Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.
Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.
Sasa polisi wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wale wanaowashuku kuuza au kuvu bangi kisha kuwaua kinyama. Misiba ni mingi mitaani, inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.
Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.
Rais Samia utakuwa na mwisho mbaya. Police wamegeuza Kitonga Dar kuwa machinjio ya binadamu. Hata familia zenu zina vijana wa hovyo, wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road. Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.
NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu, ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, huzuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda uswahilini Tandika na Buza ni huzuni.