Unyama uliofanywa na vyombo vya Ulinzi na Usalama

Unyama uliofanywa na vyombo vya Ulinzi na Usalama

Eti kuna wapuuzi wanakuambia tz ni nchi ya amani, amani ipi hiyo wanayozungumzia kama watu wasiokuwa na hatia wanateswa na kuuwawa?
 
Maandamano ya amani hawayataki wanauwa watu iliyobaki ni kufanywa sunna tu na faradhi ikibidi
Mimi nashauri watanzania wote tufanye tuwasomee duwa hawa washenzi Mungu atatusikia tu , mimi kila siku nikitoka kubeba boksi lazima nimsomee Jiwe dua ya viongozi dhalimu , jeuri ndio nilale yaani wote tukifanya hivyo damu za waliokufa hazitapotea bure . Kama watu hamuijui niwawekee hapa nikumgonga duwa Jiwe na ka Hussein Mwinyi Mpaka wabroo .
 
663B1664-8D60-4E64-952B-9BC3EE2A70FC.jpeg
 
Mzee wa historia Bw.Ameir ambae ni miongoni mwa waathirika wa matukio ya uchaguzi wa Oktoba 2020.

Majeraha hayo yametokana na kipigo na mateso aliofanyiwa na vyombo vya ulinzi wanaolipwa kwa kodi ya Wananchi akiwemo Mzee Ameir ambae hajawakosea jambo lolote kachukuliwa kwake wakampeleka wanako kujuwa wao na kumfanyia unyama huo. Mzee Ameir hapungukiwi miaka 80 kwa kukisia.

Allah ndie mlipaji
View attachment 1632457

View attachment 1632458
Ni wazi Hawa wameumizwa Sana Kama video hii ni ya kweli....Mungu awalinde kwa kweli...ila waliumizwa wakiwa nyumbani kwao au kwenye matembezi yao mitaani?!
 
Ni wazi Hawa wameumizwa Sana Kama video hii ni ya kweli....Mungu awalinde kwa kweli...ila waliumizwa wakiwa nyumbani kwao au kwenye matembezi yao mitaani?!
Sikiliza hii clip

 
Siamini hata kdg kama vyombo vyetu vya ulinzi na amani vinaweza kuonea watu bure, HAPANA. Lazima kuwe na sababu, kutofuata amri au maelekezo: Mkiambiwa fuateni utaratibu hamsikii, mnataka vurugu, kutaka kuiingiza nchi kwa machafuko. Dawa ya moto ni moto, hapana chezea amani yetu, kaa mbali na chokochoko. Kuna baadhi ya watu wamelewa kwa ajili ya amani, siku tukiingia kwenye vurugu kama Libya tunaanza kujuta. Lazima amani, utulivu na mshikamano wetu ulindwe kwa nguvu zote.
Uko sahihi, mshikamano wenu lazima ulindwe kwa nguvu zote. Mshikamano wenu ni legelege na bila kutumia nguvu ya ziada utaporomoka. CCM ulisha sambaratika kitambo, ni gundi ya NEC, TISS na police iliobaki kuinatisha pamoja. Ni muda nayo itaishiwa nguvu.
 
Yule mwanafunzi alipatwa na risasi bahati mbaya, ila chanzo ni maandamano ya chadema. Ndo maana wana kesi.
Nao chadema waliandamana kwenda kwa mkurugenzi kupata vibari vya mawakala wao, nae mkurugenzi alikataa kuwaapisha mawakala kwa sababu aliagizwa toka juu, nao walioko juu waliogopa kushindwa uchaguzi kama utaendeshwa kwa uhuru na uwazi, nao uchaguzi hauendeshwi kwa uhuru na uwazi kwa sababu wananchi wameichoka CCM.......
 
Hakuna askari mzee, labda kachoshwa na maisha, au alidanganya umri wakati wa kuajiriwa. Askari wa mstari wa mbele hustaafu at 55yrs. Uzee ni kuanzia 60 yrs.

Itakuwa hukuelewa hata niliyemjibu amekimbia kaelewa
 
Sikiliza hii clip


Nimeisikiliza...Kama kweli idadi ya vifo ni kubwa na mateso mengi ni jambo baya..
Lakini swali ni kuwa maafa yalitokea majumbani au mitaani/barabarani? Halafu maalim atafanya jambo la maana Kama ataite belea pia familia ya Askari yule aliyechinjwa Kama kuku
 
Nao chadema waliandamana kwenda kwa mkurugenzi kupata vibari vya mawakala wao, nae mkurugenzi alikataa kuwaapisha mawakala kwa sababu aliagizwa toka juu, nao walioko juu waliogopa kushindwa uchaguzi kama utaendeshwa kwa uhuru na uwazi, nao uchaguzi hauendeshwi kwa uhuru na uwazi kwa sababu wananchi wameichoka CCM.......
Kwani ni LAZIMA kuandamana kudai vibali? Walikuwa na kibali cha maandamano? Haya ndo tunayosema kila siku, Fuateni utaratibu!! Vinginevyo mtaendelea kulalamika kuonewa, wakati hamfuati utaratibu. Na usipofuata utaratibu, utapigwa tu!
 
Back
Top Bottom