Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

HILI LA KUUA PANYA ROaD SIO SAHIHI.. kila mtu asikilizwe na ahukumiwe na sheria mahakamani. Mtu akifa unaweza kumpa hatia yeyote hata kama aliuliwa kwa makosa...
Ile tume ya kuangalia Jeshi letu ifanye kazi kwa haraka..
Uhalifu haujawahi kuisha kwa watu kupelekwa mahakamani. Wacha vijana wakabaji wale ‘Chuma’ tu.
 
Tulisema humu, raia wakasema tunatetea panya road.

Vp watoto wa wakubwa masaki na oyster bay wale wabwia unga nao wameuwawa?
Kuna mtoto mmoja wa kiongozi mkubwa namaanisha mzazi wake yuko kwenye utatu Mtakatifu.
Ni mtukutu sana na lisumbufu, angekuwa Uswahilini naye angepigwa risasi kwa tabia zile.
 
Hapa naona unaingiza watoto wa hao unaowaita wakubwa ili kutafutia huruma wahalifu.

Hao unaosema wanabwia unga wamevamia sehemu na kukata watu mapanga?

Waelezeni watoto wenu na kaka zenu njia sahihi za kujipatia kipato, huwezi kutafuta kipato kwa kuua wengine kinyama na kuwatia watu makovu ya kudumu halafu utegemee huruma.

Huruma hizi zitatuzalia magaidi huko mbeleni.

Bila mkono wa chuma kutumia watoto hawasiki....we unafikiri hao watoto wanaiogopa jela,jela wakienda si wanajua watatoka tu

Ova
 
Hapa naona unaingiza watoto wa hao unaowaita wakubwa ili kutafutia huruma wahalifu.

Hao unaosema wanabwia unga wamevamia sehemu na kukata watu mapanga?

Waelezeni watoto wenu na kaka zenu njia sahihi za kujipatia kipato, huwezi kutafuta kipato kwa kuua wengine kinyama na kuwatia watu makovu ya kudumu halafu utegemee huruma.

Huruma hizi zitatuzalia magaidi huko mbeleni.
Sitetei uhalifu,vnakataa POLICE kiruhusiwa kufanya KAZI ya mahakama.

Tufuate utawala wa Sheria, we huoni Hilo?

Hawa wanachukua pesa zetu Kwa nguvu kwenye miamala ya kibenki mbona hatuwauwi tunaviachia vyombo husika???😠😠😠
 
Wewe nae haueleweki. Hakuna mtu anayefurahia kuona hawa madogo wanadhibitiwa kwa style hii ila ndio namna rahisi iliyopo ya kuwanyoosha. Wewe unadhani vile wanavunja maduka ya watu hata mara 4 kwa wiki na kuacha majeraha na kudhuru watu kuwatia vilema ni jambo zuri?!

Sasa wewe jifanye mwanaharakati za binadamu. Hao vijana unaosema wanajivutia bangi na sio wahalifu wewe una uhakika gani na ushahidi upi namna wanayatumia masaa yao kwa siku?!

Hebu siku tukupeleke kwa watu wenye makovu ya mishono mwilini ujionee hao vijana walivyowatukutu na wasivyostaili kuachiwa waendelee kupumua.

Ugaidi huanza hivi hivi kwa watu kama wewe ambao haujawi pitia au kuexpirience shambulio la hawa wahalifu kutetea kuwa haki za binadamu zinakiukwa.

Kama ni haki yao kuishi pia basi ni haki yao kuishi kwa kuheshimu raia wengine na kutii sheria. Maisha ni magumu kweli na ajira ngumu ila sio excuse sasa yakuwa mhalifu na kudhuru watu wengine.

Hivi wewe mtu anaenyanyua panga na kumkata mtu asiyemjua na hajamkosea lolote kwasababu ana hasira ya ugumu wa maisha na analenga kumnyang'anya mali yake utakuwaje na huruma na mtu wa hivyo?!

Wewe subiria siku mkeo, baba au mama yako, kaka yako, dada yako itokee kashambuliwa na uvamizi wa hawa wahuni uone majeraha ya kukatwa mapanga vidonda vibichi vikitoka damu na mishono ya nyuzi sehemu za usoni ndipo utavuta picha ya ukatili uliofanywa na hawa jamaa na ndipo utajua kwann serikali kupitia jeshi la polisi wameamua kuwa aggressive na hao takataka.

Jambo lingine usije ukadhani askari wanaruka tu kuja kukamata vijana hovyo bila kuwa na background data. Mtoto wako kama ni muhalifu kila mtu atamuona kwa mwenendo wake na tabia na hata hao wahuni wanapokamatwa huwa wanataja wenzao. Ni ngumu muhuni kumtaja mtu asiyemjua na asiye na mazoea nae ambae hawashindi pamoja. Wanapo kamatwa na kutiwa mbaroni sura zao zinatia huruma sana unapowatazama utasema hawa vijana mbona wanaonekana ni waadilifu ni maisha ya kipato cha chini tu yanawapa muonekano mbaya sasa wewe ngoja ukutane nao eneo la tukio la uhalifu ndipo utajua kuwa shetani akimvaa mtu nini huwa kinatokea.

So funga tu bakuli lako na uwe muungwana kwa jamii yako. Nenda hospital ya temeke mwambie nesi naomba unionyeshe majeruhi wa matukio ya panya road then uone kama utaendelea kuongea haya maneno yako ya unafiki.
 
Wao wanapojeruhi, kuiba na kuuwa wanakuwa na inform yoyote?
Kama hayajakukuta hauwezi kujua madhara makubwa ya hawa mbwa.
Huyu hajawahi kukutana na hawa jamaa chobingo wakaanza mtia mapanga bila kosa na kumsaula mali zake. Anakuja kujifanya mwanaharakati. Huyu kama vipi na yeye auliwe na polisi unaweza kuta anashiriki uhalifu huu wa panya road why anakerekwa kusikia unatokomezwa?!
 
Hapa naona unaingiza watoto wa hao unaowaita wakubwa ili kutafutia huruma wahalifu.

Hao unaosema wanabwia unga wamevamia sehemu na kukata watu mapanga?

Waelezeni watoto wenu na kaka zenu njia sahihi za kujipatia kipato, huwezi kutafuta kipato kwa kuua wengine kinyama na kuwatia watu makovu ya kudumu halafu utegemee huruma.

Huruma hizi zitatuzalia magaidi huko mbeleni.
Hawa wanaowatetea panya road natamani siku wakutane nao watalelewa. Me wamempora simu shangazi yangu, mama mtu mzima wa miaka 70 wamempiga na bapa za panga alfajiri tu asieee .

Sasa nadhani watu hawajui ubaya wa hawa vijana hadi wakutane nao kwenye eneo la tukio.
 
Habari!
Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.
Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.
Sasa police wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wanavuta bangi kisha kuwaua kinyama.
Misiba ni mingi mitaani. Inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.
Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai,. Upelelezi wa kutosha umefanyika ?
Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia .
Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.
RAIS SAMIA utakuwa na mwisho mbaya.
Police wamegeuza KITONGA Dar kuwa machinjio ya binadamu.
Hata familia zenu zina vijana wa hovyo wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road.
Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.
NB: Mimi si mhalifu, ni mtumishi wa umma safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, hudhuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda Uswahilini Tandika na Buza ni hudhuni.
Tuache police wafanye kazi yao, tumewasema sana hapa, na hao police wanawajua vizuri hao vijana na wao ndio wanaowafuga. Tunaihitaji mfano wa maangamizo ya kweli Kwa hao panya road ngedere, Dj Santana waue waue, hakuna kulea ujinga. kibiti , rufiji na mkuranga mbegu yake ndio huanza kama hao panya road.

Police timizeni wajibu ueni hao wote msiache hata mmoja
 
Habari!
Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.
Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.
Sasa police wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wanavuta bangi kisha kuwaua kinyama.
Misiba ni mingi mitaani. Inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.
Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai,. Upelelezi wa kutosha umefanyika ?
Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia .
Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.
RAIS SAMIA utakuwa na mwisho mbaya.
Police wamegeuza KITONGA Dar kuwa machinjio ya binadamu.
Hata familia zenu zina vijana wa hovyo wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road.
Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.
NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, hudhuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda Uswahilini Tandika na Buza ni hudhuni.
Walikua wameshaanza kuota mapembe na kuuwa watu
 
Hawa wanaowatetea panya road natamani siku wakutane nao watalelewa. Me wamempora simu shangazi yangu, mama mtu mzima wa miaka 70 wamempiga na bapa za panga alfajiri tu asieee .

Sasa nadhani watu hawajui ubaya wa hawa vijana hadi wakutane nao kwenye eneo la tukio.
Pole sana, bt kuua so Suluhu, JAMII na Serikali ,wazazi tukae kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto hizi.
 
Wewe kama kijana unajua vizuri operation linaloendelea sasa ni kuwasaga 'panya road' halafu wewe bado unakaa maeneo hatarishi usiku mkubwa eti unavuta bang.

Polisi haiwezi kutofautisha kibaka na mvuta bangi endapo utakutwa usiku sehemu isiyoeleweka na ukaamriwa ujisalimishe kisha ukatoka nduki lazima risasi zikuhusu mkuu.

Siungi mkono mauaji ya aina yoyote yale ila kipindi hiki cha operation maalum tujihadhari sana na kuzurura usiku pasipo sababu inayoeleweka.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kesho yako au ya ndugu yako huijui.
 
Back
Top Bottom