Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Zaidi ya watoto milioni 10 ni miongoni mwa wale wanaokabiliwa na ukame mkali katika Pembe ya Afrika.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef, linakadiria kuwa idadi hii ni milioni tatu zaidi ya ilivyokuwa miezi miwili iliyopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unicef Catherine Russell amesema kuwa ukame ni "dharura mbaya zaidi iliyosababishwa na hali ya hewa katika kipindi cha miaka 40". Na kama msaada wa haraka hautafikishwa au mvua kunyesha watu wanaweza kupoteza maisha
Ameeleza kuwa Unicef inahitaji takriban $250m (£199m) kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa Ethiopia, Somalia, Kenya, Eritrea na Djibouti.
Chanzo: BBC