Unyanyasaji kwenye ubalozi wa Marekani

Unyanyasaji kwenye ubalozi wa Marekani

Asanteni kwa cheko na heko mlilonipa wote mlioandika kwenye huu uzi khaaa.....

Maana hadi mmoja wa mods ameweka emoji ya kicheko kwenye moja ya quote.

Pole mtoa mada kwa yaliyokusibu. Kila la kheri kwenye safari yako ya USA Baby....

Wacha nimtaarifu Raisi wa wabeba boksi USA ajiandae kukupokea jimbo utalofikia....😄😄😄😄😄

Wakati muomba visa ya US ana henyahenya na hekaheka za kuoata VISA, wenye ubalozi wao na nchi yao wamekaa paleee wanakuchungulia....😂😂😂😂😂.



Tafadhali uje kutupa mrejesho ukifanikiwa kupata VISA ama hata wakikunyima. Uje utuelezee na utaratibu wa kule ndani na namna unahojiwa....🤣🤣🤣🤣🤣🤣.
 
Nafikiri tunaweza kuwapelekea Locker na bench moja na tuandike kuwa; Msaada huu umetolewa kwa hisani ya wananchi wakereketwa wa Tanzania
Wangepata cha kujifunza

Hiyo ni fursa, wako wengi wanaenda pale hawajasoma maelezo mtandaoni wanakuwa na simu saa pochi na vyote hivyo haviruhusiwi.

Angetokea mtu achongeshe kabati la loka hata 60 na funguo zake achaji kwa saa ama flat rate kuhifadhi vifaa vyote ambavyo mtu haruhusiwi kuingia navyo ubalozini. Atapiga hela sana, tena akae kwa wale wenye maua baada ya ukuta wa nyumba za Tanesco na mwingine akae kwenye ule mgahawa ulio opposite na Kituo cha Polisi.

Haya wadau mchangamkie fursa hiyo.

Maana pale ubalozini kila leo watu wanaenda kuomba visa.
 
Sasa si mnawashobokea sana, hebu acheni kwenda huko muone kaama watakuwa na maringo.., fanyeni kila kitu online, labda unaenda kutalii
 
Kuna unyanyasaji nilioushuhudia ubalozi wa Marekani nilipoenda kushughulikia visa.

Kwanza pale getini, unaambiwa unaacha kila kitu huingii na chochote! Ila cha kushangaza, hawajaweka hata sehemu ya kuhifadhi mkoba au simu. Sasa sijui wanategemea ukienda huko usiende na pochi? Na je simu unamwachia nani?

Zamani wakati visa zinashughulikiwa ubalozi wa Uingereza, kulikuwa na lockers nje unaweka simu yako na kupewa kikaratasi. Sasa hawa binafsi sijawaelewa.

La pili; Ukishaingia ndani ya compund, nje ya ofisi zao, mnapanga foleni hapo nje mmesimama, hakuna hata benchi la kukaa! Iwe mvua liwe jua! Nikajiuliza je, na wenye ulemavu inakuwaje? Wanashindwa nini kuweka shed fulani na benchi angalau watu wakae?

Kutafuta visa ya Marekani ni kama kutafuta ruhusa ya kwenda mbinguni, wakati wao, wanaweza hata kupata visa airport! WHY?

Naamini wakiambiwa wanaweza kujirekebisha. Hakuna sababu ya kutunyanya kiasi hicho!
Kwa unyanyasaji huo UNGEJIONDOKEA ZAKO TU NA KUJISEMEA " KWANI NIMEFUKUZWA KWETU TZ"

UNGESUSA INGELETA HESHIMA SANA
 
SHUT UP! Ni visa ya mkutano walionialika wao! Kama shule, nilishamaliza zamaniii! Na kama marekani, nilishaenda naijua. Hivyo sina cha kupapalikia. Wananihitaji wao siyo mimi nawahitaji! Get it clear!
Pole mkuu.

Imagine wanakuhitaji na ndiyo wameku harass namna hiyo...

Mi ningesusa siendi! Yani mnihitaji nyie halafu nataka kuja mnaniwekea uzibe?
 
Dah! Watanzania! Kwa hiyo, mnadhani nadanganya? Na je, ofisi zetu zikiiga hayo, ni sahihi?

Haya, I rest my case!

Iweee hii ni JF get used to it aahahahaa

Wacha nikuitie kaka yako Baba Bataringaya walau akupunguzie machungu kwa kukupa hinti za hapa na pale za USA Baby....

Baba Taibaliiiiii..... RRONDO njooo huku umsaidie iweee nabonaituu....😄😄😄😄

By the way nobody says you are lying, just keep sharing your experience please, actually you are helping people silently and they are not telling you, this is JF.....😅😅😅.
 
Pole mkuu.

Imagine wanakuhitaji na ndiyo wameku harass namna hiyo...

Mi ningesusa siendi! Yani mnihitaji nyie halafu nataka kuja mnaniwekea uzibe?

Hawa watu wanajielewa wenyewe....

Wanaweza kuwa wanakuhitaji na bado visa wakakunyima vilevile...😅😅😅
 
Hawa watu wanajielewa wenyewe....

Wanaweza kuwa wanakuhitaji na bado visa wakakunyima vilevile...😅😅😅

Hapa tatizo siyo wao bali ni sisi. Tunawanyenyekea sana.

Mimi kwa kweli kama wao ndiyo wameniomba niende halafu Ubalozini kwao wananiwekea zengwe Wala nisingehangaika kubembeleza..
 
Kuna wakati nilihudhuria semina fulani ya taaluma yangu hapo ubalozini kwao. Huo ulinzi ni balaa, unakaguliwa mara tatu ndio uingie ndani kabisa uliko ukumbi wa mikutano. Ilifika zamu yangu kukaguliwa na ile mitambo yao nikapigiwa king'ora na mtambo wao, ikabidi niwekwe pembeni kwa ukaguzi zaidi. Kumbe ni bakoli ya mkanda tu ndiyo iliyopigiwa king'ora na mtambo wao, sikuwa na silaha au kitu cha hatari. Kwa ukaguzi niliofanyiwa peke yangu nilifedheheka sana japo sikuvua nguo ila nilimbezewa scanner mwili mzima
Pale hata kutembea unatembea kwa kufata mstari aisee acha tu
 
Pale hata kutembea unatembea kwa kufata mstari aisee acha tu
halafu kwa pembeni kuna zungu limevaa kijeshi liko busy na mitambo ndani ya kichumba kama strong room sijui linarekodi nini na kutuma taarifa kwao
 
Back
Top Bottom