Unguja: Mke achoma moto gari ya mumewe baada ya kuoa mke wa 2

Unguja: Mke achoma moto gari ya mumewe baada ya kuoa mke wa 2

Afadhali kaongeza Mke wa pili kuliko kuzini, maana wanaume walio wengi wana vimada nje ya ndoa Na wake zao wanadhani wapo peke yao, bora kuoa ikawa wazi kiliko kuchepuka.
Hongera sana Bwana Hajji.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja limeanza kufanya uchunguzi zaidi kuhusu tukio la Msimu Jaffari (33), kudaiwa kuchoma moto gari ya mumewe, ambaye wiki iliyopita alitoa taarifa ya kuongeza mke wa pili katika ndoa yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Suleiman Hassan alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Kesi hiyo imeripotiwa katika Kituo cha Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Kamanda Hassan alisema tukio hilo, limeripotiwa mwishoni mwa wiki huko Kitumba Wilaya ya Kati Unguja. Gari aina ya Spacio inayomilikiwa na Abdallah Hijji (43) ilitiwa moto usiku.

Mke wa kwanza wa mtu huyo, anatuhumiwa kufanya tukio hilo. Alisema taarifa za awali katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi, unaonesha kwamba Hijji alitoa taarifa kwa familia na mkewe wake wa kwanza, kwamba anakusudia kuongeza mke wa pili.

‘’Uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika hatua za awali unaonesha kwamba tukio hili linahusishwa na wivu wa kimapenzi, ambapo mume alimjulisha mkewe nia ya kuoa mke wa pili na kama unavyojua wanawake wengi hawapendi ukewenza. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na ukweli halisi wa tukio hilo,’’ alisema.

Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, kwa kuwahoji watu mbalimbali huko Kitumba, umeonesha kwamba Hijji aliongeza mke wa pili wiki iliyopita. Hatua hiyo ilimtia hasira mke wa kwanza, ambaye kabla ya ndoa hiyo alikuwa akitoa tahadhari kwa mumewe, kwamba asithubutu kuoa mke mwingine.

‘’Huyu mwanamke hataki ukewenza, kwa muda mrefu amekuwa akimuonya mumewe asijaribu kufanya kitu hicho na akifanya atajuta,’’alisema jirani ya Hijji, Haji Omar ambaye alidai amekuwa akishuhudia mara kwa mara ugomvi wa watu hao.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi utakapomalizika, jalada la kesi hiyo litapelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Chanzo: HabariLeo
MKE ana hekimaa sana nampa U DK MPKA SAA MBILI KESHO ASBH WANAUMEE MKOME VIBOROSHUTAAA PAMBAVUI
 
Hakuna cha bora hapo huyo kafanya kosa kubwa kukubali kuolewa na muislam wakati yeye taratibu za dini hazitaki si ukafiri huo ,kiislam kuongeza mke ni utaratibu wa kawaida angedai taraka kuliko kuanza kuharibu mali za mumewe
Bora alivyochoma gari..maana mwingine angechoma hata huyo mke mwenzie.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria za dini ya Islam zinataka muumin uwe na subra na usiwe na moyo na hisia za kibinadamu. Allah awajalie wepesi hawa waumini wake
 
Sasa huoni anaechepuka anakuwa na wanawake wengi zaidi ya huyu alieongeza? Halafu uwezekano wa mchepukaji kuleta maradhi ni mkubwa kuliko alieo

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakwambia hata mwanaume awe na wake watano panamzuia kuchepuka ni nini?
Kwanza ukiona anaanza kuongeza mke wa pili jua huyo ana tamaa. Akioa wakifika wa nne unadhani hataendelea kutamani? Na akitamani huku sheria imemlimit unafikiria nini? Atachepuka tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mwanamme anaetosheka na mwanamke mmoja, ndio maumbile ya wanaume, labda huyo mwanamme awe na mapungufu, na ili kudhibiti suala la mwanamme kuwa na wanawake wengi ndio mana wao wakaekewa sheria yaani ruhusa hadi ya kuoa wake 4. Jamii yote ya wanyama huo ndio mfumo wao.
Nani kakwambia hata mwanaume awe na wake watano panamzuia kuchepuka ni nini?
Kwanza ukiona anaanza kuongeza mke wa pili jua huyo ana tamaa. Akioa wakifika wa nne unadhani hataendelea kutamani? Na akitamani huku sheria imemlimit unafikiria nini? Atachepuka tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom