndo sheria za dini inabd ziheshimiwe tu hamna namna

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu hawwonewi.

Kama ni hivyo watatokea wanaume watadai uislamu umewaonea kwa sababu kwenye ndoa mnaishi wote lakini uislamu umetaka maharai atoe mwanaume.

Na uislamu ukataka mume ndo awe na jukumu la kulea familia na kuhudumia mke kwa kila kitu hata kama mwanamke anao huo uwezo wa kujilisha lakini mume ndo jukumu lake.

Kwa hili nalo wanaume ilikuwa walalamike ila haiwezekani kwa sababu dini ya uislamu ni ya uadilifu na sio usawa.yani inaweka mambo kwa hekima sana pengine hapa mwanamke akapewa kipaumbele na kule akapewa mwanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo gari ya mumewe ni gari yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…