Kwa hiyo bw Robert, ukikutwa na na panya road, adhabu yako ni kifo?
Huwa nasoma makala zako nakuona kama ni mtu mbobevu,
Kumbe unashabikikia uuwaji wa watuhumiwa,?
Mahakama zifutwe ili police watoe hukumu kwa watuhumiwa,
Hakuna sehemu nimesema wauawe,
Ingawaje hao Vijana ukicheza nao Kwa kuwabembeleza wanaweza kukutoa roho kiutani utani.
Nimeshashuhudia matukio kama matatu ya hao panyaroad, najua vile wanavyo react wanapokutana na Polisi.
Kama watashindwa kujisalimisha Kwa polisi alafu wanawashambulia polisi ili wakimbie unategemea nini kitatokea?
Sishauri watu wauawe na polisi bila kufuata sheria lakini nafahamu zipo Ajali katika Kazi pale polisi wanapokabiliana na hao Vijana.
Polisi lazima wazingatie sheria,
Lakini kuna wakati wahalifu hutumia udhaifu wa sheria hiyohiyo kuwadhuru Polisi,
Wale waliouawa bila Shaka ni kwaajili ya kuwaogopesha Panyaroad wengine ndio maana Hali itatulia Kwa Muda.
Lakini amini usiamini wezi na panyaroad wa mtaani hawaogopi mahabusu.
Mbona kila wakati wanapelekwa na kutolewa,
Maeneo Kama Banana, airport, vingunguti, mpaka unatokea Buguruni wapo Vijana wahuni wanakamatwa kila leo Kwa matukio ya kihuni hata kabla haya ya panyaroad ya juzi.
Tatizo ni kuwa hawaogopi jela kwani wanatolewaga wanachoogopa ni kifo tuu.
Ukiwatishia kuwakamata kwao sio tatizo, Ila ukiwatishia Uhai wao hapo lazima wapoe.
Approach iliyotumiwa na Jeshi la polisi kuanza Kwa kuua Wale sita ilikuwa nzuri, ili kuwatisha panyaroad, na wametishika.
Lakini kama wangeanza na kukamata Kwanza ninakuhakikishia bado matukio yangekuwa yanaendelea Kwa baadhi ya Maeneo.