Magufuli kafanya mambo mengi mazuri na pia ni binadamu ana mapungufu. Katika mambo anayopaswa kuyasahisha kama ataendelea awamu ya pili ya miaka mitano..
1. Kurudisha uhuru wa Bunge na Mahakama
2. Kupunguza na kupitia upya sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari
3. Kurudisha imani ya wananchi kwenye vyombo vinavyosimamia chaguzi yaani NEC na ZEC
4. Kuzuia / kutokomeza matumizi ya watu wasiojulikana...
5. Kulegeza suala zima sheria za mifuko ya hifadhi ya kijamii (MAFAO)
6. Kupitia upya makato ya makopo ya Elimu ya juu (retention fees).
7. Bunge live
Hayo mambo sita naimani kabisa yangekuwa hata ndani ya Ilani ya CCM, tungeongea mengine kwenye uchaguzi huu.
"maendeleo hayana chama"