Uchaguzi 2020 Ununuzi wa ndege na ujenzi wa Chato Airport ni kashfa inayomtesa Magufuli?

Kabla sijajibu kwa Uelewa wangu nami naomba Kwanza nikuulize je, Ndege hazina Tija Kiuchumi? Je, Rais Kujenga Uwanja wa Ndege Kwao Kosa?
Ndege zina faida kiuchumi ila hapo hoja ni serikali kuingia kwenye biashara moja kwa moja kwa kununua ndege tena cash, mf baada ya kuingia corona ndege hazijafanya kazi so hapa ni hasara kwa wananchi ndo maana biashara kama hizi zinafanywa na mashirika private like fastjet
 
Issue ni kwamba Magufuli kachoka mnooo....hata sura imeporomoka Sana, haina nuru.... something is not normal internally.
Unashangaa nini kumuona Magufuli kachoka hujui kwamba Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja?

Kwanza anaendesha nchi kama rais pia anafanya kampeni.

Usimlinganishe na Lissu ambaye kazi yake kubwa ni kupayuka tu.
 
Nasikia wanataka kuchukua kibondo na chato uwe mkoa mpya.
Nadhani hili lina ukweli asilimia 90, wakati wa sabasaba kwenye banda la TBA kulikuwa na ramani na majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa sehemu mbalimbali za nchi.

Mojawapo ni jengo la hospitali ya rufaa mkoa wa Chato, nilimuuliza mara mbili binti aliyekuwa anatoa maelezo kwa wageni, hakuwa na jibu zaidi ya kuniangalia tu.
 
Unashangaa nini kumuona Magufuli kachoka hujui kwamba Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja?

Kwanza anaendesha nchi kama rais pia anafanya kampeni.

Usimlinganishe na Lissu ambaye kazi yake kubwa ni kupayuka tu.
Kwani Magufuli ndio wa kwanza kuongoza nchi na kupiga kampeni kwa wakati mmoja?
Acheni kujitoa ufahamu, mdau kachoka....halafu sauti yake imekuwa ya kukoroma sana au mmedunga steroids?
 
Comrade tunapowaambia chama chetu ccm kimejipanga muwe mnatuelewa.

Iyo ni survey kutaka kujua idadi ya wanachama ambao wana kadi ya mpiga kura.
Kimejipanga kwa wizi wa kura majambazi wakubwa safari hii haibiwi mtu
 
Ni maamuzi ya hovyo kabisa, maana bajeti yake haikupita bungeni
 
Kimejipanga kwa wizi wa kura majambazi wakubwa safari hii haibiwi mtu
2015 mlituhakikishia kuwa yule mtalaamu wa kuiba kura lowassa amekuja nae chadema. Baada ya hapo hamjawahi kutuambia kama aliondoka na lowassa au bado mpo nae.
 
Comrade tangu lini keyboard ikawa jambia??
Hii yote ni kwanini?
Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Ndio maana sasa maccm wakiongozwa na Meko wanafoka jukwaani. Wananchi wanataka maji unanunua ndege, wao wanataka hospitali unajenga flaiova, wao wanataka shule unajenga SGR fupi.

Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Maccm badilikeni
 
Comrade msipende kupinga pinga tu kila kitu, umeme kaulize matokeo ya REA, hospital na vituo vya afya zimejengwa nchi nzima. Sijui kwanini mnajitoa sana ufahamu?

Mfugale flyover imepunguza tatizo la foleni pale tazara kwa kiasi kikubwa sana. Comrade unaishi wapi wewe mpaka uponde ujenzi wa flyover?
 
Umeona wapi hakuna maji? Umeona wapi hakuna hospital?
 
Akichukizwa zaidi arudishe pesa zetu,asitufokee wakati katupiga yeye na doto
 
Hizo ndege soon atazikabidhi jeshini na atasema marufuku kuzijadili Mali za Jeshi
 
Mkuu Urais si mhimili wa kukosea ukajirekebisha, ukikosea unawajibika au unawajibushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…