Unyakuo u karibu, nimemwona King Jesus mawinguni amepanda farasi mweupe akiwa na jeshi kubwa la Malaika na Watakatifu

Unyakuo u karibu, nimemwona King Jesus mawinguni amepanda farasi mweupe akiwa na jeshi kubwa la Malaika na Watakatifu

anajifichaficha tu na panga lake, Netanyahu tunamuona kila siku BBC & Aljazeera akiwa na makombora km yote.
 
Neno la Mungu linasema wazi, Unyakuo utatokea maisha yakaendelea kama kawaida,

Wawili watakuwa shambani wakilima, mmoja atatwaliwa mwingine ataachwa,

Wawili watakuwa wamelala kitandani, mmoja akitwaliwa, mwingine akiachwa.

Nami ni mtumishi wa Mungu, nikitwaliwa nikiwa nafanya KAZI ya Mungu pia ni jambo jema.


Karibu katika familia ya WATAKATIFU waishio duniani🙏


Huo Ujumbe ulikuwa Kwa watu gani?
 
Salaam,Shalom!!

Nalikuwa katika Roho, usiku, ndani ya nyumba, ghafula nikapata uwezo wa kuona nje mawinguni,

Naliona jeshi kubwa la Malaika na WATAKATIFU wakiongozwa na jemedari mkuu, Yesu Kristo, amevaa taji yenye kungaa sana kichwani mwake, mikononi alishika upanga ungaao sana, alipita mawinguni amepanda farasi mweupe, na farasi huyo alipita akikanyaga mawingu kama farasi apitapo Nchi kavu,Majeshi ya Malaika yalifuatana naye wakiwa pia wamepanda juu ya farasi weupe Kila Mmoja, na baada ya Mfalme Yesu kupita akiambatana na Majeshi ya Mbinguni, aligeuka na kunitizama huku usoni mwake akiwa ametabasamu.

Nilijaribu kutaka kuwaonyesha Walio karibu yangu Ili waangalie juu na kuona kinachotokea lakini sikuona aliyebahatika kuona nilichoona, nilitamani kumfuata huko aliko mawinguni Ili kufurahi na kuambatana naye lakini baada ya kunitizama, akageuka na kuendelea na msafara wa Majeshi ya Malaika na WATAKATIFU wake.

.......Mwisho wa taarifa......

Source: Niliyoyaona na kuyaandika, yapo katika vifungu hivi ndani ya BIBLIA.

(Waraka wa Yuda 1:14)
Na Henoko, mtu wa Saba baada ya Adamu, aliutoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, angalia Bwana alikuja pamoja na WATAKATIFU wake, maelfu elfu. Ili afanye HUKUMU juu ya watu wote.

Ufunuo wa Yohana 14:1-5,

1: Kisha nikaona na tazama huyo mwana kondoo, amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye Jina lake na Jina la baba yake limeandikwa katika VIPAJI vya NYUSO ZAO.

Ufunuo wa Yohana 19:11-16.

11: Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi weupe, na Yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa- Kweli, naye Kwa HAKI ahukumu na kufanya vita.

12:Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya KICHWA chake, vilemba vingi, naye ana Jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila Yeye mwenyewe.

13: Naye amevikwa vazi lililochovywa katika Damu, na Jina lake aitwa NENO la Mungu.

14: Na Majeshi yaliyo Mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15: Na upanga mkali hutoka kinywani mwake Ili awapige mataifa Kwa huo. Naye atawachunga Kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadgabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16. Naye ana Jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Ikiwa unapenda kujitakasa Ili usiachwe pale WATAKATIFU watakaponyakuliwa, fuatisha Sala hii:

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, UZINZI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN.

Karibu katika familia ya Mungu 🙏
Weka namba ya simu Mtumishi ili tukutumie faster sadaka zetu za kujimaliza.
 
WATAKATIFU waishio duniani,

Unatukumbusha kutakasa mavazi yetu Ili Yesu arudipo asikuache.
Amina mtumishi
Ila mimi sijielewi, najikuta nakata tamaa tu nasema liwalo na liwe , ila mda mwingine napata hofu kuikosa mbingu, ila mwingne sielewi yani najikatia tamaa tu nikiona labd dhiki kuu nitahimili mateso ikitokea simo unyakuoni.
Yani sijielewi.
 
WATAKATIFU waishio duniani,

Unatukumbusha kutakasa mavazi yetu Ili Yesu arudipo asikuache.

Hayo ni maagizo walipewa watu flan, sio kila agizo la kwenye biblia ni la watu wote ndio maana nakuuliza walipewa watu gani?
 
Ila hii issue ya marejeo ya Yesu kuwa karibu sana unaweza kuwa kweli. Kuna ndoto 2 niliota mwaka 2024 zikihusiana na jambo hilo.

Cha ajabu, kila anga lilipong'aa kwa utukufu wa ujio wake, mimi sikufurahishwa na jambo hilo. Nilihuzunika sana kwamba sikujiandaa kwa ujio wake.

Hizo ndoto nimeshinda kuzielewa kabisa, japo ninaamini ni ujumbe fulani nimetumiwa niufanyie kazi. Eeeh Mungu nisaidie. 🙆
 
Ni Kweli kabisa,

Walio na asili Toka juu, huonekana wendawazimu Kwa wenye asili Toka chini kuzimu.

And vice versa is true.
Mnaenda mpaka kuuziwa udongo eti ni upako, si uchizi huo 😂

Eti kamuona yesu 😂😂😂😂

Una utakatifu gani wa kumuona yesu wewe?! Kutwa unawaza ngono, kujichua, wivu na chuki binafsi. Eti ukamuone yesu 😂😂😂

Jidanganyeni hivyohivyo
 
Back
Top Bottom