University of Dar es salaam: Mnavyowafanyia wanafunzi wa masters na PhD mnakiua chuo, badilikeni

Nilishajiapiza siwezi kusoma masters wala phd hapa tz.
Tatizo vijana wanadhan Masters/PhD utasoma Kama undergraduate. Wengi uwezo Mdogo Kama kuandika tu thread tu hapa ishu itakua dissertation/thesis? Eti akaenda academic block kuulizia?
 
Mtu anakuzungusha masters ya miaka 2 unaisoma miaka 6 kwa nini usimshshe futi sita tu..hao maprofesa wengi wametoka kwenye familia masikini sana...kwa hiyo hawataki watu wenye shahada 2 au tatu wawe wengi wakihisi thamani yao itapungua mtaani.
 
Mbona wenzao kule UDBS kwamaana ya Shule ya Biashara hawana kona kona wakati ni chuo hicho hicho kimoja?
Ila Lecturers wa UDSM Mungu anawaona
 
Tatizo hamjamuelewa lala miko lake...
Base kwenye content... You know character is fun huh?
Waliosoma fasihi na literature tutaelewana hapa.

Anyway ujumbe umefika ni wakati watanzania tunatakiwa tubadirike inakera kwKwerli.
 

Mwanafunzi wa level ya Masters anaweza kujisimamia mwenyewe. Mzazi pamoja na mapenzi yote kwa mtoto wako, ifike mahali umuache apambane mwenyewe. Unaweza ukafuatilia ukiwa nyumbani lakini kwenda front kama hivyo kunaleta mashaka juu ya uwezo wa mtoto wako kujisimamia na hata kazini kwa mwenendo huu hataaminika.

Otherwise poleni kwa changamoto.
 
Binafsi pia ni mhitimu wa UDSM. Ila niliapa! Sitakuja nirudi tena kwenye kile chuo kusoma kozi ya aina yoyote ile, kutokana na mazingira magumu niliyopitia kwa miaka yangu yote mitatu pale chuoni.

Baadhi ya wakufunzi walikuwa ni wakuda sana kiasi cha kukaribia kuwa wachawi! Halafu wadau wengine unakuta wanapiga tu ma GPA ya 4......!
 
Yaani Masters unaenda Chuo na mama yako kuongea na Waalimu? Kama mimi ni Lecturer hakika sikusikilizi……I’m sorry to say this lakini huyo kijana wako huenda ni tatizo na kama ndio hivyo tunazalisha wasomi wa ajabu sana, huyo akipata hata shida kazini atamuita mama yake, mwambie mimi nimelipa ada nataka nione cheti, hizo stories za masupervisors pambana nazo mwenyewe akishindwa basi hata hiyo Masters haimfai.
 
BA Archaeology kwa nn usipate GPA ya 5?
 
Ndugai alisomaga UDSM?
Vipanga wengi miaka ya nyuma walisoma udsm! Maana wahitimu walikuwa ni wachache na hakukuwepo na vyuo vya kata kama ilivyo sasa. Hivyo usimchukulie poa Spika wako! Alikuwa naye ni mmoja wa vipanga wa nchi hii!

Ni bahati mbaya tu ukiingia ccm, akili zote zinahama kutoka kichwani na kukimbilia tumboni.
 
Ukitaka kusoma kwa kurelax Masters nenda Udbs Kyle kama unaqualify na courses za kule..........ila huku kwingine kama department ya Political science na Sociology labda uwe unaongea Kihaya utafanikiwa fasts........
 
Umeongea pumba
 
Ipo tofauti kubwa ya uelewa kuhusu makuzi na maana ya familia; kama mwanao atakosa future Kwa sababu ya urasimu ukadhani kumwacha aangamie nikumkomaza fine. Lakini pia inategemea unasoma masters ukiwa na umri gani?Kusoma ni jambo Moja nakukwamishwa na wenye taasisi ni jambo jingine.

Umewahi kujiuliza kwanini familia za wanasiasa Tanzania zinazidi kukabidhiana Madaraka? Unadhani Ridhiwan ana qualities kuliko wengine nchini kuwa Naibu Waziri? Ni Kwa sababu mzazi wake yupo nyuma yake; family it's like project, ukiruhusu Mradi wako uharibiwe na watu flan unaharibu the all project.

Karne hii Sijui MTU anaitwa examination au external anakaa na kazi ya mwanafunzi miezi mitatu hadi sita no comment tuseme mtoto afuatilie Mwenyewe? Nchi imejaa watu wenye Phd kibao wakusahihisha izo kazi kwanini umpe MTU asiyekuwa na muda wakusahihisha? Then akipewa inakuwa Siri mwanafunzi apaswi kujua Wala kuhoji , haya mambo hakuna Tena kwenye mifumo hata ya kindergarten, masters page 80 unatumia 90dys kuzisoma? You have softwares zakukusaidia kufanya analysis na kuangalia plagiarism unaagua Nini Siku tosini?

Ni fedhea kuona tunatetea watu wasiotaka kutimiza Wajibu wao. Udsm ilipaswa kufanya kazi Kwa standard ya ulimwengu wa kwanza ambapo 18 months sharp mwanafunzi amemaliza chuo.

Mtoto anasoma mwaka na nusu then anakuambia nimemaliza course work ndo tunaanza kuandika proposal............let us accept reforms maisha yamerahisishwa.

Leo Duniani Kuna watu wamespecilize kuandika research, you just collect data and submit to them. Wewe kazi Yako nikuangalia utafiti wako umeandikwa kama ulivyoona field? Mabadiliko kwenye elimu muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…