Ng'wale
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 4,690
- 3,399
Ng'wale
Na wewe ni kamchezo kako nini au familia yako wanako hako kamchezo mbona unatoka povu kwa mtu kuambiwa muuaji,ndege wa rangi moja huruka pamoja na wewe pia ni family ya hako kamchezo ka kuua na kiruka na ungo
Unashangaa msomi kuwa mchawi mbona wewe ni mmoja wao na wapo wengi walikabidhiwa mikoba pamoja na kwamba wameenda shule sasa povu la nini jombaa?
Au Ndugai ni mjombako hivyo unamtetea huenda akakupa ufagizi bungeni? Polocy yenu anayetoa matusi anapata kazi endelea bro
Sina namna ambayo naweza kukubadilisha mtazamo wako, najua tunatofautiana kimtazamo. Hakuna mtu ambaye anaweza kuunga mkono muuaji, lakini kitu kinachogomba hapo ni imani iliyopo kwa baadhi ya watu kwamba hapo kuna connection ya uchawi. Ningeendelea kufikirisha kichwa changu kama tungeambiwa dereva wa Lorry hilo alipewa maagizo ya kusababisha ajali hiyo, lakini siwezi kuungana na wale wanaoliweka ktk imani ya kichawi.
Kwamba mtu anayepingana na imani yako ya kuamini katika uchawi basi naye ni mchawi, huo ni mtizamo wako ambao pia siwezi kuubadili. Ni sawa na ilivyo imani katika Mungu, wapo wanaoamini kuwa Mungu yupo na wapo wasioamini kuwa yupo. Ni vema ukaachwa uendelee katika imani yako na wale wasioamini hayo wakaendelea pia.